Search This Blog

Monday, July 9, 2012

HATIMAYE FRANCIS CHEKA AFUNGIWA NA TPBO BAADA YA KUGOMA KUPIGANA NA KASEBA

Siku moja baaada ya kupanda ulingoni na kugoma kupigana na Japhet Kaseba - taarifa nilizozipata kutoka kwenye chama cha mchezo wa ngumi TPBO ni kwamba chama hicho kimefungia Francis Cheka kwa kutofanya nae kazi, wala kutoa kibali chochote cha pambano la aina yoyote limhusulo Cheka.
TAARIFA RASMI KUTOKA TPBO

NDG WAANDISHI WA HABARI   [MICHEZO]

AWALI YA YOTE NINAPENDA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWENU KWA JINSI AMBAVYO VYOMBO VYENU VYA HABARI VIMEKUWA VIKITUSAIDIA SANA KATIKA KUUKUZA MCHEZO HUU WA NGUMI ZA KULIPWA KWA KUUANDIKA VIZURI SANA NA HATIMAYE KURUDISHA IMANI KUBWA KWA WAPENZI WAKE AMBAO TAYARI WALIKUWA WAMEUKIMBIA KUTOKANA NA SABABU AMBAZO MNAZIFAHAMU FIKA ,NA HATA WADHAMINI KUKAA PEMBENI NA KUUTELEKEZA KABISA.

LAKINI MIAKA ANGALAU MINNE BAADA YA KUPOTEZA MWELEKEO HATIMAYE MASHABIKI WAMEUPOKEA TENA KWA MIKONO MIWILI ,

HIVI KARIBUNI TAYARI PEPO MBAYA AMEANZA KUJITOKEZA KWA LENGO LA KUUVURUGA TENA MCHEZO HUU AMBAO NI NGUVU KAZI YA VIJANA KTK KUJIPATIA PESA ZA KUJIKIMU KIMAISHA KUPITIA NGUMI ZA KULIPWA.

HIVI KARIBUNI VYOMBO VYENU VYA HABARI VIMEKUWA VIKIRIPOT TAARIFA ZA MVUTANO MKUBWA ULIOJITOKEZA KATI YA BONDIA FRNCIS CHEKA NA WAANDAAJI WA TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI KUHUSU PAMBANO LAKE NA JAPHET KASEBA HUKU CHEKA AKIKANUSHA KWAMBA HAKUSAINI MKATABA WA KUCHEZA NA JAPHET KASEBA NA BADALA YAKE ALISAINISHWA KUPIGANA NA BONDIA KUTOKA MISRI.HAPO TAREHE 07-07-2912 KTK UWANJA WA TAIFA

KIMSINGI TU CHEKA ANAJARIBU KUWAFANYA VIONGOZI WA KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA -TPBC HAWAJUWI WAJIBU WAO KWA KUMPA PROMOTA KIBALI CHA KURUHUSU PAMBANO AMBALO NI FEKI WAKATI SIYO KWELI ,

MIMI BANAFSI NILIPATA NAFASI YA KUONGEA NA CHEKA NI KWA NINI ALIPIMA UZITO HALI AKIJUA HATACHEZA PAMBANO ? NA KWA NINI ALIFIKA UWANJANI HALI AKIJUWA HACHEZI PAMBANO ? ALISHINDWA KUNIJIBU .MAHOJIANO HAYA TULIYAFANYA SIKU YA PAMBANO NDANI YA UWANJA WA TAIFA.

TPBO INAAMINI KWA DHATI KABISA KWAMBA LENGO LA FRANCIS CHEKA LILIKUWA NI KUJARIBU KUTENGENEZA MAAFA MAKUBWA AMBAYO YANGESABABISHA UVUNJIFU WA AMANI KWA KWA MASHABIKI AMBAO WALIKUJA MAHUSUSI KUANGALIA PAMBANO LILE .

