Search This Blog

Tuesday, August 7, 2012

MASWALI YA KUJIULIZA KUHUSU USAJILI WA MRISHO NGASSA KWENDA SIMBA - TUJADILI

Takribani wiki nzima iliyopita kulikuwa na sekeseke la usajili wa winga wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa ambaye ni mchezaji wa Azam FC - washindi wa pili wa VPL na Kagame Cup.

Siku mbili baada ya kombe la Kagame kumalizika klabu yake ya Azam ilimuweka kiungo mshambuliaji huyo sokoni - wakihitaji kulipwa $50,000 kwa klabu inayomhitaji ili kuweza kuwauzia mchezaji huyo ambaye amebakiza mmoja kwenye mkataba wake kumalizika.

Timu za Simba na Yanga zikapeleka ofa ya kutaka kupata saini ya Ngassa, lakini kwa bahati mbaya wakapeleka ofa ambazo hazikuwa zimefikia hata nusu ya waliyoitaka Azam, lakini kutokana na kwamba Azam walikuwa wapo radhi kufanya chochote kwa madai yao ili kumuondoa Mrisho Ngassa klabuni na kutompotezea muda na kukirudisha kipaji chake nyuma ikabidi waamue kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo, na katika hilo Simba wakawazidi nguvu Yanga na wakamsaini Mrisho Ngassa kwa ada ya uhamisho ya millioni 25, huku mchezaji mwenye akipewa ada ya usajili ambayo ina thamani ya millioni 30 (fedha na gari aina ya Verossa). Mabingwa hao wa Tanzania wakatangaza na mchezaji mwenyewe akakiri kwamba amesaini Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

MASWALI
1: Azam FC kupitia viongozi wao wamekuwa wakisema wamempeleka Mrisho Ngassa kwa mkopo Simba wenye umri wa mwaka mmoja. Lakini Simba na mchezaji mwenyewe wanasema wamesainishana mkataba wa miaka miwili. Utata upo hapa, Azam wanasema mkopo  wa mwaka  mmoja  Simba na Ngassa wanasema miaka  2. Je huu ni mkopo au mauzo kamili?

2: Inawezekana ni uelewa wetu finyu wa mambo ya sheria za mikataba ndio unapelekea kuhoji hili. Kwa kumbukumbu zetu za kuhusu masuala ya uhamisho, kitu kama hichi ni kigeni. Mrisho Ngassa bado ana mkataba na Azam FC ambao unaisha mwakani ambao pamoja na mengine yote unatoa taarifa kwamba mchezaji ana haki ya kulipwa millioni 2 kwa mwezi. Kwa mujibu wa Azam FC wamewauzia kwa mkopo Mrisho Ngassa Simba kwa mwaka mmoja, lakini Simba nao wametoa mkataba mpya wa miaka 2 kwa Ngassa ambaye bado ni mwajiriwa wa Azam FC mpaka mkataba wake halali utakapoisha. Sasa je suala hili linatafsirika vipi kisheria, yaani mtu binafsi anaweza kuwa mikataba miwili ya aina moja na pande mbili tofauti kwa wakati mmoja? Kama hapana mkataba upi kati ya Mrisho KhalfanNgassa na Azam FC au Simba SC na Mrisho Khalfan Ngassa ulio halali? Tunauliza tu tunaomba majibu jamani.......

3: Swali tatu na la mwisho ni hivi, Azam FC wana mkataba wa mwaka Mrisho Ngassa ambao uhai wake unaisha mwakani. Kwa kuangalia hilo - Azam hao hao ambao wana mkataba wa mwaka mmoja na mchezaji husika, wamemtoa mchezaji huyo kwa mkopo wa mwaka mmoja(wenye gharama za millioni 25) kwenda Simba. Sasa Ngassa si atacheza Simba kwa mwaka mmoja, na mpaka anamaliza mwaka mkataba wake na Azam si utakuwa umeisha. Kwa maana hiyo Azam na Ngassa watakuwa wamemalizana kwenye kipindi cha miezi 12 ijayo na mchezaji atakuwa huru, au sio jamani! Huu ni mkopo au mauzo kamili??? Tunauliza tu.

