Search This Blog

Monday, July 16, 2012

SAKATA LA USAJILI WA YONDANI: SIMBA YAIANDIKIA BARUA KALI TFF KWA SABABU YA KELVIN YONDAN


Simba Sports Club imesikitishwa na hatua ya Katibu Mkuu wa TFF kujichukulia mamlaka ya Kamati ya Katiba na Sheria na kuamua mustakabari wa suala la Kelvin Yondani kwa barua yenye kumb namba TFF/TECH/GC.12/62 ikijibu pingamizi la Simba Sports Club lililokuwa likitaka mgogoro huo uamuliwe na chombo husika.

Masikitiko hayo ya Simba Sports Club yanatokana na jinsi haki  na misingi bora ya uendeshaji wa mpira inavyoonekana kupindishwa waziwazi kwani Simba Sports Club imeshaandika barua nyingine mbili kwa Rais Tenga moja ya terehe 7/6/2012 yenye Kumb na SSC/5/6/02 ikilalamika juu ya uendeshwaji wa sakata zima la udanganyifu wa usajili wa mchezaji wa Simba Kelvin Yondani ambayo Rais alitoa maagizo kwa Katibu Mkuu na nakala kuja kwa Simba SC kwa barua pepe ya tarehe 8/6/2012 lakini baada ya kutofanyika utekelezaji wowote na badala yake watendaji wa TFF kuendelea kuongea katika vyombo vya habari wakisema mchezaji huyo ni mchezaji huru, Simba Sports Club iliandika barua nyingine kwa Rais Tenga juu ya kukosa imani na sekretarieti ya TFF  kwa barua ya tarehe 23/6/2012 yenye kumb na. SSC/24/6/02 jambo ambalo limeonekana wazi kwamba sekretarieti ya TFF haitendi haki kwa Simba kwa jinsi  ambavyo haikufanyia kazi barua mbili lakini Katibu Mkuu wa TFF amekuwa mwepesi wa kujibu pingamizi wakati si kazi yake ili mradi timu yake ya Yanga mabayo yeye ni mwanachama ifanikiwe jambo lake.

Katika barua ya pingamizi dhidi ya mchezaji Kelvin Yondani kutumiwa na klabu ya Yanga katika michezo ya kirafiki na ile ya CECAFA  ya tarehe 11/7/2012 yenye kumb namba SSC/1/7/02 Simba Sports Club iliomba suala la mchezaji huyo lipelekwe katika kikao cha kamati ya katiba na sheria ambayo muda wake wa kukaa bado kwani kamati hiyo inaweza kukaa baada ya wiki mbili za kufunga usajili na kupokea pingamizi mbalimbali lakini taarifa za uhakika ni kwamba kamati hiyo ilijaribu kuitishwa haraka haraka ili kulitolea suala hili uamuzi lakini corum haikutimia hivyo ikashindwa kutoa maamuzi lakini kwa ubabe Katibu Mkuu akaamua kujichukulia mamlaka yasiyokuwa yake na kumpa leseni ya Yanga Kelvin Yondani huku Simba ikipokea majibu tarehe 14/7/2012 kwa barua uwanja wa Taifa wakati mechi kati ya Yanga na Atletico imeshaanza na ipo dakika ya 18.

Katika barua yake ya kumuidhinisha Kelvin Yondani katibu mkuu kakiri kuwepo kwa mkataba wa Yondani na Simba unaoisha mei 31, 2012 na kakiri pia kupokea nyaraka ya makubaliano ya Simba SC na Kelvin Yondani lakini kwa sababu yeye si mwanasheria na ndio maana kazi hiyo ni ya kamati ya katiba na sheria amezitafsilia pande mbili za mkataba yaani Simba Sports Club na Kelvin Yondani nia yao wakati wanaingia mkataba kwamba mkataba utaanza tarehe 23 december 2012 na kuweka kiambatanisho cha sehemu ya kusaini ya Simba Sports Club ambayo kwa sababu za kibinadamu ilikosewa na inasomeka tarehe 23 december 2012.

Katibu Mkuu wa TFF ameshindwa/amejikataza kuusoma mkataba tangu mwanzo na kuona nia za pande za mkataba ni zipi kwani katika ukurasa wa kwanza mkataba unasoma kwamba umesainiwa tarehe 23/12/2011, pia mkataba unatambua uwepo wa mkataba wa pande hizo mbili unaoisha tarehe 31/5/2012 na pande husika katika mkataba zimeonyesha nia ya kuongeza mkataba mara tu ule wa awali unapoisha.

Katika kipengele cha kwanza mkataba umeshuhudia pande zikitamka waziwazi kwamba mkataba umeongezwa kuanzia (effective) tarehe 1/6/2012 mara tu mkataba wa awali unapoisha sasa inashangaza Katibu Mkuu anazitafsiria pande nia zao kwamba mkataba utaanza tarehe 23/12/2012 wakati mkataba umetamka waziwazi.

