Search This Blog

Tuesday, July 3, 2012

HIVI NDIVYO CASILLAS, XAVI, INIESTA TORRES NA WENZAO WANAVYOWEZA KUSAIDIA KULIPA DENI KUBWA LA TAIFA HILO

Usiku wa Jumapili, timu ya taifa ya Spain ilishinda 2012 UEFA European Championsship, na wakawa timu ya kwanza kushinda makombe matatu makubwa mfululizo. Spain kwanza walishinda Euro 2008 na baadae World Cup 2010.

Ukiachana na hilo, wakati huo huo, Uchumi wa Spain umekuwa kwenye hali mbaya sana. Wakati timu ya soka ikishinda ubingwa waulaya mambo yamezidi kuwa mabaya kwa nchi hiyo hasa kwenye mgogoro wa kiuchumi wa madeni ya nchi za ulaya.

Katika kutafuta namna atleast ya kupunguza deni la taifa, baadhi ya watu na taasisi kadhaa zimekuja na habari za kufurahisha sana, kwa pamoja wamekaa chini na kuanza kufanya tathmini ya thamani ya jumla ya wachezaji wa kikosi cha wachezaji wa La Roja na namna gani thamani yao inaweza kuisadia serikali ya Spain kukabiliana na matatizo ya kiuchumi yanayoikabili.

Katika uchunguzi uliofanywa na CIA World Factbook, na transfermarket.co.uk unaonyesha kwamba, ikiwa wachezaji wa Spain watataifishwa na kuuzwa, basi uchumi wao kidogo utapata nafuu japo sio sana.

Thamani ya kila mchezaji imefanyiwa tathmini kulingana na mikataba yao ya hivi karibuni na soko la usajili lilivyo sasa - ambapo mtandao wa transfermarkt.co.uk wamekadiria kwamba kikosi cha kwanza cha Spain ambacho kinahusisha wachezaji bora kabisa duniani kina thamani ya ujumla ya 400 million euros. Ukiwachanganya pamoja na walio benchi thamani inapanda mpaka millioni 658 za uero, ambazo zinaweza kulipa asilimia 0.05 ya pato la taifa la Spain. Hivyo kuwauza wachezaji hawa kama assests au kama dhamana inaweza kuwasaidia Spain kupunguza mzigo mkubwa kwenye uchumi wake ikiwa serikali ingekuwa inaweza kutaifisha timu za vilabu.

Kwa upana zaidi kwenye hili wazo lingekuwa na effect kubwa kwa vilabu vikubwa viwili vya nchi hiyo. Spain ndio nyumbani kwa klabu mbili ambazo ni moja ya vilabu maarufu zaidi duniani, F.C Barcelona na Rea Madrid C.F. Hivi vilabu viwili ndio timu zinazokusanya wachezaji maarufu zaidi duniani.

F.C Barcelona ndio nyumbanikwa mchezaji bora wa Euro 2012 - Andres Iniesta na mchezaji bora wa dunia Lionel Messi. Kwa pamoja kikosi cha Barca kina thamaniinayokadiriwa kufikia 603.5 million euros. Real Madrid wapo nyuma ya maadui zao, kikosi chao kina thamani ya 546.5 millioni euros, wakiwemo wachezaji kama Cristiano Ronaldo na Mesut Ozil. Pamoja, wachezaji wa vilabu hivyo wana thamani ya ujumla inayokaribia 1.15 billion euro au asimilia 0.14 ya deni la Hispania.

HIZI NDIO THAMANI ZA BAADHI MCHEZAJI MUHIMU WA VILABU
    •    Cesc Fabregas: 50 million euros.
    •    Xavi Hernandez: 35 million euros.
    •    Andres Iniesta: 65 million euros.
    •    David Silva: 46 million euros.
    •    Xabi Alonso: 35 million euros.
    •    Iker Casillas: 35 million euros.
    •    Fernando Torres: 35 million euros.

No comments:

Post a Comment