Mapema mwaka jana, Manchester City, inayomilikiwa na mmoja ya wanafamilia wa familia ya kifalme ya Abu Dhabi, iliingia mkataba wa udhamini ulio mnono zaidi katika historia ya soka na Etihad Airways, ambayo inamilikiwa na familia ya kifalme ya Abu Dhabi. Hii ilionekana kama ni janja ya City kuweza kuepeukana na matatizo ambayo wangeweza kukutana nayo dhidi ya sheria ya Financial Fair Play, ambayo inahitaji vilabu kutumia fedha kwa kadri inavyoingiza tu na sio kutoka mfukoni kwa mtu/watu fulani, rafiki au ndugu/familia.
Baada ya City kufanya hivyo, sasa watumiaji wengine wakubwa wa EPL, klabu ya Chelsea nayo imesaini mkataba wa wenye thamani kubwa na kampuni ya Gazprom Energy.
Gazprom, ni kampuni kubwa ya nishati nchini Urusi, imesaini mkataba wa miaka mitatu huku thamani halisi ya deal hilo ikiwa imefichwa na pande zote mbili. Hii sio mara ya kwanza kwa mmiliki wa Chelsea kufanya biashara na Gazprom .
Gazeti la Telegraph la Uingereza linaeleza:
"Sheria ya UEFA inawalazimisha vilabu kuacha kukubali dili za udhamini kutoka kwa watu/kampuni zenye mahusiano nazo. Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich, aliuza hisa zake kwenye kampuni ya mafuta ya Sibneft kwenda Gazprom kwa £8.4 billion mwaka 2005 na Uefa na sheria zake zinakataza uhusiano kama huu kwenye - ambapo mmiliki wa klabu anakuwa na uhusiano na kampuni inayotoa udhamini kwa klabu."
Lakini Manchester City wameweza kupita na dili lao la rekodi ya dunia na Etihad, basi na mkataba wa Chelsea na Gazprom itabidi uvuke vikwazo vya UEFA - kwa kuwa Abramovich alishauza hisa zake za kampuni yake ya zamani kwa mdhamini mpya wa Chelsea kwa hiyo anaweza kusema hana nguvu yoyote katika kukamilika kwa udhamini huo wa Chelsea.
Kwa maana hiyo Chelsea na Manchester City wataendelea kutanua misuli ya fedha kwenye soko la usajili pamoja na Platini kuleta sheria yake ya Financial Fair Play.

No comments:
Post a Comment