Search This Blog

Wednesday, August 29, 2012

EDEN HAZARD: BALAA JIPYA KWENYE LIGI KUU YA ENGLAND - ATOA SIRI YA MAFANIKIO YAKE



Eden Hazard ametoa siri yake nyuma ya miguu yake yenye hatari katika kuuchezea mpira - anasema wakati akiwa mdogo alitumbukia kwenye maji ya baraka na miujiza.

Ndio maana haishangazi kuona mshambuliaji huyu wa Chelsea akiwa ameiweka ligi kuu ya England kwenye miguu yake sasa.

Wachezaji wachache, kama wapo, wameonyesha kiwango kikubwa kama Hazard kwenye mwanzo wa msimu huu.

Mpaka sasa, winga huyo wa Ubelgiji anaongoza kwa kutoa assist na pasi nyingi kwenye tatu ya mwsho ya uwanja.

Katika kumsaidia Roberto Di Matteo na kikosi chake kukaa usukani, Hazard ndio mchezaji aliyefanyiwa rafu nyingi mpaka sasa.

Maisha yawe mazuri kiasi gani kwa mbelgji huyu, ambaye aliwagharimu Chelsea £32 million kutoka Lille mapema msimu huu.

Hazard anatoka kwenye familia ya soka, na hivi juzi tu mdogo wake anayemfuatia Thorgan Hazard alisajiliwa na Chelsea: "Mimi na ndugu zangu tulidumbukia kwenye maji ya baraka na maajabu tulipokuwa wadogo na ndio maana naamini tuna uwezo, na soka ni mchezo ambao upo ndani ya famia yetu - baba yetu na baba zetu wadogo wote walicheza soka

Eden Hazard mwenye jezi nyeupe alipokuwa mdogo

"Ni vizuri sana, kwa maana muda mwingi ndani ya nyumba tunaongelea soka"

Akiwa na takribani miezi miwili ndani ya Chelsea Hazard anaelezea maisha yake ndani ya klabu hiyo: "Nimeshapazoea hapa na maisha ya London. Mara unakuwa unataka kufanya vizuri sana unapowasili kwenye klabu kubwa ambayo ina wachezaji wenye majina makubwa.

"Lakini mwishowe unajiambia mwenyewe 'Hawa ni watu kama mimi wenye miguu miwili na mikono miwili'. Ofcourse, ninawaheshimu sana wachezaji niliowakuta lakini sasa ni juu yangu  namna ya kuchonga njia yangu.

"Nijiambia tangu mwanzo kwamba naenda kwenye nchi mpya, kwenye utamaduni mpya, unaotumia lugha mpya.
"Lakini tayari nilikuwa nimeshabadili nchi pale nilipotoka Ubelgiji na kwenda France, hivyo nilitumia njia zile zile hapa Uingereza.
"Hii ni nchi yangu ya tatu na nimekuja haoa kucheza soka. Kama kwenye kila timu, kuna wimbo wa kuanzia, nilivyofika hapa niliwaimbia rap ya kifaransa na walicheka sana.

"Nkaumbuka Frank Lampard alicheka sana nilipofanya interview yangu yangu ya kwanza ya kiingereza - jaokuwa haikuwa mbaya sana ukizingatia ndio nilikuwa naanza.

"Nina bahati kuna wachezaji wawili hapa wanaongea kifaransa - Petr Cech  anaongea na pia Florent Malouda."

Hazard alianza vizuri kwenye ligi kuu ya England - Chelsea waliposafiri kwenda kwa Wigan, akitengeneza goli  moja na kusababisha penati ambayo ikafanya matokeo kuwa 2-0 mpaka mwisho wa mchezo.

Na katika mechi ya pili dhidi ya Reading, mechi yake kwanza kwenye uwanja wa nyumbani akazidisha balaa, akisababisha penati, kutengeneza bao la mwisho na hatimaye mchezo ukaisha 4-2.

Anasema: "Nadhani mchezo wangu wa kwanza dhidi ya Wigan ungekuwa kuwa mbaya! ulikuwa mchezo wangu wa kwanza katika premier league na kwa uzito huo  lolote linaweza kutokea. Kwa bahati nzuri nikafanya vizuri katika dakika 15 za kwanza , lakini haikuwa vizuri sana. Bado ninahitaji kuizoea ligi ya kiingereza.

"Mechi za hapa ni za kasi zaidi, kuna changamoto kubwa na mashabiki wanaishi kwa ajili ya soka, jambo ndilo ninalopenda.

"Mechi yangu ya kwanza kwenye uwanja wa nyumbani ilikuwa nzuri kuliko mechi ya Wigan. Sikuwahi kuwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge kabla, hivyo kuwepo mbele ya umati wa mashabiki siku ile ilikuwa kitu special sana kwangu.

" Goli la nne dhidi ya Reading, nilikuwa nimebaki na kipa na ni kweli ningeweza kujaribu kufunga lakini nilimuona Ivanovic na Torres walikuwa huru. Hivyo nikajiambia mwenyewe, "Zamu yangu ingekuja kwenye mchezo unaofuata.

"Ivanovic ni mtu mzuri sana hivyo nikajisemea, 'Nimuachie afunge"

Hazard aliendelea kuiambia TV ya Ufaransa: "Ofcourse inafurahisha kutajwa kuwa mchezaji bora wa mechi lakini hilo sio lengo langu kuwa mchezaji bora kila wiki.

"Kama tutashika nafasi ya 3 mwishoni mwa msimu na nikiwa na mituzo ya mchezaji bora wa mechi, zitakuwa hazina kwangu."A

No comments:

Post a Comment