Hatimaye kocha aliyekuwa akisubiliwa kwa hamu na wapenzi na mashabiki wa klabu ya Yanga Tom Saintieft raia wa Ubelgiji amewasili nchini leo kwa ajili ya kukinoa kikosi cha Mabingwa wa soka kwa nchi za Afrika Mashariki na kati Yanga.
Akizungumza mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,kocha huyo amesema amekuja nchini kwa ajili ya kuiwezesha klabu ya Yanga kupata mafanikio, hivyo anawaomba Viongozi,Wapenzi na Mashabiki wa timu ya Yanga kumpatia ushirikiano katika kukiimarisha kikosi hicho.
Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo Kocha huyo alipokelewa kwa shangwe na mashabiki waliokuwa wamefurika uwanjani hapo na kupelekwa katika gari lililokuwa limeandaliwa kwa ajili yake na msafara huo ulielekea barabara ya Msimbazi yaliyopo Makao Makuu ya Watani wao Simba, huku mashabiki wa Yanga wakiimba nyimbo za furaha wakati Mashabiki wa Simba wakiwa wameduwaa wasijue la kufanya mara baada ya kumuona kocha mpya wa Yanga.
Saintfiet alipokelewa tena na Wanachama wa Yanga katika Makao Makuu ya Klabu ya Yanga na kupelekwa moja kwa moja katika ofisi ya Katibu Mkuu ambapo aliweka saini yake katika kitabu cha wageni.
Kocha huyo hapo kesho anatazamiwa kufanya mazungumzo mafupi na viongozi wa Yanga halafu ataingia Mkataba wa kuifundisha Klabu hiyo jioni katika uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya Klabu hiyo.
Haya Karibu. Uzuri wetu wapenzi wa Mpira hapa kwetu siku ukija unanukia vizuri saana!!!. Tutakupokea kwa shangwe zote, magazeti yote na Matv yatauza sura yako, tutakupa jina zuri, tutakusifia sana, na hasa ukishinda mechi tutakupa sifa unayotaka. Lakini baadaye utananuka vibaya mno!!!!, siku ukiondoka hakuna hata atakeyekusindikiza, watu hawatajua umeondoka lini!!!!. hakuna atakayekupiga picha ukiondoka. Karibu
ReplyDelete