Search This Blog

Friday, August 10, 2012

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA MSEMAJI WA SIMBA EZEKIEL KAMWAGA.


Salaam ! Kwa waliosoma gazeti la Super Star la leo, watakuwa wameona stori yenye kichwa cha habari; "Sinema Mpya Ngassa, Twite." Ndani yake kuna maelezo kwamba Ngassa na Mbuyi Twite wanakwenda Yanga. Kuwa eti Azam wameamua kumpeleka Yanga kwa vile wamekasirishwa na hatua ya Simba kumsajili Redondo. Chanzo cha habari, hakitajwi. Wamezungumza na mimi nimesema hakuna kitu kama hicho. Wamezungumza na Msemaji wa Azam kawaambia hakuna kitu kama hicho. Lakini wameandika hiyo stori kwa kutumia "VYANZO VYAO." Hivi mwandishi kama huyu nikigoma kumpa ushirikiano nitakuwa nimekosea? Chini yake kuna stori ya Okwi. Uongo mtupu. Sote tunajua Okwi amekwenda kuitumikia timu yake ya taifa na atarejea baada ya hapo. Lakini mwandishi, kwa sababu zake, ameamua kufanya hilo lionekane ni tatizo!!!!!! Kwamba sasa Okwi bye bye Simba...Inauma sana lakini waandishi hawa ni rafiki zangu, wanataaluma wenzangu nk.... Tutafanyaje kazi zetu katika mazingira haya ambapo mtu anatunga stori ili auze gazeti????? Naomba mfahamu kwamba kuna watu wanaumia sana kwa habari za namna hii. Hawali wakashiba na wanakaa na wahka siku nzima. Tuthamini hisia za wenzetu

2 comments:

  1. sina nia yakumtetea mwandishi aliyetunga stori hiyo. ninaamini kuwa siku zote swala la pesa limekuwa mbele. wakati huohuo mashabiki tunauelewa na magazeti yetu ya hapa nyumbani, huu ni wakati wa usajil waache watengeneze fedha kwani magazeti yanapata zaidi soko kipindi hiki cha usajili. baada ya hapo ukitunga stori hutauza sana. leo si ndio tarehe ya mwisho? huyo mpotezee tuu...

    ReplyDelete
  2. Haya mambo Ezekiel tumeyazoea na ndio maana baadhi yetu magazeti fulani fulani hata ukipewa bure huchukui.Inasikitisha kwa kweli lakini tufanyaje maana tunaambiwa UHURU WA VYOMBO VYA HABARI.Ni aibu kwakweli kwa mwana taaluma kufanya vitu vya aibu kama hivi.Wanapaswa wajuwe kwamba uandishi wa habari nao ni taaluma wanapaswa waiheshimu.

    ReplyDelete