Kwa yoyote anayehusika kwa namna moja au nyingine - tunaomba majibu.
By Shaffih Dauda & Aidan Seif Charlie

15 comments:

  1. kisheria inakubalika kwa maana pande zote husika zimeridhia makubaliano, yaani consent ipo. mkataba sio lazima uandikwe ndio uwe halali. ila pia kibiashara ipo, kilichofanyika ni kuwa simba wamenunua mkataba wa mwaka mmoja wa Ngasa na kumwongezea mmoja.

    Mwamba hapa....!

    ReplyDelete
  2. Jambo 1 ambalo lilinishangaza ni hatua ya Azam ya kumpeleka Ngassa kwa mkopo Simba, mkopo wa ada ya Mil 25 huku mshahara wake wa kila mwezi ukilipwa na team iliyokopeshwa hapa ndo utata ulipoanzia,haya gafla baada ya Ngassa kuweka bayana kuwa hayupo tayari kukipiga Simba kwa kupelekwa kama gunia la viazi,Simba wakamtafuta Kijana faster na kuzungumza naye,mwisho wa mazungumzo yale ikaelezwa kuwa Ngassa ameridhia kukipiga na Msimbazi baada ya kukamilishiwa kile lichokuwa anakihitaji Mil 30,Gari Verosa na Mshshara wa Mil 2 kwa mwezi,wakati hilo likielezwa hivyo nilimsikia Ngassa kwa kauli yake mwenyewe kuwa ame'sin kukipiga Simba kumalizia mkataba wake wa mwaka mmoja uliosalia kule Azam na kwamba Simba waliununua huo mkataba kutoka Azam hapohapo tena zikatoka taarifa kuwa mkataba wake wa kukipiga pale Msimbazi ni wa miaka miwili,kuna habari za kutatanisha tena katika hilo,habari nyingine zikisema itaanza baada ya mkataba wa Azam kukamilika ikimaanisha kuwa jumla ya kipindi atakachoipiga pale(kama Allah atajalia lkn) kitakuwa ni miaka mi'3 wakati habari nyingine zinasema miaka miwili aliyo'sign kwa fungu lile alilopewa na gari imejumuisha mwaka mmoja anaomalizia mkopo wa Azam sasa which is which bila shaka ukweli anaujua Kaburu/Rage na Ngassa himself,lkn in whatever the case sheria inasemaje kuhusu hii miaka miwili(whether imejumuisha au haijajumuisha mwaka mmoja wa mkopo wa Azam,je sheria inaruhusu kwa Club kuingia mkataba mpya na mchezaji wakati mkataba wake na team yake ya awali haujakamlika? ikumbukwe (labda Azam waadishe)Azam bado wana mkataba na Ngassa ambao hawakuwa ayari kuuvunja na ndo maana wakamtoa kwa mkopo.
    Kwa mtazamo wangu mimi kuna kila dalili za kina Kaburu kuwa wamecheza blanda kwenye hili sakata,sina shaka yeyote kuwa Ngassa atakipiga Msimbazi ki'halali kwa mwaka huu mmoja(wa mkopo) lkn pindi utakapomalizika waombee asiingie kidudu mtu endapo lolote litaibuka kuhusiana na mchezaji huyu kuna asilimia kubwa Simba wanaweza kuwa losers katika hili.
    Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  3. Habari,

    atleast leo nimeona waandishi wahabari wa Tanzania wameumiza vichwa kidogo. Maswali haya nilitegemea sana wandishi mngewauliza hao simba na Azam badala ya kushabikia tuu. Hili swala la Ngassa Simaba wamelifanya kisisasa ili kuwafurahisha washabiki wao lakini kisheria na nina imani kwamba TFF itatoa maelekezo zaidi ni kwamba mikataba miwiwli haiwezi kusajiliwa TFF yaani mkataba wa Azam amabo upo already and huu mpyaa wa Simba.Hivyo basi yechnically Ngassa ana haki ya kujisajili timu nyingine baaday ya mkataba wake na Azam kuisha na huo mkopo.

