Search This Blog

Wednesday, July 18, 2012

LIVE MATCH CENTRE: SIMBA 3 - O AS PORT - FULL TIME


Hapa wakishangilia bao la tatu.

Mashabiki wa Simba wakishangilia magoli ambao timu ilikuwa ikifunga kwenye mchezo wa leo uliomalizika dakika chache hapa uwanja wa taifa - Dar es Salaam.

DK 90: Simba 3 - 0 AS port.

DK 85: Simba 3-0 AS Port 


DK. 74: Abdallah Juma anaifungia Simba baola tatu.

DK: 70  - Anatoka Haruna Moshi anaingia Uhuru Selemani
DK 68: Abdallah Juma wa Simba anakosa bao yeye na nyavu hapa, baada ya kumpora kipa mpira.

DK 65: Felix Sunzu anaenda kupiga penati na anafunga.
DK 64: Mwinyi Kazimoto anaingia kwenye boksi anajaribu kuvika kanzu beki ambaye anaushika mpira na inakuwa penati.

DK 60: Abdallah Juma anaiandikia Simba bao la kwanza katika mchezo huu.

DK 55: Shomari Kapombe anagongeana vizuri na Felix Sunzu na wanaingia mpka kwenye 18 - Sunzu tena anakosa nafasi ya wazi ya goli kwa mara nyingine tena.

DK 50: Simba kama ilivyokuwa kipindi cha kwanza Felix Sunzu anapoteza nafasi ya kufunga bao hapa.


Selemani Matola anazungumzia namna Simba walivyocheza ovyo kipindi cha kwanza na kutoa ushauri nini kifanyike ili kuweza kupata ushindi.


Second Half inaanza Simba wanafanya mabadiliko anaingia Juma Nyosso anatoka Amri Kiemba.


Mashabiki wa klabu ya Simba wakionekana kutofurahishwa kabisa na timu yao inavyocheza



DK 45: Timu zote zinashambuliana lakini Simba wanaonekana kulisakama sana goli la wapinzani wao ingawa safu ya ushambuliaji imeendelea kuwa butu.

DK 40: Simba 0-0 AS Port

DK 30: Kanu Mwabivyanga wa Simba anaingia ndani ya kumi nane na kutoa krosi safi na Sunzu anaikosa na kupoteza nafasi nyingine ya kufunga. 


DK 25: Simba wanaendelea kupoteza nafasi za kufunga mabao hapa, lakini ni vizuri pia kumsifia golikipa wa AS Port, anaokoa sana michomo ya washambuliaji wa Simba.

DK 20: Simba wanalishambulia kwa kasi lango la Port na wanapata nafasi kadhaa na wanashindwa kuzitumia.

DK 15:  Timu zinashambuliana kwa zamu huku mpira ukiwa unachezwa zaidi kati ya uwanja.
DK 08: Simba 0 - 0 Port

 SIMBA VS AS PORT LIVESCORE
Add caption

Mchezaji wa zamani wa Simba Seleman Matola akiwa na Ezekiel Kamwaga ambaye ni msemaji wa klabu hiyo wakisubiri mpambano kuanza

Baadhi ya mashabiki na wadau wa Simba wakiwa wnasubiria mechi ya timu yao kuanza.

Mchezo wa kwanza wa kundi hili umeisha kwa matokeo ya klabu ya URA ya Uganda kuitungua Vita ya Kongo kwa mabao 3-1.

2 comments:

  1. mimi nimeutazama mchezo wa jana wa simba kupitia supersport,sijaelewa uliposema kua simba ilicheza ovyo kwasababu tangia kipindi cha kwanza simba ilifika golini na ilitengeneza nafasi kadhaa isipokua sunzu hakua vizuri na hakuzitumia nafasi,na pia ukumbuke wale jamaa jana walipaki basi kimtindo na hawakufunguka kivile na ndio maana mabadiliko aliofanya milovan yalilenga kuongeza pace na kutanua uwanja ili kuwastrech wale jamaa,na simba alitumia nafasi alizopata kipindi cha pili pamoja na kuendelea kukosa mabao sasa sielewi kama kukosa magoli ndio kucheza vibaya ama ndo unazi na propaganda za wachambuzi wetu

    ReplyDelete
  2. shaffii,siku ulizompa mzee akilimali zilishapita na hujatoa tamko lolote tuelewe nini ama mzee alikua sawa ama umepewa chako umefyata mkia

    ReplyDelete