Search This Blog
Sunday, July 29, 2012
ROBERT KABATI NAHODHA WA TSC NA WENZIE WAZUNGUMZIA UTOFAUTI WA SOKA LA BONGO NA ULAYA
Huyu ni nahodha wa timu ya TSC Academy kutoka Mwanzam akizungumzia mamb tofauti aliyojifunza baada ya kufanya mazoezi na kikosi cha TSG Hoffenheim. Robert anasema kwanza kitu kinachowatofautisha na wenzao ni kujitambua. Wachezaji wa ulaya wanajitambua na kuelewa nini wafanya wanapokuwa dimbani. Pili wana umakini mkubwa uwanjani kiasi kwamba hawakurupuki kufanya maamuzi bali wanajipanga na kucheza kwa utulivu mkubwa na matokeo kufanya vitu vya uhakika.
Mchezaji huyu yeye alizungumzia namna soka lilivyo na manufaa barani ulaya - anasema wachezaji wadogo tu kama wao tayari wanaishi maisha mazuri wakiwa na makwao, magari na mjumba ya kifahari kutokana na soka. Pia alizungumzia jinsi wachezaji wenzao wa kijerumani walivyo wakarimu anasema kabla ya kuja huku alikuwa na fikra za kwamba wajerumani ni watu waliojawa ubaguzi lakini tangu amefika hapa amekutana na hali ya ukarimu ambao umemstajabisha.
KOCHA WA MAKIPA WA TSG NAE ALIKUWA NA HAYA YA KUZUNGUMZA KUHUSU TSC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment