Wilhelm Gidabuday ( Kulia )
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UFISADI NDANI YA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA NA CHAMA CHA RIADHA TANZANIA, NA SABABU KUU YA KUTOTUMIKA KWA KATIBA WAKATI WA UCHAGUZI WA CHAMA CHA RIADHA TANZANIA: SEREKALI SASA IWEKE TUME HURU YA UCHUNGUZI ILI BENDERA YETU ISIENDELEE KUWA TAMBARA BOVU KATIKA OLIMPIKI IJAYO:
- Mwaka 2002: Filbert Bayi aliwasimika viongozi wa wanariadha badala ya viongozi hawo kuchaguliwa na wanariadha kama ilivyoainishwa kwenye katiba ya RT. Chama hicho cha wanariadha kinastahili kupokea ruzuku kila mwaka lakini fedha hizo zinapotelea nyumbani kwa Bayi. Hivyo usimikaji huo ulifanywa ili aweze kuzipora hizo hela ambazo ni za wanariadha.
-
- Mwaka 2006: Filbert Bayi kwa kushirikiana na Suleiman Nyambui waliwazuia wanariadha Michael Mislay Tluway na Rogarth John Stephen katika timu ya kwenda jumuia ya madola Australia dakika za mwisho ili kuwapa marafiki zake wauza madini kutumia tiketi hizo kwa kimvuli cha timu hiyo (kana kwamba wao ni wanamichezo ama viongozi) ili wakafanye biashara ambazo bila shaka watagawana na wahusika wenyewe. Cha kujiuliza ni kwamba kwa kufanya hivyo Bayi na Nyambui hawajatumia vibaya madaraka yao?. Pia kwa kufanya hivyo hawajaipunguzia Tanzania uwezekano wa kupata medali?.
-
- Mwaka 2008: Timu iliyojiandaa kwenda Edinburg Uk ilinyimwa visa ya Uingereza kutokana na ubalozi wa Uk kubaini kuwepo wazamiaji katika timu hiyo, Suleiman na Filbert Bayi ndio waliojaribu kuwasafirisha wazamiaji hao kwa kuwatoza kati ya USD 2,500 na USD 4,000. Tabia hiyo ya kuwasafirisha wazamiaji ni ya muda mrefu sana na viongozi hao wawili wanafaidika kila panapokuwepo na mashindano ya kimataifa. Pia mwaka huo huo timu ya olimpiki ya Beijing iliingia katika malumbano baada ya viongozi wa TOC na RT kusaini mikatabo miwili tofauti ya
-
- PUMA na LINING. Tafrani hiyo iliisababishia Tanzania kutiliwa mashaka na makampuni hayo kuacha kudhamini timu zetu hadi leo. Je kama huu sio uwizi ni kitu gani hicho?. Pia mwaka huo huo Suleimana Nyambui aliwapatia watu barua ya kuomba visa ya Australia, watu hao walikamatwa na madawa ya kulevya walipofika Australia, kitendo ambacho kiliiaibisha taifa letu.
-
- Mwaka 2009: Timu ya Tanzania iliyokwenda Berlin katika mashindano ya dunia ililazimika kila mwanariadha kukatwa pesa zao za posho ili kumlipia Meta Petro tiketi ya ndege. Meta Petro ni mjumbe wa kamati tendaji ya RT. Hivyo wanariadha walipewa “AMRI” sio ombi kwamba ni lazima wachangie malipo ya bosi huyo wa RT. Je hiyo siyo matumizi mabaya ya madaraka?.
-
- Maandalizi ya Olimpiki: Inafahamika kuwa kila mwaka wanariadha wote duniani ambao wamewahi kushiriki mashindano ya olimpiki huwa wanapewa fedha za maandalizi ya olimpiki ijayo kupitia kamati ya olimpiki ya nchi husika. Hivyo hamna mwanariadha yeyote hapa Tanzania ambaye amewahi kupata ruzuku hiyo kwa sababu viongozi wa TOC wanazitumia wao wenyewe kwa kudanganya IOC (International Olympic Committee) kwamba fedha hizo zinawafikia walengwa. Je serekali inafahamu ufisadi huo?.
Maswali muhimu ya kujiuliza ama kuwauliza waheshimiwa serekalini na wizarani:
- Je ikulu inafahamu kwamba huenda bila kujua waliwaalika viongozi mafisadi ambao wameliibia serekali na wanariadha wa kitanzania kwa muda mrefu?. (Ukiwaacha Malinzi, Waziri na wanaojiita viongozi wapya) Hakika rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapaswi kukaa meza moja na “Human traffickers”. Ubalozi wa UK ulibaini hilo 2008.
