Pichani kulia ni mmoja wa waratibu wa tamasha la Serengeti Mc
Shujaaa-Mwanza,Adam Mchomvu akimtangaza mshindi wa shindano la Serengeti
Mc Shujaaa,aitwaye Ramastar pichani shoto ndani ya jijini la
Mwanza.Shindano hilo limefanyika jioni ya leo kwenye kiota cha maraha
cha Clup Lips,Isamilo jijini humo.Katika mchakato wa shindano hilo
kulikuwepo na msisimko mkubwa kwa vijana wengi kujitokeza na kushiriki
kikamilifu na kuwa ushindani mkubwa,aidha walijitokeza vijana wapatao 56
na hatimaye kupatikana mshindi mmoja ambaye atakwenda Dar kushindana na
wengine kutoka mikoa mbalimbali kwenye kilele cha tamasha la Serengeti
Fiesta 2012 lililopangwa kufanyika katika viwanja vya Lidaz
Club,Kinondoni.
Fainali ya kumsaka kinara wa Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012 ndani ya
jiji la Mwanza,pichani kulia ni Ramastar akimisikiliza kinara mwenzie
Ramside akighani katika hatua ya mwisho kabisa.
Adam Mchomvu akiwa na washiriki wawili wa shindano la Mc Shujaa,kulia ni
Ramastar na shoto ni Ramside ambao walionesha umahiri na ushindani
mkubwa katika suala zima la kughani mbele ya mashabiki kibao (hawapo
pichani) waliojitokeza kushuhudia mpambano huo ndani ya Club
Lips,Isamilo jijini Mwanza.
Pichani kulia ni mmoja wa majaji wa shindano la Serengeti Fiesta Mc
Shujaa 2012,Prodyuza Duke akizungumza machache kabla ya shindano
halijaanza,shoto kwake ni jaji mwingine na pia ni mmoja wa waratibu wa
shindano hilo Reuben Ndege a.k.a Ncha Kali akisikiliza kwa makini.
Adam Nchomvu akisoma majina ya washiriki waliongia kwenye robo fainali ya Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012
Msanii chipukizi Ramastar akionesha umahiri wake wa kughani.
Baba Johniiii nae akishusha mistari yake mbele ya washiriki walioingia robo fainali.
Mmoja wa washiriki aitwaye Pusha akikamua vilivyo mitindo huru.
Majaji wa shindano la Serengeti Fiesta Mc Shujaa 2012 wakiwa makini
katika suala zima la kutafuta kinara wa shindano hilo ambalo kwa
asilimia kubwa vijana wengi wamevutiwa nalo,kiasi hata kupelekea vijana
wengi kujitokeza na kushiriki safi kabisa.Pichani kulia ni Jaji Ncha
Kali,Deey-Classic pamoja na Prodyuza Duke.
No comments:
Post a Comment