NDG ZANGU WAANDISHI WOTE HEBU JIULIZENI KAMA PAMBANO HILI LINGEKUWA NI LA KAWAIDA NA LIMEPANGWA KUFANYIKA KATIKA UKUMBI WOWOTE ,NA PROMOTA AMESHAWATOZA WATU PESA NA WAMEJAA UKUMBINI ,NA KISHA FRANCIS CHEKA AMEINGIA UKUMBINI NA KISHA KUKATAA KUPIGANA JE MNADHANI MASHABIKI WANGEKUBALI ? NI LAZIMA WANGEFANYA VURUGU KUBWA AMBAYO INGEWEZA HATA KUPOTEZA MAISHA YA WATU WENGI SANA NA VYOMBO VYENU VYA HABARI VINGEKUWA NA KAZI KUBWA SANA YA KUWAHABARISHA WATANZANIA JUU YA MAAFA HAYO AMBAYO YANGESABABISHWA NA UJINGA WA MTU MMOJA TU FRANCIS CHEKA.

TPBO IMESIKITISHWA SANA NA TUKIO HILI AMBALO LIMEUVUNJIA KABISA HESHIMA MCHEZO HUU ,NA HASA UKUZINGATIA KWAMBA VIKUNDI MBALIMBALI VILISHIRIKI KUCHANGIA UJENZI WA MABWENI A WASICHANA ,NA HATA WAREMBO WALIJITOLEA KUPANDA ULINGONI KWA LENGO LA KUCHANGIA ELIMU.

TPBO INAWAPONGEZA WASANII WOTE WA BONGO MOVIE ,WANAMUZIKI WA AINA ZOTE ,NA WABUNGE WOTE KWA MOYO WAO WA HURUMA WALIOUNYESHA KUFANIKISHA LENGO LA TAMASHA HILO .PIA PONGEZI KWA MABONDIA WOTE WALIOKUBALI KUSHIRIKI KUCHANGIA

BONDIA FRANCIS CHEKA AMESHINDWA KABISA KUWATHAMINI WANAJAMII AMBAO KWA MCHANGO YAO WAMAWEZA KUMFANYA AJULIKANE TANZANIA NZIMA ,NA AMEWADHARAU SANA NA AMEUVUNJIA HESHIMA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA KWA UJUMLA  WAKE ,NA AMEUDHALILISHA SANA MCHEZO HUU MBELE YA JAMII YA KITANZANIA NA AMEWAFANYA MAADUI WASIOUTAKIA MEMA MCHEZO HUU KWA KUTOKUUDHANINI WAAMINI KWAMBA HUU NI MCHEZO WA WAHUNI NA WAVUTA BANGI .

                         IMANI ZA TPBO
                        -------------

KUTOKANA NA MAELEZO YOTE NILIYOYATOWA KWENU NI VIZURI PIA MKAJUWA IMANI   ZA TPBO

[1] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA INAAMINIWA NA WATANZANIA WOTE WAPENDAO NGUMI ZA KULIPWA KOTE NCHINI TANZANIA NA INAZINGATIA NIDHAMU NA INAPIGA VITA UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA MICHEZONI ,NA HATA BIASHARA YENYEWE YA MADAWA HAYO. KWA WANAMICHEZO WOTE NCHINI

[2] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA NGUMI ZA KULIPWA NI KAZI KAMA KAZI NYINGINE AMBAZO HUMPATIA BINADAMU KIPATO CHA HALALI ILI KUJIKIMU KIMAISHA.

[3]TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA HAKUNA BONDIA YEYOTE MWENYE AKILI TIMAMU AWEZAYE KUDHARAU JAMII IILYOMZUNGUUKA NA KUFANYA AWEZE KUFANYA MAMBO AMBAYO YATAIKERA JAMII HIYO .

[4] TPBO INAAMINI KWAMBA KILA BONDIA ANAZO HAKI SAWA ZA KUTETEWA NA KULINDIWA HAKI ZAKE PAKE ZINAPOKUWA HATARINI KUPOTEA.

[5] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA WAKUZAJI [MAPROMOTA] WATAPEWA MSAADA MKUBWA PALE WANAPOANDAA MAPAMBANO YAO NA WANAPATA USHIRIKIANO WA DHATI KUTOKA KWA MABONDIA ,IKWA NI PAMOJA NA KUTANGAZIWA MAPAMBANO YAO KWA USHIRIKIANO MKUBWA NA MABONDIA WAHUSIKA.

