Search This Blog

Tuesday, July 31, 2012

BRAZILI NA MIAKA 50 YA OLYMPIC: MFUPA ULIOWASHINDA PELE, RONALDINHO, NA RONALDO - WATAUWEZA NEYMAR, OSCAR, MOURA NA WENZAO???

Brazil - jina ambalo ni vigumu kuacha kulitaja unapozungumzia soka. Kutoka kwa Pele mpaka kwa Ronaldinho na Socrates mpaka kwa Neymar, hakuna ubishi kuhusu ufalme wao wa soka.

Hivyo kwanini, mabingwa hawa wa mara tano wa kombe la dunia, mara nyingi kuliko nchi yoyote, wakiwa na jezi zao rangi ya njano na kijani hawajawahi kuwa na mafanikio kwenye michuano ya Olympic?

Jumapili, 29, July 2012 itakuwa siku ya kukumbukwa kwa soka la Brazil. Katika miaka 50 ya kucheza Olympic tangu walipoanza kushindania kombe la michuano mwaka 1952 iliyofanyika Helsinki - Nermay akafunga bao la 100 ya nchi katika michuano hiyo ya Olympic.

Hii ni mara ya 12 Brazil inashiriki Olympic kwenye soka, je utakuwa mwaka ambao hatimaye watashinda medali ya dhahabu?,  mchezaji ambaye mfalme wa soka duniani Pele anasema ni mkali kuliko Lionel Messi - Neymar alipoulizwa kwamba mwaka huu Brazil wataondoa mkosi wa kutokufanya vizuri kwenye Olympic alijibu: " Kiukweli sijui, ni michuano migumu kuna timu nzuri nyingi sana, lakini tutacheza kwa jitihada zote."

Mwaka 2008 walikuwa na kikosi kikali sana, wakiongozwa na Ronaldinho, Thiago Silva na Alexandre Pato, lakini wakapigwa kipigo kibaya na mahasimu wao Argentina, wakifungwa mabao 3-0. Lakini baada ya Spain kutolewa mapema baada ya kufungwa na Japan na Honduras, mabingwa watetezi Argentina wameshindwa kufuzu, labda safari hii wanaweza kupata kile wanachokitafuta kwa takribani miaka 50.

Brazil tayari wameshapita kwenda robo fainali huku wakiwa na mechi moja mkononi, wanaweza kukutana na Honduras kwenye robo kuelekea nusu fainali.

Kwenye karatasi tayari wameshaonekana wao ndio wanaopewa nafasi ya kuwa mabingwa. Je huu ndio mwaka ambao akina Nermar watafanikiwa kuutafuna mfupa uliowashinda kaina Pele, Ronadinho na Ronaldo? Je wao ndio watakuwa mabingwa watetezi huko Rio De Jeneiro 2016? Muda pekee ndio utasema ukweli.

No comments:

Post a Comment