Search This Blog

Monday, July 9, 2012

MKATABA WA FRANCIS CHEKA KUCHEZA NA BONDIA TOKA NCHINI MISRI.


Jamani twende mbele turudi nyuma, huu kweli unaweza kuwa mkataba wa pambano kubwa la ndondi linalomuhusu bondia kama Francis Cheka ?
Kwa aina ya mkataba kama huu ambao unaonekana hapo juu siwezi kushangaa bondia akaingia mitini,
Mimi huwa sipendi kuangalia nilipoangukia bali hupenda kuangalia nilipojikwaa ili nisije jikwaa tena,
Cheka kweli ana makosa kutokana na hili sakata la kushindwa kupanda ulingoni,lakini pia inaonekana MAPROMOTER wetu nao wana matatizo makubwa,kama promoter anachukulia mambo poa poa namna hii siwezi kushangaa kumuona Bondia anagoma kupanda ulingoni.


 maoni ya Mdau.

Kwako Cheka mimi ni Mshabiki wako namba moja Lakini kwa juzi dah umenifanya ni-judge uwezo wako wa Kufikiri, Ulienda Msumbiji ukasema kuwa hutapigana, Umetumiwa tiketi ya Ndege na Shigongo umeenda kupima sasa iweje usipande ulingoni wakati mtu uliyekuwa unatakiwa kupigana nae alikuwa anapima na wewe?? ulisema utapigana na Bondia kutoka Ghana leo unasema Bondia ilibidi atoke Misri, dah kaka unajichanganya sana Jipange upya, angalia hadhi yako umepoteza heshima yako, umetupotezea muda wetu namambo mengine, mwisho ulichonikera eti ukapanda ulingoni na Jeans!!!! dah umechemka Brother jipange upya

7 comments:

  1. ulitaka apande uchi?usiwe mjinga mjinga wewewe

    ReplyDelete
  2. mbona wa shigongo karatasi safi na wa misri karatasi chafu halafu limechanika na kufutika mwaka si ndo magumashi hayo

    ReplyDelete
  3. nilikuwa naangali taarifa mbalimbali za habari za michezo kutoka kwenye tv mbalimbali za hapa bongo nilikuwa namuona cheka na kaseba wanatambiana katika picha za pamoja,vile vile niliona siku wakiwa na mkutano na wanahabari na hata wazazi wao nakumbuka walitambiana kuhusu hili hata uzito wamepima...ina maana matangazo na magazeti yote yale yaliobandikwa hakuyaona wala kuyasika kwa nini asiende kwenye media kama halivyofanya jana ili kutuambia sie wapenzi wake tulio safiri toka mkoa kwamba yeye hapigani vile vile tuangalie tarehe ambayo inaonyesha hapo kwenye mkataba je,ndio hii ambayo inatakiwa wapigane!!!mbona tarehe hazifanani?......mimi sijakuelewa naomba unieleweshe tena mimi shabiki wako!!!!

    ReplyDelete
  4. TARAKIMU: 4,800,000
    KWA MANENO: MILIONI NANE ONLY.

    KAZI IPO JAMANI. MWANDIKO OVYO, MKATABA OVYO. NI UPUUZI MTUPU.

    ReplyDelete
  5. nilikuwa naangali taarifa mbalimbali za habari za michezo kutoka kwenye tv mbalimbali za hapa bongo nilikuwa namuona cheka na kaseba wanatambiana katika picha za pamoja,vile vile niliona siku wakiwa na mkutano na wanahabari na hata wazazi wao nakumbuka walitambiana kuhusu hili hata uzito wamepima...ina maana matangazo na magazeti yote yale yaliobandikwa hakuyaona wala kuyasika kwa nini asiende kwenye media kama halivyofanya jana ili kutuambia sie wapenzi wake tulio safiri toka mkoa kwamba yeye hapigani vile vile tuangalie tarehe ambayo inaonyesha hapo kwenye mkataba je,ndio hii ambayo inatakiwa wapigane!!!mbona tarehe hazifanani......mimi sijakuelewa naomba unieleweshe tena mimi shabiki wako!!!!

    ReplyDelete
  6. KAKA SHAFFIH
    Ahsante kwa kipande hiki cha mkataba. Inaonekana kulikuwa na makubaliano ya mdomo kwamba kama bondia kutoka misri hatakuja basi apigane na kaseba!!! Kitu ambacho Cheka angeweza kutekeleza au kukataa kwa muda wowote huo. Kingine kinachinishangaza huu mkataba mbona hauko vizuri, kwanza hauna mhuri wa Mwanasheria wa pande zote ambao wangeshuhudia utiaji sahihi huo. TPBO haina ruhusa yoyote katika mkataba huo( haihusiki)kwa sababu huu mkataba kwanza haujasajiliwa na TPBO. Kama Cheka angepatwa na madhara TPBO wangesema nini?
    KAKA SHAFFIH HUU NI UHUNI WA PROMOTA WA BONGO HATA Mr. SUGU ALISHAWAIMBA HAO.
    cHEKA BIG UP
    TPBO MMECHEMKA NA PROMOTA WENU.
    NENDENI MAHAKAMANI MKAJIHUKUMU WENYEWE

    ReplyDelete
  7. Hawa mapromota feki na vyama vya kihuni vya ndondi ndio wanaoua boxing tz,pia mabondia wananyonywa sana haki zao hazisimamiwi ipasavyo hawana hata bima iwapo watapata matatizo mchezoni.

    ReplyDelete