[6] TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA WANAZO HAKI ZA KUPATA BURUDANI YA MCHEZO HUU IL WAEENDELEE KUUPENDA KWA FAIDA YA MABONDIA WOTE .

[7] TPBO INAAMINI KILA BONDIA ANAPASWA KUHESHIMIWA NA HAKUNA BONDIA ALIYE JUU YA SHERIA NA KANUNI ZA MCHEZO ZIENDESHAZO NGUMI ZA KULIPWA.

NA TPBO INAAMINI KABISA KWAMBA  MWENYE MAMLAKA YA KUBADILISHA MPINZANI WA CHEKA NI PROMOTA NA SIYO BONDIA, NDIPO CHAMA HUSIKA KINATOWA KIBALI KWA AJILI YA PAMBANO HILO , NA NDIYO MAANA HATA RAIS WA TPBC KUPITIA VYOMBO VYA HABARI ALIUTANGAZIA UMMA WA WATANZANIA KWAMBA ANAITAMBUA MKATABA /MIKATABA ALIYOISANI FRANCIS CHEKA KUPAMBANA NA JAPHET KASEBA.

                     MAAMUZI MAGUMU YA TPBO
                    ---------------------------


\ KWA KUWA JAMII YA WAPENZI WA NGUMI ZA KULIPWA WAMEFADHAISHWA SANA NA TUKIO LILIOFANYWA NA BONDIA FRANCIS CHEKA NAMI NAUNGANA NAO KTK MFADHAIKO HUO NA KUWAOMBA MSAMAHA KWA TUKIO HILO , NA ILI KUHAKIKISHA KWAMBA SOTE TUMEFADHAISHWA NA JAMBO HILO-;

TPBO INAMUONDOWA  RASMI BONDIA   FRANCIS CHEKA KATIKA ORODHA YA MABONDIA INAOWATAMBUWA NA HAITAFANYA NAYE KAZI YA IANA YOYOTE KTK ULIMWENGU WA MASUMBWI KTK KIPNDI CHOTE CHA UHAI WA TPBO. NA UHAI WANGU BINAFI.

HII HAINA MAANA KWAMBA ANAKATAZWA KUCHEZA NGUMI , LA BALI HUU NI MSIMAMO WA TPBO , NA DAIMA MIMI HUIFANANISHA TPBO NA SIMBA DUME LENYE MENO NA AMBALO HALITAKI KULA MIZOGA , LAKINI KAMA VIKO VYAMA NINAVYODHANI KWAMBA BILA CHEKA HAVIWEZI KUIMARIKA NA VIMTUMIE SINA PINGAMIZI NAVYO.

TPBO IPO IMARA NA ITAENDELEA KUWA IMARA KWA KUFANYA KAZI NA MABONDIA WENYE NIDHAMU NA KATIKA MAAMUZI YETU HATUMUOGOPI YEYOTE ILI MRADI TUMO NDANI YA SHERIA NA KANUNI ZA MCHEZO



                  AHSANTENI SANA

NB- KWA TAARIFA HII NINAUFUNGA RASMI MJADALA KUHUSU BONDI FRANCIS CHEKA.

               IMEANDIKWA NAMI ;-
         YASSIN ABDALLAH -USTAADH
    RAIS-TANZANIA PROFESSIONAL BOXING ORGANISATION-TPBO

13 comments:

  1. TPBO?kwendeni zenu msitake kujisafisha wakati mliyajua haya tangu pambano linaandaliwa,kuna mambo mengi tu ya kipuuzi yametokea mmeyafumbia macho leo hii mnajifanya eti mmekereka sana na hili,mashabiki wa kaseba waliingia ulingoni kuleta vurugu hamkuwachululia hatua zozote za kinidham,mada maugo alidiriki kusema kua waamuzi wenu hua wamevuta bangi na kutoa kashfa nyingi dhid ya TPBO hamkufanya kitu leo hii hili la cheka mnajifanya kumind,tokeni hapa ama kwakua sio wa dar"?nyie wote ni wababaishaji cheka,kaseba na njaa zake pamoja na TPBO

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ushabiki wewe, Ina mana cheka wakat anasain mkataba hakujua km kaseba c saizi yake? Shule nayo muhmu jamani tusiendeshwe na imani za kishirikina. SAFI sana TPBO mana jamaa keshajiona TYSON wakat hata level za Matumla hajazifikia bado.

