Search This Blog
Friday, August 10, 2012
LUCAS MOURA ALETA KIZAIZAI KWENYE SOKO LA USAJILI - AS ROMA WASEMA DE ROSSI ANAUZWA KWA ZAIDI YA €100 MILLION, SANTOS WASEMA NEYMAR NDIO HAGUSIKI KABISA
Siku moja baada ya mchezaji wa kimataifa wa Brazil anayeichezea Sao Paolo Lucas Moura kusajiliwa kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekdi kwenye soko la usajili nchini Brazil kwenda Paris Saint Germain, marais wa vilabu vingine duniani wameanza kutoa kauli ambazo zitaleta gumzosana kwenye soko la usajili duniani.
PSG wametumia kiasi cha £150 millioni katika kipindi cha mwezi mmoja kufanya manunuzi ya kuwasajili Lucas Moura, Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva.
Matumizi ya namna hii yameanza kuwatia vichaa baadhi ya viongozi wa vilabu vingine, Kwa upande wa AS Roma ambao mchezaji wao Daniele de Rossi amekuwa akitakiwa na Manchester City nao wameingia tamaa.
Akiongea mkurugenzi wa Roma Walter Sabatini mara laipoulizwa juu ya thamani ya Rossi, akaanza kwanza kuzungumzia mchezaji wa Fiorentina Stevan Jovetic ambaye aliwekwa kwenye thamani ya €30 million na klabu yake, na Napoli nao ambao walisema mchezaji wao Edinson Cavani alikuwa na thamani ya €100 million kwa timu ambazo zilikuwa zinamtolea macho.
"Gharama ya De Rossi ni juu zaidi ya majina yote uliyoyataja hapo juu, kwani maana hiyo Rossi ana gharama zaidi €100 miilion na zaidi." -Sabatini
Ikiwa na kiungo huyo mwenye miaka 29 atakuwa na gharama hiyo , unadhani mchezaji ambaye anatajwa kuja kuwa na kiwango kikubwa kuliko wote, Neymar atakuwa thamani ya fedha ngapi?
Kwa mujibu wa raisi wa Santos Luis Alvaro, amesema baada ya Lucas Moura kuuzwa kwa bei ya €45 million huku alilipwa mshahara wa £250,000 kwa wiki, basi bei ya Neymar haielezeki - yaani anaweza hata asiuzike.
Neymar kwenye mkataba wake ana kipengele kinachomruhsu kuuzwa endapo klabu inayomtaka itatoa £57 million.
Lakini baada ya Moura kuuzwa kwa bei chafu bei hiyo ya Neymar inaweza ikapanda maradufu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Nadhani soko la usajili linakoelekea ulaya ni uwenda wazimu haya ni mameno ya arsene wenger na mimi nakubaliana naye hiyo yote inakuja kwa sababu hawa jamaa wa middle east wana pesa hawajui hata wazifanyie nini mtu kutoa paundi millioni 50 na mshahara wa paundi 250,000 tax free kwa wiki si kitu wakati kuna watu dunia hii hata riski ya kutia mdomoni hajui hatapata wapi ila sio ishu.
ReplyDeleteMoura ni mchezaji mzuri ila kuhamia kwake Parc Des Princes mawili yanaweza kutokea,tunaweza kuona kupotea kwa kipaji ambacho pengine kilikuwa hakina mwisho hiyo yote ni kwa kutoka na maslahi mazuri anayoyapata katika umri mdogo ikamkosesha changamoto na mandhari ya paris pia kwa ujumla au la kuhamia kwake PSG inaweza ikawa changamoto tosha kwake kutaka kufanya vizuri na ikawa faraja kwa watazamaji kuona mchezaji wa kipaji chake anafikia uwezo wake anyways time will tell ila kwa wale waliobahatika kuona michuano ya olimpiki inayoendelea London kati ya Lucas Moura na Oscar naamini Oscar ndiye anayeweza kustahili ada ya uhamisho wa Lucas Moura kwenda PSG,after 2 or 3 season nadhani chelsea watarudi nyuma na kusema bei waliomnunulia Oscar ni kama vile wamempata bure au pia naweza nikawa nimekosea ikawa PSG wenye kusema hivyo juu ya Moura all in all they are 2 guys of outstanding talents.
hapo mkuu umeongea kweli kabisaa!hawa jamaa hela zao wanashindwa kuzitumia vizuri sasa,hasa ukizingati jamaa zao huko wengine wanakufa hata senti hawan! lakini yote ndiyo maisha ya soka tu! waarabu na hela zao za mafuta hizi wana uwezo wa kuwanunua wachezaji wanaowataka ila saa nyengine sasa wanatia chumvi zaidi! angalia zile hela alizotumia mansour ktk usajili wa mwaka jana! dah we acha tu yaani wewe unafikiria hata hiyo ya kula leo tu miujiza wao wanabadilishia wasenge tu!
ReplyDelete