    Sasa katika hili ndio nitamuona Ngassa akiingia Yanga mwakani kwa mkataba mpyaa. simba wanajua waliyoyakuta kwa Yondani sasa wanarudia ujinga ule ule. kabla ya mktaba wa Ngassa kuisha na Azam anaruhusiwa kuanza mazungumzo na klabu mpya wakati mkataba umebakia miezi 6 kuisha.

    sijajua tatizo la Rage na simba ni nini kwani wanashindwa kabisa kuelewa vitu basic kabisa kama hivi amabvyo havihitaji kusomea sheria.

    hebu endeleeni kuulizia TFF watoe ufanunuzi zaidi. ila naona uhuni na sifa ndio umetawala swala hili la Ngassa.

    ReplyDelete
  4. Mimi ni mwanachama hai wa Simba SC tena ni mjumbe toka tawi la Mashujaa Tegeta. Ninachoelewa Simba haijaingia mkatataba wa miaka 2 na Ngasa bali ni mkataba wa mwaka mmoja utakaonza kutumika mwakan baada ya mkataba wake na Azam kuisha. Hivi sasa Ngasa yupo Simba kwa mkopo akitokea Azam. Baada ya kipindi chake cha mkopo kukamilika Ngasa ataendelea kuitumikia Simba kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao ameshasain na Simba.

    ReplyDelete
  5. Kaenda Simba kwa mkopo msimu wa 2012/13 na kununuliwa kiujumla kwa msimu 2013/14. Hayo ni maneno ya Kaburu.

    ReplyDelete
  6. hili jambo linachanganywa na maneno tu. Ila kwa sasa Ngasa atatumikia mkataba aliokuwa nao Azam kwa mwaka mmoja, lakini ametolewa kwa mkopo kwenda Simba na ataumalizia mkataba huko. Yawezekana ni tafsiri kama ni mkopo au mauzo ila mkopo wa malipo upo. Walichofanya Simba na Ngasa ni kusainishana makubaliano ya Ngasa kuchezea kwa mwaka mmoja zaidi baada ya huu mkataba wake na Azam kuisha. Pengine huu bado haujawa mkataba halali (bado ni makubaliano), kwa kuwa mkataba huu sidhani kama utasajiliwa na TFF mpaka baada ya miezi 6 ibaki kwa huu wa mwaka mmoja (wa Azam) kuisha. Kwa lugha nyingine mkataba wa mwaka m1 kati yake na Simba bado haujaanza kufanya kazi. Kimsingi sasa Ngasa amekubaliana na Simba kuwa atakuwa hapo kwa miaka miwili kuanzia sasa.

    ReplyDelete
  7. Shaffih kuchangia vizuri ni vema tukajua kanuni za usajili za TFF, kama zipo katika soft copy tafadhali tuwekeeni wazi tuziangalie, hapo ndio utaweza kujadili kwa kina na vizuri. Shaffii tuwekee hizo kanuni za usajili ktk blog yako tafadhali, kwani nimeangalia wesite ya TFF sioni kitu

    ReplyDelete
  8. Hivi Baada ya Miezi Sita (6) Ikitokea Timu ikamsainisha na ikataka kuusajili mkataba huo itakuwaje? Uelewa wangu mdogo wa kisheria ni Kwamba "any agreement which is not enforceable is null and void" sasa mkataba wa simba na ngassa wa mwaka mmoja kuanzia july 2013-June 2014, is it Enforceable?. na kama sio, upi utakuwa sahihi au itabidi tumpeleke Ngassa kwa vyombo vya sheria kwa udanganyifu ? samahani kwa kuchanganya lugha. TFF itengeneze mazingira mazuri ya kuingia kwenye Professional Football, sisi bado tupo kwenye armature tuuuuu na tunakurupuka kwenda kwenye professional wakati hatujajiandaaa.

