Na Arone Mpanduka-Radio Tumaini
Nimetumia muda mwingi sana kumchunguza Cristiano Ronaldo na matukio yake na leo hii nimepata kitu fulani cha kukuelezea juu ya hilo.Je unafahamu kwamba neno ‘mwisho’linaweza kuwa rafiki na wakati huohuo pia kuwa adui mkubwa kwa nyota huyu? Fuatana nami katika hilo.
NI MTOTO WA MWISHO KUZALIWA
Cristiano Ronaldo ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya mzee Jose Dinis Aveiro ambaye sasa ni marehemu.Katika familia hiyo Ronaldo ana kaka yake mmoja mkubwa aitwaye Hugo sanjari na dada zake wakubwa wawili Elma na Liliana.Kitendo cha kuzaliwa wa mwisho kilimfanya apendwe na wazazi wake ambapo ilimlazimu mama yake mzazi Maria Alveiro kumpa jina la Ronald Reagan, jina ambalo lilikuwa la rais wa Marekani kwa wakati huo.Hiyo ndiyo sababu ya Cristiano Alveiro kuitwa Cristiano Ronaldo ambapo jina Ronaldo linatokana na ‘Ronald’.
AWEKA REKODI KWENYE MECHI YA MWISHO YA LIGI
Katika mechi ya mwisho wa msimu wa ligi wa 2011-2012, siku ya Mei 13 mwaka 2012, Ronaldo aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao katika kila mechi hasa kwa ligi kuu ya soka ya Hispania.Aliweka rekodi hiyo baada ya kufunga bao kwenye mechi hiyo dhidi ya Mallorca na kushangilia vizuri ubingwa wao ambao walikuw awameutangaza kabla ya ligi kumalizika.
ALIKOSA BAO MUHIMU KATIKA DAKIKA ZA MWISHO
Katika dakika ya 90 Cristiano Ronaldo alishindw akufunga bao muhimu ambalo pengine bila ubishi lingeipeleka Ureno katika hatua ya fainali ya euro 2012 baada ya shuti lake kukosa muelekeo wakati walipokuwa wakicheza na Hispania katika mechi ya nusu fainali.Kitendo cha kukosa bao katika dakika za mwisho kwa namna moja ama nyingine kiliipeleka Ureno kwenye muda wa nyongeza na baadae mikwaju ya penati ikawaondoa Ureno kwenye michuano.
ALIPENDA KUPIGA PENATI YA MWISHO AMBAYO HAKUPIGA
Baada ya dakika 120 kumalizika za mchezo kati ya Ureno na Hispania, iliamriwa zipigwe penati tano tano ili kupata mshindi.Cristiano Ronaldo aliomba awe mtu wa mwisho kupiga penati.Lakini kinyume na maratajio wareno wenzake Joao Moutinho and Bruno Alves walishindwa kukwamisha wavuni mikwaju yao ya penati na kufanya kusiwe na ulazima kwa Ureno kumalizia penati ya tano ambayo ilipaswa kupigwa na Ronaldo.
Hatua hiyo ilimazilika kwa Hispania kushinda kwa penati 4 dhidi ya mbili za Ureno.
ALIACHWA NA NDEGE BAADA YA KUTAKA KUKAA SITI ZA MWISHO
Siku moja baada ya Ureno kutolewa katika michuano ya euro 2012 huko Poland na Ukraine, Cristiano Ronaldo aliachwa na ndege iliyokuwa inawarudisha wachezaji nchini Ureno.
Wakati wakiwa uwanja wa ndege wa Ukraine, Cristiano Ronaldo alimtaarifu mtu anayepanga safari kwamba angependa kukalia moja kati ya siti za mwisho za ndege hiyo.
Baada ya kukubaliwa Ronaldo aliomba ruhusa ya kwenda kwenye mgahawa kuchukua vyakula vyake huku akimsisitiza muhusika wa usafiri wa anga kwamba kama ndege inataka kuondoka basi amshitue.
Matokeo yake ni kwamba ile ndege iliondoka na kumuacha Cristiano Ronaldo akishangaa shangaa kwenye uwanja wa ndege.
SAFARI YAKE YA SOKA KWA UJUMLA
Ronaldo alianza maisha ya soka katika klabu ya soka ya Andorinha ambako alicheza kwa miaka miwili kabla ya kuhamia katika timu ya soka ya Clube Desportive Nacional.Mwaka 1997 alitimkia katika klabu ya soka ya Sporting Club de Portugal.Umahiri wake ulimvutia kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye mwaka 2003 alimsajili kwa ada ya paundi milioni 12.24 ambazo ni sawa na euro milioni 15 na wakati huo Ronaldo alikuwa na umri wa miaka 18.Msimu uliofuata Ronaldo alishinda taji la FA na na baadae alishiriki fainali za EURO za mwaka 2004 akiwa na taifa lake la Ureno na kwenye michuano hiyo nyota huyo alifunga bao lake la kwanza katika mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ugiriki na aliisaidia Ureno kutinga fainali.Ronaldo alikuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo za PFA na FWA akifanya hivyo mwaka 2007 na mwaka 2003 alishika nafasi ya tatu kwenye kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa dunia wa mwaka.Mwaka 2008 nyota huyo alishinda taji la klabu binga barani Ulaya akiwa na Manchester United na alitangazwa kuwa mshambuliaji bora pamoja na mchezaji bora wa michuano hiyo na pia alikuwa mfungaji bora wa michuano hiyo na kutwaa kiatu cha dhahabu.Ronaldo pia aliwahi kuweka rekodi nzuri ya kufunga bao kwa kupiga shuti umbali wa yadi 40 wakati timu yake ya Manchester United ilipokuwa ikicheza na FC Porto katika mchezo wa robo fainali wa Chamions League mwaka 2008.Hii ilimfanya bingwa mara tatu wa tuzo ya Balon dOr Johan Cruyff kusema kwenye mahojiano maalum kwamba “Ronaldo ni bora kuliko George Best na Denis Law ambao walikuwa wachezaji wakubw akatika historia ya Manchester United”.
MAISHA BINAFSI
Baba mzazi wa Ronaldo Jose Dinis Alveiro alifariki dunia mwaka 2005 kwa tatizo la ini ililotokanana unywaji wa pombe kupita kiasi na wakati huo alifariki akiwa na umri wa miaka 52 huku mwanae Ronaldo akiwa na miaka 20.Ronaldo ana maduka makubwa mawili ya kifahari yote yakiwa nchini Ureno ambapo moja lipo mjini Lisbon na lingine lipo pale Madeira.Maduka hayo huuza bidhaa mbalimbali hasa mavazi yenye lebo yake ya CR7.Hadi kufikia mwezi Agosti mwaka 2010,Cristiano Ronaldo alifikisha jumla ya mashabiki milioni 10 katika mtandao wa kijamii wa Facebook.Ronaldo awali alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo wa Uingereza Alice Goodwin na baadae Gemma Atkinson na mwanzoni mwa mwaka 2010 alikuwa na mahusiano na mwanamitindo mwingine kutoka nchini Urussi Irina Shayk.
mpanduka@yahoo.com(0713 896320)
No comments:
Post a Comment