Mauzauza katika soko la Tanzania yanaendelea, kama ilivyo ada kuna baadhi ya watu wanapenda kufanya mambo kinyume na utaratibu, leo nimetumiwa malalamiko haya ya juu ya mambo yanayoendelea katika kutafuta viongozi wa chama cha soka cha mkoa wa Kigoma.
ZENGWE
Kaka katika mazingira ambayo yanaonekana wazi kuwa katibu wa KRFA Kigoma
kutaka kuendelea kung'ang'ania madaraka tayari zengwe limeanza kwa
katibu huyo kuwakatalia wadau wa soka hasa wanaotoka wilayani kuchukua
fomu za kugombea na tayari chama cha mpira wa miguu wilayani Kasulu
KaDFA kimeandika barua ya malalamiko kwa mwenyekiti wa kamati ya michezo
mkoani humo kama barua niliyoambatanisha hapa inavyoeleza, zaidi
tutasikia nini kitajiri hadi mwisho, kwa hiyo tusaidiane katika hili
maana kuna watu kama Mugabe kwenye soka letu la bongo.
No comments:
Post a Comment