-
- Je serekali haistahili kuweka timu maalum ya kuchunguza madai hayo kama ilivyofanya kwa madai ya TBS?. Je wananchi tungejuaje ufisadi ndani ya TBS kama uchunguzi usingefanyika?.
-
- Je wizara na serekali kwa pamoja hawaoni haja ya wahusika hao kujiuzulu kupisha uchunguzi halali ili kubaini ukweli na ili wanariadha wapate motisha kwa mashindano yajayo?.
-
- Je serekali kupitia wizara husika inafikiria nini kuhusu USD 100,000 zilizototewa na IOC kwa maandalizi ya olimpiki ya London, na je inaridhika na kwamba wanaokwenda kutuwakilisha ni wachache mno kwa bajeti ya fedha hizo?. Je hela inatumikaje, je kuna mkaguzi anayefuatilia fedha hizo?.
Wote tunapenda nchi yetu kuleta medali, lakini “taaluma ikidharaulika kwa kulinda maslahi binafsi nchi hii isitegemee medali”.
Watanzania wameshuhudia uchaguzi wa RT ukifanyika bila katiba kwa kutumia mabavu ili kulinda maslahi ya wachache hao wanaokwenda London kuunganisha dili zao ili waendelee kuwepo katika system na kuendelea kunufaika na “voting power” ambayo watapata kutokana na kuwaweka watu wao lindoni. Wizara imeelezwa mara nyingi lakini haichukui action.
Hivi sasa “waliokataa kutumia katiba iliyopo ndiyo wanaopewa dhamana ya kuunda katiba ijayo”. Inamaana kama wanariadha wote ni vipofu, HATA WAZIRI PIA NI KIPOFU?. Tutaangalia kwanza wafike hapo wanapotaka kufika, lakini umma wa watanzania ujue kwamba “Time will tell”.
By:
jmaa anauchungu na nchi yke au kunakitu alikuwa anakitaka ss amekikosa ameamua kumwaga ugal?? kipind chote ich ye alikuwa wap??
ReplyDeleteAcha upuuz wewe m2 anasema mambo ya maana badala ya uchunguz upite ili tujue ukwel uko wapi we unaleta unaz haya madudu mpaka lini? Edwin dushi
ReplyDeleteHuyu mkubwa kiboko kwanza ana uchungu alafu ana rejea za kutosha lakini suala linakuja kwa nini masuala kama haya yanafumbiwa macho yanapokuwa yanatendeka mpaka ovu linapotokea ndipo siri nzito kama hizi zinafichuliwa
ReplyDeleteI think the time has come for changes to be made, hope the government will investigate this as it is shame for our country.
ReplyDeletesafi sana kaka kwa kuwachana,hawa viongozi wetu wanakula pesa zetu sana tu mfano mdogo kulifanyika mashindano ya east africa and central ya senior uwanja mpya mwaka jana hatuja pewa poosho zetu mpaka leo ni 150,000/= kila mchezaji hawa wametuibia ndugu mwandishi na tunaomba serikali kupitia wizara ya michezo ifuatilie hili,hivi unawezaa kupeleka wanariadha 6 na viongozi 8 olympic hii idadi jaman ni sahihi?pesa wanakula wao so sisi wachezaji tunapinga vikali nyambiu kurudi RT yaani tumekwisha jamani.mm nasikitika kuona miaka yote wanapeleka watu wa mbio ndefu tu na wakati watu wa short distance na miruko wapo wachezaji chipukizi wengi tu bt wanashindwa kufikia malengo kutokana na ubinafsi wa viongozi kupeleka watu wao wa mbo ndefu eti kwa sababu wao walikimbia mbio ndefu.tunairaani timu iliyochaguliwa kwenda london na haitarudi na medal hata moja cos viongozi wamechagua watu wao so wanashindwa kuiga hata kwa wenzetu kenya mbio inaandaliwa ya kuchagua timu sio hapa kwetu wanaitana tu flani njoo kambini tena kwa filbert bayi ili fedha ya camp aichakachue jaman hivi hamuwezi kuona ndugu waandishi timu ya taifa tena inaenda olympic inalala kwny mabweni ya wanafunzi badala ya hotelini?for more information call 0712 146911
ReplyDelete