Kikosi cha TSC kilichochukua ubingwa kwa kuifunga Stuttgart. |
Ziara ya timu ya kituo cha TSC Mwanza nchini Ujerumani imeendelea leo kwa kushiriki kwenye michuano mifupi ya 1 ya kombe la Brackenheim-duerrenzimmern iliyoshirikisha timu 3, ikiwemo klabu bingwa ya Bundesiliga under 19 mara 10, klabu ya Stuttgart ya hapa Ujerumani.
Kwenye michuano hiyo iliyoanza mida ya asubuhi hapa Ujerumani, timu ya kituo cha TSC Mwanza iliifunga klabu ya Statauswahl kwa bao 2-1, magoli yakifungwa na Tito Jonas na Japhet Vedastus, kabla ya jioni kucheza yake ya mwisho dhidi ya mabingwa wa mara 10 wa Bundesiliga under 19, klabu ya Stuttgart na kufanikiwa kuifunga kwa mabao matatu kwa mawili.
Kikosi cha Stuttgart kilichoanza leo dhidi ya TSC. |
Benchi la ufundi la TSC Mwanza |
No comments:
Post a Comment