      Delete
  2. ukute cheka alienda kwa babu kuchungulia akaambiwa leo unachezea kichapo akaamua bora lawama kuliko fedheha

    ReplyDelete
  3. wewe kama umeingia mkataba na ukapima uzito hinakuwaje hutaki panda ulingoni huu ni huuni na huuni kama huu autakiwi sehemu yeyote ingekuwa kwenye ngumi za kawaida kwenye kumbi zetu si tungeuhana

    ReplyDelete
  4. inaonyesha jinsi gani mabondia wetu walivyokuwa vilaza..unapima uzito,unaingia uwanjani alafu unakataa kupambana..ni bola ungekataa tokea mwanzo na ata kupima uzito usingepima

    ReplyDelete
  5. Inaonekana Cheka ni kweli alijua atachezea kichapo ndio maana akaingia mitini lakini ajue amejitia aibu sana kaingia mkataba na kuchukua advance ni aibu + utapeli matokeo yake amesababisha shabiki wake mkubwa Mudi Tanga amekimbilia Nairobi kujificha kwa Aibu.

    ReplyDelete
  6. RAIS-TANZANIA PROFESSIONAL BOXING ORGANISATION-TPBO,LABDA UNGETUELEZA KIFUNGU GANI CHA SHERIA AMBACHO CHEKA AMEKIVUNJA KWA HIYO ADHABU YAKE NI KUFUKUZWA.NI KAMA VILE TONAVYOONA KWENYE SOKA.TUWEKENI WAZI KWA HILI.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani wew hujui kusoma nn km CHEKA, Si usome kwenye hizo document za juu zilizotolewa na TPBO zinazoonyesha sababu za kumfungia kilaza Cheka. Usituletee siasa kwenye mambo y U proffessional.Kuna mashirikisho meng y ngumi TZ, kw hyo anaweza kufany kaz na mashirikisho mengine na C TPBO.Hukuambiwa km hatocheza ngumi la hasha, ila TPBO wameamua kutofany nae kaz mana n aibu kwa shirikisho.Hii iwe fundisho kwa mabondia wote ambao huw wanakurupuka kusain mikataba hali y kuw bado hwajazungumza na kamati zao za ufund.

      Delete
  7. TPBO acheni chuki zisizo na tija mnamfungia cheka kwa kisa kutopambana na kaseba kwanza pambano lenyewe si la mkanda pili lina muongezea nini cheka au kaseba?nandani cheka alisha sema awali yeye km winner hapa tz hana mpinzani sasa kwann mumfosi apambane tena bila kuwa na mkana wowowte wale malaya wamepanda pale tunaambiwa wana act movie sasa si ni upuuzi ulikuwa,mtemeni cheka huyo ni bingwa kwa taifa zima linamtambua hila za kwanini mkanda upo moro hizo zinawakereketatpbo na wewe raisi wa tpbo,

    ReplyDelete
  8. yasin wewe una chuki binafsi na cheka kila mtu anajua ilo wewe ndio ulikuwa wa kwanza kumkataza Cheka asipande ulingoni katika pambano lake la Morogoro na Maugo kwa kuwa ukuandaa wewe sasa leo inakuwaje unafungia kwa kutopanda jukwaani

    ReplyDelete
  9. yasin una chuki binafi na Cheka unakumbuka wewe kupitia vyombo vya habari ulikuwa unamkataza Cheka asipande jukwaani kupambana na Mauogo katika pambano la Morogoro kwa kuwa ukuandaa wewe pambano je leo unamfungia Cheka kwa kutopanda jukwaani uoni aibu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwan lazma cheka kufany kaz na TPBO, wew vp? Yeye c bingwa wa mabara na aendelee na ubingwa wake sasa. We unadhan alichokfany cheka n sahh? Chek hana sababu z mcng z kutopambana na Kaseba. Kwan yy hajui kusoma? Kw nn alisain mkataba?

      Delete