Derrick Walulya mchezaji wa timu ya URA FC kutoka nchini Uganda ambaye aliwahi kuchezea timu ya Simba pia ya Tanzania akimiliki mpira mbele ya Felix Sunzu mshabuliaji wa timu ya Simba katika mchezo wa kuwania kombe la Kagame linaloandaliwa na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika Mashariki CECAFA unaochezwa kwenye uwanja wa Taifa jioni hii mpaka sasa mpira umekwisha na timu ya URA imeifunga timu ya Simba magoli 2-0. magoli hayo yamefungwa na mchezaji Feni Ali wa URA FC.
Waamuzi wakiongoza timu kuingia uwanjani tayari kwa kuanza mchezo huo.
Wachezaji wa timu za Simba ya Tanzania na URA ya Uganda wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Watangazaji wa kituo cha televisheni cha Supersport cha Afrika Kusini wakitoa tathmini ya mchezo huo kabla ya timu hizo kukutana ambapo inaonyesha kuwa Simba mara nyingi imekuwa ikifungwa na URA FC wakati timu hizo zinapokutana katika michuano mbalimbali.
Mashabiki wa timu ya Simba wakiwa wamefurika katika uwanja wa Taifa kujionea timu yao ikicheza na Waganda URA FC. (Picha kwa hisani ya fullshangwe.blogspot.com)
NINGESHANGAA KUONA MAFURIKO YAMEMBEBA MBAMBA ALAFU KEENGE YAMWACHE!!?. HONGERA SIMBA NA WANASIMBA WOTE ENDELEENI KUSHANGILIA YANGA KAFUNGWA
ReplyDeleteNaona baada ya kushindwa kujizuia kwa unazi umetoa matokeo,jana ulikuwa unatoa update kila dakika,shaffih acha hizo bwana
ReplyDeleteAsante kwa analysis nzuri leo kwenye Sport extra kama Simba wangekusikiliza huenda matokeo yangekuwa walau tofauti kidogo maana uliweka shilingi yako kwa URA mimi Yanga damu lakini mpira Tanzania kama alivyosema kaduguda ktk analysis yake jana kwenye Nipashe basi bado tuna kazi ndefu kufikia ktk soka la kisasa na wala tusitarajie maajabu yeyote iwe klabu au timu zetu za taifa tanzania bado kabisa hata hatujaanza safari yenyewe
ReplyDeleteWapi Simba, mbona leo mmekua kimya? Yapi yamewasibu leo? Mwenzio akinyolewa, zako tia maji..
ReplyDeleteKWAKWELI SHAFII JANA UMEONYESHA UNAZI WAKO SIJAONA MUELEKEO WA MECHI UKIRIPOTIWA KAMA MECHI YA JUZI KEEP IT UP BOY..
ReplyDeleteshafii umezidisha unazi!kitakachokuja kusibu cku moja ni kuvunjiwa heshma mbele za watu au kuwa adui wa upande flani!
ReplyDelete