Kila mtu ana maoni yake juu ya kinda hili la kibrazili, na huku Kombe la dunia likiwa linaelekea Brazil miaka miwili ijayo ijayo, maisha ya soka yanazidi kumnyookea Neymar.
................................................
Ingeweza kuwa ndoto ya matukio ya kutoka kwenye filamu za miaka ya 1970's za vikatuni, kama isingekuwa mechi ya mchezo wa soka. Tarehe 6, mwezi wa nne, 2011, na Santos wakiwa mbele kwa 2-0 katika mchezo muhimu wa kombe la mabingwa wa Amerika ya Kusini dhidi ya timu kutoka Chile Colo Colo. Mashabiki wa Santos waliojazana kwenye uwanja wa Vila Belmiro walivvalia vinyago vya plastiki vyenye sura ya staa wao mshambuliaji Neymar. Anafunga goli zuri na mashabiki wanainuka kushangilia, mmojawapo ni Robinho, ambaye alikuwa amekaa kwenye jukwaa karibu na mstari wa mpaka wa uwanja, Neymar anakwenda kushangilia mbele ya mchezaji mwenzie huyo Brazil, na Robinho anampa kinyago, Neymar anakivaa juu chini, na anaendelea kushangilia.
Vuta hisia: mchezaji maarufu kabisa nchini Brazil, amevaa kinyago cha sura yake juu chini, huku akiwa anashangiliwa na maelfu ya mashabiki waliovaa vinyago swa nae yeye.
Neymar akiwa na kinyago cha sura yake |
Ushangiliaji huu ghafla unageuka mchungu. Kushangilia na kinyago ni kinyume na sheria; adhabu yake ni kadi ya njano. Na huku Neymar akiwa ameshapewa kadi ya njano kabla, anapewa nyingine kwa kuvaa kinyago na kutolewa nje. Colo Colo wanarudisha magoli yote mawili lakini Santos wanajitahidi na kupata goli la ushindi na mchezo unaisha 3-2. Ushangiliaji wa kuvaa vinyago kwa mashabiki ulibuniwa na shabiki na mwandishi mmoja nchini Brazil, lakini aliyetoa fedha za utengenezaji wa vinyago hivyo alikuwa mdhamini mmojawapo wa Neymar.
"Niliudhiwa na kitendo kile cha kupewa kadi, kwa sababu kuvaa kinyago cha sura yangu sikumuumiza mtu wala sikumfanyia mtu yoyote dharau," alimwambia mwandishi wa jarida la Lence mwaka jana. "Sikustahili kupata kadi, lakini hizo ndio sheria."
Usiku mwingine, mechi nyingine, na kichwa kingine cha habari kwenye maisha ya Neymar da Silva Santos Junior, mwenye 20.
....................................................................................................................................................................................................
Macho yote kwa Neymar, na sasa ndio kabisa. Ndio mchezaji muhimu zaidi kwenye mashambulizi ya Brazil, na alionyesha umuhimu wake kwenye michuano ya Olympic iliyomalizika hivi karibuni ambayo walifungwa na Mexico kwenye fainali, huku wakiitumia michuano hiyo kama matayarisho ya World Cup 2014.
Neymar amekuwa akitizamwa na maskauti kutoka vilabu vyote vikubwa barani ulaya, kuanzia Manchester City, Chelsea, Juventus, Real Madrid mpaka Barcelona, huku wote wakiwa na matumaini ya kushinda mbio za kupata saini ya kinda hilo linalokuja kwa kasi kwenye soka.
Mjadala mkubwa nchini Brazil sasa unahusu kama ni sahihi Neymar kwenda kujiunga na timu kubwa ulaya ili kuongeza makali yake kwa ajili ya kuisadia Brazili kwenye kombe la dunia 2014. "Nafahamu kuna maskauti wengi kutoka ulaya ambao wanahudhuria mechi za Santos huku wengine wakisafiri kila timu ya taifa inapoenda."
Lakini wakati dunia nzima ikizidi kumuangalia Neymar na kumfananisha na Messi, nchini Brazil kinda huyu anaishi ya kisupastaa sana muda wote akizingirwa na kufuatwa fuatwa na waandishi wa habari na mashabiki wake. Kila anachofanya Neymar kuanzia maisha yake ya kawaida, soka mpaka binafsi yanaripotiwa kwa undani mno. "Siwezi kwenda sehemu bila mtu kunijua kama mie ni nani. Haijalishi wapi nilipo.Watu wananijua mpaka New York," anasema Neymar. "Kuna mambo mengine ya ajabu yanatokeaga muda mwingine. Kuna siku moja kuna mtu alinisimamisha na kuniambia kama naweza kumpa shati yangu niliyovaa japokuwa haikuwa hata jezi - ilikuwa ya kawaida tu."
Anaweza kuwa na miaka 20 tu, lakini mshambuliaji huyu wa kibrazil mwenye ujuzi mkubwa kucheza soka na kufunga mabao kiasi cha wengine kufikia kumuita 'Messi Mpya' au 'Pele Mpya'. "Neymar ni fundi," anasema Ronaldinho. "Ni mmoja kati ya wachezaji bora hapa Brazil; mchezaji ambaye naamini hivi karibuni atakuwa akicheza kwenye klabu kubwa duniani na atakuwa akigombania tuzo ya kuwa mchezaji bora duniani."
Hata Pele, mchezaji wa zamani wa Santos amekuwa akimsifia sana Neymar na alitoa kauli moja hivi karibuni akisema: "Kabla ya Messi hajawa mkali kama mimi, inabidi awe kwanza mzuri kama au zaidi ya Neymar."
Neymar ana kipaji kizuri kweli kweli, hivi karibuni kwenye mechi ya kombe la mabingwa wa Amerika ya kusini dhidi ya Internacional, aliwadhihirishia ambao bado wana mashaka na uwezo wake. Aliuchukua mpira katikati ya uwanja kasogea nao na kuanza kuwapita mabeki wenye jezi nyekundu za Inter, kabla ya kubaki na kipa na kufunga bao. Muda mfupi baadae akafanya vile vile. Santos walishinda 3-1, huku Neymar akifunga mabao yote.
Santos sasa wanavuna zaidi ya $19million kwa mwaka kutoka mkataba wa jezi, Reuters waliripoti mwezi June. Neymar anapata £936,000 kwa mwezi - kiasi cha pesa ambacho angelipwa ulaya - huku robo tatu ya pesa hizo ikitoka kwa wadhamini, kwa mujibu wa Reuters.
Japokuwa amekuwa akitengeneza fedha nyingi kwa mwaka taarifa za hivi karibuni zinahusiana na vitabu vya mahesabu ya fedha zake zinaonyesha kijana huyu kibrazili anaeleka kwenye kufikilisika. Ni vipi anayetengeneza kiasi cha pesa kisichopungua $10 millioni kwa mwaka afilisike???
Kwa majibu ya maswali haya kaa tayari kukamata kopi yako ya Jarida la Number 10 litakalotoka tarehe 17 mwezi ujao.
By Aidan Seif Charlie
No comments:
Post a Comment