    ReplyDelete
  9. ndugu shaffih,mimi nina wasiwasi sna na huyu jamaa kaburu,kwasababu kwanza sujui kiwango cha elimu yake,maana uwezi kumsainisha mtu mkataba mpya wakti ukijua umepewa kwa mkopo,na azzam wanakili mpaka leo kuwa ngasa ni mchezaji wao kaenda simba kwa mkopo,kwa masikio yangu tulimuuliza ngasa umeenda simba kwa mkatba upi?akajibu nimeeenda kwa mwaka mmoja kwa mkopo,leo tunasikia miaka miwili?je FIFFA wanaruhusu hili.Hapo ndio utajua hata suala la chombo kaburu kaingizwa mkenge,huyu jamaa ni mfanyabiashara na kaamua kufanya biashara na wachezaji.yeye kaburu angesema tuu kwa mashabiki jamani mimi nimekuwa wakala lakini kwa wachezaji wa ndani tuu,maana haiwezekani mchezaji anakuja anakwambia nisajili sina mkataba unamsajili je?amekuonyesha copy ya mkataba kama umeisha ok labda kakuonyesha feki kwani pale karume ni mbali kwenda kuulizia,kaburu si mjinga anakula nao pamoja hawa wachezaji,chukua 20 mimi kumi,kesho tutajua TFF watakuruhusu wapi,ni kama suala la jeba tuu.Nawasilisha hakuna mchezaji anayepelekwa kwa mkopo na club na ndani ya mkpo akasaini mkatba,hatuoni suala la adebayor pale man city,niwasilishie hili shaffie katika kipindi chako cha sports watu wasikie biashara ya kaburu simba

    ReplyDelete
  10. Shaffii,

    Huwa napatapa shida sana kuona viongozi wa wanatumia uelewa mdogo wa washabiki wao kufanya biashara za kijinga. hata waandishi wa habari wanatumika sana kupotosha ukweli au kutokutaka kuingia ndani zaidi kupata ukweli.

    Huwa napenda sana kuangalia media za Kenya jinsi walivyo professional kuripoti na kukupa malaji habari iliyo kamili. yaani waandishi walitakiwa waande TFF kuzijua zaidi sheria za usajili in details then baada ya hapo watujuze.

    ina sikitisha sana hakuna hata mwandishi mmoja aliyesumbuka kichwa kuzijua hizi sheria baadala yake tunaona wakina Kaburu wanacheza micheo mibaya ya kibiashara kila siku bila kufuata sheria. pole sana wana simba ila pole zaidi wana Tabora cos siamini kabisa mbunge mzima anafanya vitu bila kufuata sheria au anapindisha sheria kwa manufaa yake. sasa je huko bungeni si ndo biashara na mikataba feki imetawala. Rage tafadhari sana heshimu position yako. SWALA la Ngassa mmelifanya kishabiki sana mkifikiri mnawakomoa Yanga kumbe mmejikomoa wenyewe.

    TFF please toeni ufanunuzi na wewe shaffii fuatilia hili kwa mapana.

    ReplyDelete
  11. Swala hilo liko wazi na wala hakuna utata hapo! mchezaji anayepelekwa timu nyingine kwa mkopo halipiwi ada ya uamisho! katika suala hili timu ya Azamu ndio wanaochanganya watu tena kwa makusudi. Kama walikubali ada ya uhamisho ya sh. 25,000/- (buy out clause) maana yake wamevunja mkataba na Ngasa na timu iliyolipa ndio yenye haki na mchezaji husika. kwa maana hiyo Ngasa yupo Simba kihalali kwa mkataba wa miaka miwili na si mkopo.

