Robin Van Pesie - Niende wapi?????? |
Ni wapi ambapo RVP atacheza msimu ujao???
Robin Van Persie yupo katika hatari ya kuishiwa machaguo - na huku Arsenal wakiwa wanakaribia kukamilisha rasmi usajili wa Santi Cazorla, hali inazidi kuwa mbaya kwa upande wake.
Van Persie ana klabu tatu ambazo zinamtaka: Juventus, Manchester City na Manchester United.
Juventus wameanza kukata tamaa ya kumsaini, wameshatuma ofa ambayo tayari imeshakataliwa na Arsenal na wapo tayari kumpa RVP mkataba wa miaka 5 na mshahara wa £190,000 kwa wiki baada ya kodi.
Lakini huku mabingwa hao wa Italia wakiwa katika hatihati ya kocha wao kufungiwa kwa kutojkna kuhusishwa na kashfa ya upangaji wa matokeo wa mechi, hivyo suala hili linampa wakati mgumu Van Persie kwenda Turin.
Juventus walianza kwanza kutuma ofa ya kiwango chini ambayo ilikataliwa na na Arsenal, wamerudi tena na ofa nyingine ambayo bado haijafikia kiasi cha fedha ambacho Arsenal wanahitaji.
Manchester United wanaonekana kujiamini wakiwa nyuma ya pazia lakini hisia kwamba hawatoongeza ofa yao pamoja na kwamba ofa yao ya mwanzo inayokadiriwa kufikia £15 millioni kupigwa chini na Arsenal.
United wanaelewa fika kwamba van Persie anatimiza miaka 29 mwezi huu, ana rekodi mbovu ya majeruhi na thamani yake ya kuuzwa tena baada ya kusajiliwa na timu mpya kutoka Arsenal inaweza kukaribia na kutoka patupu. Haya yote yapo kinyume na sera ya uhamisho ya klabu ya akina Glazers.
Labda United wanahisi kwamba Arsenal watalazimika kupunguza bei wakati mwezi huu ukiwa unaishia kwa kuwa wanaweza kuwa radhi kumuuza chini ya £20 millioni kuliko kumpoteza bure msimu ujao wakati mkataba wa Van Persie utakapokuwa unaisha.
Pia inaaminika kwamba van Persie havutiwi na Manchester City - japokuwa tayari wameshatuma ofa kwa ajili yake. City wanaelewa juu ya klabu yao kutomvutia RVP na ndio maana wanajaribu kuangalia namna ya kuweza kumsaini wabadala kama Gonzalo Higuain.
Gonzalo Higuain - Mbadala wa Van Persie @Etihad Stadium? |
Lakini pia City inabidi wauze wachezaji wake wengi ili wasajili. Uongozi wa klabu hiyo unataka kwanza kuwaondoa wachezaji wanne wanaokula mishahara mirefu kama Carlos Tevez, Emmanuel Adebayor, Roque Santa Cruz na Edin Dzeko kabla ya kununua wachezaji wengine.
Hilo linamuacha van Persie njia panda. Baada ya mwanzo kabisa kuonekana kuvutiwa na Juventus, wasiwasi wa kumpoteza manager ambaye aliiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa ni habari mbaya. Dalili zote sasa zinamuelekeza Old Trafford, lakini United wapo mbali na fedha wanayoitaka Arsenal ukizingatia mchezaji anakinzana na sera za usajili za klabu hiyo.
Lakini ni jambo lisilofikirika kwa Arsenal kutomuuza kipindi hiki cha kiangazi. Wakati Wenger akionekana kutaka kuendelea kuwa na van Persie, lakini Gunners inabidi wamuuze mdachi huyo. Kingine chochote kitakuwa hakielezeki chini utawala wa sasa mwaka mmoja baadae.
Lakini hilo linamuacha Van Pesie - ambaye ameshasema hatosaini mkataba mpya - katika hali isiyoeleweka.
Je aende City na kupingana na matakwa ya nafsi yake?
Aombe United warudi na ofa nzuri zaidi - japo hilo ni kinyume na sera za usajili za klabu hiyo?
Au aende Juventus, klabu ambayo ipo katikati ya kimbunga?
Juventus siku zote ilionekana itabidi wamshawishi sana Persie ili kuweza kumpeleka Italy. Imekuwa vigumu zaidi sasa.
Huku pia kunaonekana hakuna namna nzuri ya kurudi Arsenal - mashabiki wanaweza kumkataa na kutompa sapoti.
LUKAS PODOLSKI |
Arsenal tayari wameshaanza kujipanga kwa maisha bila Van Persie. Lukas Podolski bado hajapewa namba ya jezi lakini kwa hakika yupo njiani kuichukua namba ya jezi ya Van Persie - namba 10.
Klabu hiyo tayari imeshamnunua Olivier Giroud. Podolski anaweza kucheza kushoto, nyuma ya mshambuliaji au katikati na Giroud na mfungaji mzuri.
Wenger pia atakuwa na machaguo mengine huku Theo Walcott akiwa kulia, Gervinho yupo pembeni bado, huku Andre Santos akiwa anachezeshwa winga ya kulia kwenye mechi za pre-season
Na sasa Arsenal wamebakiza kutangaza tu rasmi kuhusu usajili wa Santi Cazorla. Akiwa na miaka 27 tayari ni mchezaji wa daraja la dunia, akiwa ameshaichezea mechi 45 Spain na kushinda Euro na World Cup, na pia anatajwa kuwa mmoja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa kama ilivyo kwa akina Cesc Fabregas.
Cazorla na Alonso |
Inaaminika tayari Cazorla ameshaini mkataba wa miaka mitano na kupima vipimo vya afya, Wenger anaweza kumtumia Cazorla kama playmaker akipangwa namba 10 katika msimu ujao unaoanza siku chache zijazo.
Pia kuna uwezekano wakampata kwa mkopo kingo wa Real Madrid Nuri Sahin.
Kwa hakika Arsenal wanajenga upya timu yao, maisha bila Van Persie - hata kabla hajaondoka.
Mdachi huyo amekuwa na msimu bora katika maisha yake miezi 12 iliyopita, akifunga mabao mazuri kwa wingi lakini sasa upepo unaweza ukawa umemgeukia.
Nini hatma ya Robin Van Persie - kwa hakika tutafahamu siku chache zijazo..
Nawasilisha - Aidan Seif Charlie
No comments:
Post a Comment