SUPER MARIO BALOTELLI
Nani mwingine zaidi ya kijana mwenye asili ya Ghana Super Mario?
Mario Balotelli alionyesha kwamba kidogo anaanza kukomaa kiakili na kutlia wakati wa Euro 2012, lakini wote tunatambua kwamba ni kichaa kiasi gani.
Kwa hakika japokuwa ameonyesha kutulia kidogo, lakini kwa Mario Balotelli unapoandama mwezi mchanga kwake basi tegemea lolote kutoka kwake akiwa uwanjani.
Marefa wa England wanasubiri ligi ianze wakutane na Balotelii aliyestaharabika lakini vinginevyo tutaendelea kuona kadi kadhaa nyekundu zikiigharimu timu yake ya Manchester City.
Na Mario ataendelea kujiuliza kila "Why Always Me" mpaka atakapoacha utukutu dimbani atleast.
JOEY BARTON
Inapotajwa listi ya wachezai watukutu nadhani jina la huyu kijana wa kiingereza haliwezi kukosa.
Ni maarufu kwa matukio yake ya ukosefu wa nidhamu kuliko soka lake, alianza kupata umaarufu kwa tabia zake za nidhamu ndogo tangu akiwa Manchester City, lakini dunia ilimtambua zaidi pale alimpokaribisha kwenye Premier League mchezaji kutoka Ivory Coast ambye ndio kwanza alikuwa akiichezea timu yake mpya ya Arsenal mechi ya kwanza ya EPL 0 na kwa bahati mbaya akakutana na mtoto wa mjini Joey Barton na akamsababishia kadi nyekundu kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu ya England msimu uliopita kati ya Newcastle na Arsenal.
Ukichaa wake kwenye msimu uliopita haukushia Newcastle tu, alipohama kwenda QPR aliendeleza ukorofi wake, na tukio kubwa zaidi alilifanya kwenye mechi ya lazima kupata matokeo chanya kwa timu ili kuweza kubaki ligi kuu dhidi ya Manchester City - matokeo yakiwa moja moja Joey Barton akaanza mtiti na Carlos Tevez na akapigwa red card, kabla ya kumtandika ngumi ya mbavu Sergio Aguero akiwa anaelekea nje ya dimba.
Pia amekuwa na matukio mengi ya kustaajabisha nje ya uwanja lakini mmiliki wa QPR sasa amempa nafasi ya mwisho huku akimvua unahodha - kwa jinsi alivyo huyu jamaa ni vigumu kuacha mtukutu Joey Barton.
Kwenye msimu unaonza ndani ya kipindi cha siku zisizopungua 35 tutashuhudia Barton akilamba kadi nyekundu nyingine kama ilivyo ada.
RYAN SHAWCROSS
Ni maarufu zaidi kwa tukio lake la kumvunja mguu mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey mwezi wa pili 2010, Mchezaji huyu wa Stoke City amekuwa na historia ya kucheza rafu mbaya sana.
Na huku akiwa anaichezea klabu inayojulikana kwa kutumia mabavu haistui kumuona kwenye listi hii.
Yeye pamoja na patna wake kwenye ulinzi Roberto Huth wanabidi wajitazame upya na aina yao ya kufanya tackling. Lakini la sivyo tegemea kumuona mchezaji huyu kinda la Old Trafford akiendelea kulamba kadi nyekundu msimu ujao.
NIGEL DE JONG
Kiungo wa Manchester City anajulikana zaidi kwa aina ya mchezo wake wa kukaba na kutumia nguvu zaidi. Nae ana historia ya matukio ya ajabu kwenye soka.
Makubwa zaidi ni pale alimpovunja mguu nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa na Newcastle Hatem Ben Arfa na lile teke la kung-fu alilompiga kiungo wa Spain Xabi Alonso kwenye world cup 2010.
Umuhimu na kuapata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kunaweza kukawa kumepungua kwa mbingwa hao wa watetezi wa EPL katika miezi ya karibuni, lakini kwa hakika zaidi ataendelea kupata nafasi kwenye kikosi na endapo atacheza basi tegemea lolote kutoka kwa kiungo huyu wa kidachi.
CHEIK TIOTE
Story ni ile ile kwa kiungo wa Newcastle Cheik Tiote.
Anaweza kuwa moja ya viungo bora wa Premier league kutokana na kazi kubwa anayoifanya dimbani hasa kwenye kulinda safu ya ulinzi, lakini rekodi ya nidhamu yake inaweza kumuangusha.
Ni mmoja ya wachezaji wanaocheza tackling za hatari dhidi ya wapinzani - huku akionyesha ni namna gani anavyojituma kwenye kuulinda ukuta wa kikosi cha Alan Pardew.
Matokeo yake msimu uliopita alipata kadi za njano 11 - hivyo tegemea kumona akiendelea kuingia kwenye vitabu vya marefa kwa red card.
No comments:
Post a Comment