    ReplyDelete
  12. Hilo mbona liko wazi Shaffih,Ngassa kapelekwa Simba kimkopo na kwakua mkataba wake unakwisha mwakni na Azam so Simba wakaamua kumpa mkataba kabisa wa 2013/2014 na ndio maana Simba na Ngassa wamesema atakupo Mscmbazi kwa miaka miwili so Yanga imekula kwao

    ReplyDelete
  13. Wadau kama simba imemnunua Ngassa basi Azam wasidanganye uma kuwa wamemtoa kwa mkopo simba. Na hapo kama ndio hali halisi basi tunamashaka na biashara hiyo ambayo ilitakiwa kuwa ya uwazi na kutoa fursa kwa timu yoyote kumnunua ngassa. Kama Simba imemchukua kwa mkopo na kumpa mkataba (up-front) hiyo kisheria kuna utata kidogo. Kama kuna mkataba ambao una exist basi ingetakiwa kuwe na addendum (maboresho ya mkataba wa awali) ambao sasa ni Azam na Ngassa. Tusiangalie kishabiki bali tuone kuwa kuna haja ya semina elekezi zitolewe kwa wadau wotye wa soka na vijarida/vipeperushi ili viongozi, wachezaji, na wadau kwa ujumla wazijue taratibu za "PROFESSIONAL FOOTBALL".

    Hivi sasa tunababaisha tuuuuu na hatutatatua haya matatizo. PIA TFF na vyombo vyake viwe na meno ya kuwaadabisha wale wote watakao kiuka (Wahuni) taratibu hizi.

    Wanahabari tusaidieni kwa hili, ili tuingie kwenye Ueledi wa soka kikweli kweli.

    ReplyDelete
  14. kwahakika viongozi wasimba na azam wameamua kwa maksudi kabisa kuupotosha umma. mpaka sasa ni kwamba usajili wa ngasa kwenda simba ni batili kwani nijuavyo ni kuwa kipindi cha uhamisho kwa wachezaji wenye mikataba na vilabu vyao kimeshapita na iliyopo sasa ni kilabu kumpeleka mchezaji timu nyingine kwa mkopo huku club yenye mkataba husika ikiendeleea kuwajibika juu ya mchezaji husika katika kila kitu. pili mkataba walioingia simba na ngasani batili kwani haiwezekani kwa timu yoyote kuingia mkata au hata kuzungumza na mchezaji kuhusu kuchezea timu husika akiwa amebakiza mkataba wa zaidi ya miezi sita. kwa hili simba wamechemka na aidha watakuwa tu wamefanya IGIZO ili kuwafurahisha washabiki wake na kupooza machungu ya kuboronga kagame wakati wakielekea kwenye mkutano mkuu. tuwatahadharishe tu wanamsimbazi kuwa wasishangae yatakapotokea yale ya yondani kwani timu yoyote inaweza kuipiku simba na kumsainisha ngasa mkataba halali inapobakia miezi sita mkataba wake na azamu kumalizika. kwa kipindi hiki pia ikitokea timu kuweka pingamizi uasjili wa ngasa simba itakuwa sahihi kabisa kwani hakuna mchezaji anayeuzwa kwa mkopo timu kwa gharama ya milion 25 pia ikumbukwe azam waliweka bayana ngasa anauzwa na kuiita ni biashara na yeyote mwenye dau kubwa atampa ndio maana simba ilipotoa dau kubwa kuliko la yanga ilifanya biashara. yawezekana watanzania hatulielewi kiswahili vizuri hivyo kushindwa kutofautisha mkopo( kitu kilichotolewa bila malipo) na biashara ya millioni 80(uds50) iliyokuwa bei halisi ya ngasa kabla simba kupunguziwa na kuuziwa milloni 25

    ReplyDelete
  15. Kutoa mkopo kuomba sasa katika fredpetersonworldloan@yahoo.com

    ReplyDelete