Search This Blog

Tuesday, July 24, 2012

SAFARI YANGU YA UJERUMANI NIKIWA KWENYE MASHINDANO YA INSEL CUP

Shaffih Dauda nikiwa na waandaji wa michuano ya Insel Cup nchini Ujerumani.

Kwa takribani siku ya pili sasa nipo nchini Ujerumani kwa ajili ya safari ya kikazi. Nikiwa hapa Ujerumani nimefanikiwa kushuhudia baadhi ya mechi ya kombe la Insel Cup - michuano inayoshirikisha vilabu tofauti kutoka sehemu mbalimbali duniani.


Moja ya timu iliyoalikwa kwenye michuano hii, ni timu ya kituo cha kulelea watoto wa mitaani cha jijini Mwanza TSC chini ya mwalimu wa siku nyingi wa soka Rogisian Kaijage. 

Kikosi cha TSC Kilichocheza na Maccabi Haifa
TSC imeshika nafasi ya sita katika michuano ya timu nane iliyoshirikisha timu kama Maccabi Haifa (under 19) ya Israel, Hoffenheim, 1860 Munich, Hadjuk ya Croatia, Karlsruher ya Ujerumani. na nyinginezo.


Katika mechi yake ya kwanza TSC walitoka sare ya 2-2 na 1860 Munich B, wakatoka sare tena ya 1-1 na TSG Hoffenheim kabla ya kutolewa kwenye robo fainali ya Maccabi Haifa ya Israel kwa bao 
1 - 0.
Kikosi cha Maccabi Haifa kilichoitoa TSC kwenye robo fainali.
Bingwa wa mashindano hayo ilikuwa ni timu ya Karlsruher ya Ujerumani iliyoifunga Hadjuk ya Croatia kwa 1-0.
Golikipa wa bora wa michuano Omary Abubakary akipokea hundi ya Euro 400 kama zawadi

Kwa bahati nzuri kwa upande wa TSC - golikipa wa timu hiyo ndio alichukua tuzo ya golikipa bora wa mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment