Search This Blog

Tuesday, July 3, 2012

KALI YA LEO: IKER CASILLAS ALIMUOMBA REFA APUNGUZE MUDA WA MCHEZO KUWAEPUSHA ITALY NA KIPIGO KIKUBWA ZAIDI




Mpaka wakati goli la nne lilipoingia kwenye ushindi wa Spain dhidi ya Italia katika fainali ya Euro, nahodha wa La Roja Iker Casillas ikabidi awaombe marefa kupunguza muda wa dakika za nyongeza na kupuliza filimbi ya kumaliza mpira.

Casillas, ambaye amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda mechi 100 za kimataifa pia kuweka rekodi ya kucheza dakika 509 bila kuruhusu wavu wake kuguswa kwenye michuano hiyo (akiizidi rekodi ya kipa wa Italia Dino Zoff ya kucheza dakika 494 bila kufungwa), Casillas alimuita refa msaidizi na kumwambia "Walindie heshima Wapinzani wetu Italia." Alisema maneno hayo wakati wachezaji wenzake wa Spain wakiwa bado wanaliandama lango la Azzuri.
    Ingawa refa hakumsikiliza mpaka dakika za nyongeza zilipoisha refa kapuliza kipenga kuashiria mwisho wa mchezo, Iker akawafuata marefa na kushikana nao mikono kabla ya kwenda kushangilia na wenzake.
Kilikuwa kitu kidogo ambacho hata hivyo hakikufanikiwa lakini jambo la msingi ni moyo wa kiuwanamichezo alionao Iker, ndio maana anaitwa "Saint".

No comments:

Post a Comment