Uongozi wa klabu ya Azam umesema tayari imepokea maombi ya makocha 12
wanaowania nafasi ya kukinoa kikosi cha timu hiyo.Maombi ya makocha hayo
yanatokana na uamuzi wa hivi karibuni uliotangazwa na uongozi wa klabu
ya Azam wa kusitisha mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Stewart
Hall.
Baada ya kutangazwa kuondolewa kikosini, klabu hiyo
ilimtangaza kocha wa muda, Vivek Nagul raia wa India atakayesaidiana na
Kalli Ongala.
Mwenyekiti wa Azam, Said Mohamed alisema kuwa
miongoni mwa maombi yaliyopokelewa ni ya makocha wazawa na mengine ni ya
makocha kutoka nje ya nchi.
"Kikubwa ni kwamba tumepokea maombi
ya makocha 12 mpaka sasa miongoni mwao ni wazawa na wengine kutoka nje
ya nchi,".alisema Mohamed.
Hata hivyo, Mohamed hakuwa tayari
kutaja majina ya makocha wala nchi wanazotoka kwa madai kwamba bado
wanafanya upembuzi yakinifu na muda si mrefu wataweka bayana.
Aliongeza kuwa, vigezo vitakavyotumika katika kumpata kocha wao mpya ni rekodi zake katika kufundisha soka na si vinginevyo.
Wakati
huu huo, Mohamed amekanusha taarifa zilizoripotiwa na baadhi ya vyombo
vya habari kuwa klabu yake imemtimua Hall baada ya kumpanga Winga
Mrisho Ngasa katika pambano dhidi ya Yanga.
"Niweke wazi kwamba
uongozi wangu unafanya kazi kwa kuzingatia ushauri wa benchi la ufundi
,hakuna tuhuma zozote zilizoletwa kwetu zinazomhusu Ngassa, sasa
kwanini tumfukuze kocha, huo ni uzushi tu.
Kukanusha huku kwa Azam kwamba walimfukuza Stewart kunakuja siku mbili baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kwambakocha huyo alitimuliwa baada ya kumpanga Ngassa kwenye fainali japokuwa likatazwa kufanya hivyo na uongozi wa AZAM FC.
No comments:
Post a Comment