Kwa mara ya pili kwenye maisha yake ya soka - kocha mkongwe Luis Van Gaal hatimaye amepata nafasi ya kusahihisha makosa yake aliyoyafanya miaka sita iliyopita kwa kuiongoza Uholanzi kukosa nafasi ya kucheza kwenye kombe ladunia kwa mara ya kwanza.
Siku kadhaa baada ya kocha Bert van Marwijk kujiuzulu kuifundisha Uholanzi baada ya kucheza kwa kiwango kibovu kwenye Euro 2012, leo hii amepata mrithi wake - Luis van Gaal.
Van Gaal kocha wa zamani wa Ajax, Barcelona na Bayern Munich anamrithi Bert, huku ikiwa ni kipindi chake cha pili kuiongoza Holland.
Baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari Van Gaal alisema: "Ni changamoto niliyokuwa nikiisubiri sana, nashukuru nina nafasi ya kurekebisha palipoenda vibaya mara mwisho nilivyokuwa mwalaimu wa timu ya taifa."
Kocha huyu mwenye miaka 60 amesaini mkataba wa ambao utampeleka mpaka kwenye fainali za kombe la dunia 2014.
No comments:
Post a Comment