Search This Blog

Wednesday, August 29, 2012

LIONEL MESSI NDIO MWOKOZI WA KIWANGO CHA WAYNE ROONEY - FAHAMU KWANINI?

  
Miaka miwili iliyopita, Wayne Rooney alikuwa on fire na akawa anatajwa kuwa anaweza kuwa mchezaji bora wa dunia muda mchache kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia.

Rooney alikuwa ndio mchezaji aliyefunga mabao megni nchini England kwa jumla akifunga mbao 34 kwa klabu yake ya Manchester United na msimu ulipoisha akachaguliwa kuwa mchezaji wa ligi kuu ya England - wiki mbili kabla ya WOZA 2010.

Alikuwa yupo katika top 3, lakini kiwango chake kibovu alichoonyesha kwenye michuano ya WOZA 2010 iliyofanyika South Africa kikamuondoa katika orodha ya washindani wa juu.

Mpaka muda wa kutajwa kwa washindani wa wa tuzo ya Ballon d'Or wanatajwa, Rooney alikuwa ni mmoja tu ya wachezaji waliowekwa kukamilisha idadi inayotakiwa.

Lionel Messi akaitwaa tuzo hiyo baadae kwa kuwashinda wachezaji wenzie wa Barcelona Xavi na Andres Iniesta.

Mwaka mmoja baadae, Messi akatajwa tena mchezaji bora wa dunia kwa mara pili na mwaka huu anategemwa kupiga hat trick ya tuzo ya uchezaji bora wa dunia.

Baada ya kutupia mabao 82 msimu uliopita akiwa na klabu yake ya Barcelona  na nchi yake, Messi anastahili kuwa kwenye category ya peke yake.

Messi alifunga mabao 14 na kuweka rekodi kwenye champions league msimu uliopita, mabao matano kati ya hayo aliyafunga kwenye mechi dhidi ya Bayern Leverkusen kabla ya mwishowe Barca kutolewa na Chelsea kwenye nusu fainali.

Amekuwa akijitoa akivuja jasho kwa ajili ya mchezo aliochagua, mbele ya mashabiki maelfu amekuwa akicheza kwa juhudi sana na ku-produce kiwango bora kabisa kwa ajili ya jezi ya Blue na nyekundu ya klabu yake ya Catalunya. Hali yake hiyo ya kujituma haijashuka, bado amekuwa ndio kiongozi wa mashambulizi ya Barca.

Wakati wa mapumziko ya msimu hapa kati kati aliwaacha wazi midomo mashabiki wa Brazil baada ya kuwapiga hat trick kwenye mechi ya kirafiki.

Akarudi Barcelona na akaanza na balaa la kufunga mabao kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Raja Casablanca, PSG na Dinamo Bucharest kabla ya show yenyewe haijaanza.

Alifungua akaunti yake ya mabao ya msimu kwa goli zuri alilowafungia Argentina katika ushindi ya Ujerumani mjiini Frankfurt.

Mshambuliaji huyo wa Barca akafunga mara mbili katika mechi ya ufunguzi wa La Liga dhidi ya Real Sociedad pale Nou Camp.

Akaongeza bao moja kwenye mchezo wa El Classico kwenye fainali ya kombe la supercup, kabla ya kutupia mabao mawili ya ushindi kwenye mgumu kwa Barcelona wikiendi iliyopita dhidi ya Osasuna

Messi kashawasha engine, na anatambua kwamba presha yote ipo juu yake baada ya kuwa na msimu mzuri na Barcelona.

Kufunga ni kazi yake ya maisha, kujitunza na kuweka umakini wake kwenye career yakeunaonekana dhahiri ukizangatia na majaribu yanayokuja na umaarufu kwa wacheza soka.

Bado anaonekana na hamu ya kuendelea kubaki kileleni, kitu ambacho kinasokena kwa Wayen Rooney tangu ahamie Old Trafford kwa ada ya £24 million mwaka 2004.

Rooney alirudi kutoka WOZA 2010 na kuanza kuandamwa na skendo kibao kuhusu maisha yake binafsi.

Alipigwa picha akiwa anakojoa mitaani huku akivuta sigara wakati kipindi cha mapumziko. Taswira ile haimuonyeshi mchezaji anayetaka kuwa bora kwa kufikia kiwango chake cha juu kabisa.

Baada ya kutofanya vizuri kwenye WOZA 2010, alirudi na kufunga mabao 11 katika premier league na kusiadia timu yake ya United kufika fainali ya kombe la mabingwa wa ulaya.

Msimu uliopita akafunga mabao 27 kwenye ligi, mabao 3 nyuma ya Van Persie mfungaji bora.

Takwimu za namna hiyo zinathibitisha kwamba Rooney ni mchezaji wa daraja la dunia lakini bado hajaweza kuvunja na kuingia rank za juu kabisa, walipo wachezaji kama Messi, Xavi, Iniesta na Ronaldo - ambao wamekuwa ndio washindani wakuu wa tuzo kubwa ya soka duniani kwa takribani miaka 4.

Akiwa na miaka 26, Rooney anabaki mmoja wa wachezaji muhimu zaidi kwenye  kikosi cha Manchester United ambacho kilipoteza ubingwa wa EPL msimu uliopita kwa sababu hawakuwa na magoli mengi ya kufunga.

Majeruhi yake ni bahati mbaya, na yatamfanya akose michezo kadhaa muhimu ya EPL na mechi za timu ya taifa dhidi ya Maldova na  Ukraine mwezi ujao.

Kinacholeata maswali zaidi, ni kitendo cha kocha wake Sir Alex Ferguson kumuweka benchi kwenye mechi dhidi ya Fulham wikiendi iliyopita.

Ingawa mzunguko wa upangaji kikosi ni lazima kwenye ligi kubwa, kumuacha Messi nje ya kikosi cha Barcelona kwenye mechi muhimu ni kitendo ambacho kigumu sana kiasi cha kutofikirika.


Anacheza kila wiki kwa sababu anataka kufanya hivyo, akihitaji kuanza kwenye kikosi cha kwanza hata kama kuna asilimia nyingi kwamba Barca watashinda vizuri wapinzani wao.

Baada ya Rijkaard kuondoka kutoka Catalunya mwaka 2008, Pep Guardiola akaichukua timu na kuweka imani kwa kijana huyu wa Kiargentina.

Kwa sasa anakaribia rekodi ya Cesar Rodriguez kama mfungaji bora wa klabu hiyo wa muda wote kwenye La Liga, Rodriguez alikuwa amefunga mabao 192, Messi tayari ana 173.

Ni suala la muda tu kabla ya Messi hajafkia rekodi hiyo, lakini kutakuwa hakuna muda wa kuziangalia tena hizo rekodi kipindi anacheza. Baadae atakapotundika daluga ndio atapata muda kuangalia na kukubali kipaji kikubwa mungu alichompa na kujua kukitumia vizuri.

Kwa bahati mbaya Rooney hatokuwa na nafasi kama hii ya Messi , isipokuwa kama atafuata nyayo na mfano bora wa Lionel Messi.

Nawasilisha - Aidan Seif Charlie

1 comment:

  1. Hizi ni moja kati ya Article dhaifu mno ambazo nimewahi kuzisoma, ukiwa unaandika makala kwenye kurasa makini kama hizi weka ushabiki pembeni ndipo ulete hoja yako. Ulikuwa una idea nzuri lakini umeshindwa kuioanisha Kichwa cha habari na maelezo yake. Uandishi bora unahitaji umakini na si kukurupuka ilimradi umejaza ukurasa.

    ReplyDelete