Hatimaye klabu ya Azam FC ya Tanzania imemuuza mshambuliaji wake Mrisho Khalfan Ngassa kwenda klabu ya Simba SC.
Azam ambao walimsaini Ngassa kwa ada iliyovunja rekodi ya uhamisho kwa wachezaji wanaocheza Bongo, Million 55, wamemuuza Ngassa kwa ada ya millioni 25 iliyolipwa cash na mabingwa wa Tanzania Simba.
Akizungumza na mtandao huu meneja wa Azam, Patrick Kahemele amesema kamati ya ufundi ya klabu pamoja na uongozi walikubalina kumuweka sokoni Mrisho Ngassa mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Kagame Cup ambayo iliisha kwa Azam kushika nafasi ya pili nyuma ya Yanga.
"Klabu iliamua kumweka sokoni Ngassa mara tu baada ya michuano ya Kagame kumalizika, kwa kuwa mwenyewe alionesha nia ya kujiunga na klabu yake ya zamani Yanga, sisi tuliwapa kipaumbele Yanga, lakini pia Simba nayo ilionesha nia ya kumtaka. Tukafungua bid na kutangaza tunahitaji $50,000. Yanga baada ya kuwajulisha juu ya hili wakatuma ofa ya millioni 20, Simba nao wakatuma millioni 25. Ofa zote zilikuwa chini ya kiasi tulichohitaji lakini baada ya majadiliano ya viongozi wote wa Azam tukaona bora tumuuze tu, kwa bei ya millioni 25.
"Kwa kuwa Simba walikuwa wameshafikia viwango na sisi lengo letu lilikuwa ni kumuuza Yanga, asubuhi ya leo tukawatumia email Yanga tukiwaambia waboreshe ofa yao na tukawaambia bid ya Ngassa itafungwa saa saba mchana, lakini hadi muda huo unafika Yanga hawakuwa wametujibu chochote, kitendo ambacho tulikitafsiri hawana nia ya dhati ya kumsaini mchezaji huyo, kwa upande mwingine Simba walikuwa tayari wamefikia dau tulilolitaka hivyo tukafunga bid na kumuuza mchezaji huyo kwa Simba," alimaliza Patrick.
Tunaendelea kumtafuta Mrisho Ngassa na pale tutakapompata tutawaletea taarifa rasmi kuhusu alivyopokea taarifa za kuuzwa Simba.
By Aidan Charlie
hiyo janja yao walishaamua kumpeleka simba ili kumomoa ngassa na yanga.uliona wapi inatangulia ofa ya simba kabla ya tangazo la kumuuza halijatoka?halafu hiyo ofa ya simba haikutajwa kiasi gani hadi yanga walipopeleka ofa yao ndio tunaambiwa simba wametoa milioni 25.Azam wanapaswa kuwa waungwana kama yanga ilivyowauzia ngassa ilipaswa nao wamrudishe walikomtoa,hakuna suala la biashara kwa mchezaji uliyemnunua kwa milioni 58 umuuze milioni 25.huo ushosti wa simba na azam mwisho wake utakuwa mbaya kwa azam,siyo simba
ReplyDelete