Pia sehemu aliposaini mchezaji Kelvin Yondani imeonyeshwa waziwazi kwamba kasaini tarehe 23/12/2011 hivyo kuacha hitimisho lisilo na shaka kwamba Katibu Mkuu wa TFF amekiuka na kujivika mamlaka yasiyo yake ili kutekeleza unazi wake wa Yanga.

Simba Sports Club inakusudia kuyakatia rufaa maamuzi haya ya Katibu Mkuu wa TFF na ipo  tayari kufuata mikondo yote ya sheria mpaka haki ipatikane kwani itatumia taasisi za TFF kwanza na isiporidhishwa na maamuzi itapeleka suala hili CAF mpaka FIFA na jambo la kushukuru ni kwamba Shirikisho la TFF limeanza kujibu barua za Simba SC suala ambalo linaanza kutoa mwanga wa nia ya kutotenda haki lakini barua hizo zitasaidia kuwaonyesha watu wa nje kama tukifika huko jinsi mpira wa Tanzania unavyoendeshwa kinazi na viongozi wa Shirikisho.

Imetolewa na
Simba Sports Club


VIELELEZO VYA SIMBA 




Kusoma vizuri double click
 

8 comments:

  1. Kiongozi pole sana,najua suala hili linakuuma sana na ndo maana unajaribu kulipa nafasi kubwa sana kuliandikia kwa upande mmoja wa team unayoishabikia lkn ndo hivyo na Kijana tayari ameshatinga uzi wa kijani na njano katika mechi ya mashindano,badala ya kulilaumu benchi lako ufundi kwa kumuacha Derick Walulya wakati msaada wake ukiwa bado unahitajika sana(ona jana alivyokuwa kizingiti kwenu) wewe unalaumu TFF kwa kutoa leseni kwa Yondani,hiyo (yako) ni akili kweli,au matope?

    ReplyDelete
  2. Simba si mkubali yaishe kha, Kelvin mwenyewe hataki kuchezea timu yenu sasa mnachomlazimisha ni nini? na hivi SUBASHI amechukua timu hapo ndo kabsaaa msahau maana kwa sasa watakuwa wanauhakika na stahiki zao zote tena ontime so tulieni tu watani kama mlijichanganya kwenye contract na mkaweka tarehe zisizo sahihi na mkasign mpaka na madole gumba its better mkasuburia hizo tarehe zifike ndo muanze kupayuka kuliko ilivyo sasa maana kwanza mnajidhalilisha wazi kuwa HAMPO MAKINI how comes swala nyeti linalohusu maisha ya mchezaji mnakimbilia kusema ni hali ya kibinaadamu? tafuteni hoja nyingine maana hiyo hoja ni hafifu sana.
    Willy

    ReplyDelete
  3. Kaburu usidanganye watu. hilo lako mwenyewe. wewe ulikuwa humtaki Kelvin. hata mimi simpendi. lakini kama hukutaka kumpa adui yako silaha basi hili ungeliweka vizuri. Hili mwenyewe ulilikosea usisingizie watu. kweli Osia Yanga tena Yanga kweli, sasa je?? Kelvin asicheze mpira kwa kuwa wewe hutaki? sio hivyo hukufanya kazi yako vizuri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna watu mna'point sana aisee...

      Delete
  4. Katika uendeshaji wa mpira watu wengine wanachukua faida ya watu kutojua nini kinaendelea. Lakini wapo wanaojua mambo ambayo yanafanyika. Kaburu anataka tu kudanganya umma. Hivi kwa kumuweka njia panda Kelvin alitegemea nini? huyu sio master of destiny ya kelvin. amwache akacheze mpira. Wengine tulio Simba pia hatukubaliani naye. Hata aina ya wachezaji aliorudisha sana sio wenyewe. Mwacheni Kelvin acheze Yanga.

    ReplyDelete
  5. Kevin , Kevin, Yondan, Yondan , kila kukicha, jamani basi tumechoka , tujadili na mengine, Yondani mbona wa kawaIda tu si alikwepo Simba mlipopigwa 3 Sudan? Na nyie Yebo Yebo juzi mmenyanyaswa na Atletico ya Burundi 2 bila mbele ya wake zenu si alicheza?? AlifaNya nini zaidi ya kugongana na Canavaro ??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Napenda nikukubalie. ila hili ukiliangalia linakuzwa sana ni siasa tu za Yanga na Simba. Ndivyo walivyo. Yondani na Maximo walitumika kama kampeni. Unalosema kweli kabisa, Mwaka huu wamehama Kigi, Bartez na Yondani. Lakini huyu ndiyo topic. Ni wa Kawaida sana ila issue ni hiyo, Siasa za Mpira.

      Delete