Search This Blog

Tuesday, July 31, 2012

AZAM INA MALENGO MAZURI ILA INA MAPUNGUFU NA KWENYE BENCHI LA UFUNDI

Kidogo niongelee soka la bongo japo kuwa sio mzoefu sana lakini haya ndio mawazo yangu.
 

Timu kubwa nchini ni Simba Sports Club na Dar Es Salaam Young African tukubali, ni kweli Azam FC imekuja na kuleta changamoto si kwa timu hizi bali kwa ligi kama msimu uliopita, lakini kwangu mimi nimeona kuwa kidogo ndugu zetu Azam walijisahau kuwa Simba na Yanga bado ni timu kubwa na wao ndio kwanza wanaanza kupanda. Sawa nakubali kabisa kuwa Azam iko well Organized, lakini the way kwa tathmini fupi niiyoiona katika mashindano ya kombe la Kagame hasa baada ya wana rambaramba kuiondoa Simba Sports club kwa mabao 3 kwa 1, walijiona wamemaliza kila kitu hali iliyopelekea kuleta dharau na kejeli na baadhi ya wadau kuanza ku-support kejeli zile, ilifikia wakati timu hizi Simba na Yanga zikifananishwa na mapacha wawili yaani "Kulwa - Yanga, Doto - Simba" na aliyebuni majina haya ni mtu wa soka na mpenda soka na kufanya kuzidi kupelekea jeuri na kujiamini kabisa "Kulwa na Doto" zitakuwa chali.

 Tatizo kubwa nililoliona hapa ni kwa wana rambaramba walidhani timu hazibadiliki kimchezo kama Azam {waanayoona iko well organized} Azam wana malengo mazuri sana kuhusu timu yao lakini uwezo wa kiufundi ndo umeishia pale. Nilikwambia siku ile waliyocheza na Vita kwamba Azam hawana plan B, na ndicho kilichojitokeza mechi ya fainali. Wanacheza formation moja, hawawezi kubadilika kutokana na mchezo
 

Ninavyohisi "sina uhakika kwa hili lakini kutokana na maneno ya wapenda soka, na lisemwalo lipo kama halipo?"  Hata wenyewe wanasema wako modern but wanapita mulemule zinapopita Simba na Yanga.
 

Kuna mtu aliniambia "Tangu lini club ikatoa tuzo kwa waandishi wa habari? Kama sio wanatengeneza mazingira ya kuwasifia hata kama wanafanya madudu! Azam nakubali wana malengo mazuri lakini njia wanazopita nao ni utata!" nilimbishia lakini ujumbe wake ulinifikia

Suala la Mrisho Ngasa kuvaa jezi ya Yanga,  kwangu mie naona wote wana makosa, Ngassa ameshindwa kutambua mpira ndio kazi yake na Azam ni mwajiri wake,  na Azam nao pia wameshindwa kuibadili mind ya Ngasa ili ajisikie yuko nyumbani. Kama mlimchukua kwa ajili ya kuleta mafanikio kwa klabu na mnaona anawaza kule alikotoka lazima mkae nae na mumuondoa kule ajisikie huku alipo sasa kuna ubora pia, ninaamini ipo siku Ngassa atafunguka kwanini alikubali kuvaa jezi ya Yanga inawezekana ni kweli kutokana na mapenzi aliyonayo kwa klabu ya Yanga lakini ile siku ya hili tukio wadau walimtaja mchezaji mwingine wa wana rambaramba kuwa yeye amekulia Yanga kabisa lakini walimpongeza wa kutokufanya kama Ngassa yaani kujionyesha hadharani, lakini pia tunaweza mlaumu Ngassa kwakua hatujui upande wa pili wa shilingi, sakata hili wanaoweza kutuondoa katika matongotongo ni Ngassa na Azam FC.

Kuna wachezaji wala mie naona hawastahili kupata namba lakini utashangaa wanapata #. Hivi Hamis Mcha ni mtu wa kumweka Ngassa benchi?   Kiwango cha George Odhiambo "Blackberry" kinaendana na sifa alizokuwa anapewa? au siku zile Blackberry ilikuwa Whiteberry?

Kiongozi wa klabu anaandika post Facebook za kuponda na kukashifu timu nyingine na kuona anayofanyia kazi ni bora sana hali inayofanya anakiuka hata taratibu za kazi na wadhifa alionao.

Wasipoangalia wataishia kuwa na viwanja vizuri, gym, hostel nzuri lakini kiuwezo wa uwanjani wakabaki vilevile.

Kiongozi anaongea na chombo cha habari anasema eti wachezaji Azam hawajazoea kucheza mbele ya watu weng ndio maana wamefungwa! Hivi Ngassa, Nyoni, Tchetche,Bocco, Sure boy, Shikanda , Blackbery na Agrey Moris hawajawahI kucheza mbele ya watu wengi? Ah hapa kachemka, aseme lingine.

Wanataka dola 50000, sawa inawezekana wanahitaji kurudisha gharama zao lakini isije ikawa ni kumkomoa Ngassa, na kuna tetesi kuwa wanataka kumpeleka Simba na kuifanyia Yanga fitna isimpate, ama ndio ile ishu tuendelee kuamini kuwa Simba Sports Club na Azam FC ni ndugu?

Ndio nasema unaweza kuwa na viwanja , apartments na gym nzuri lakini bado ukawa na team mbovu. Ukishindwa kwenye technical bench na kuijenga timu psychological ujue hauwezi kufika popote. Azam wanasema wako well organized lakini technically hawana tofauti na Simba na Yanga. Tofaut yao ipo kwny physical infrastructures tu.

Mwisho nawashauri Azam kwamba wajitahidi kuboresha na bench la ufundi pia, miundo mbinu yao haitasaidia chochote kama technical bench liko weak. Shule inaweza kuwa na kila ki2 {vitabu, madarasa, library nzuri} lakini isipokuwa na walimu bora wanaojua kumpa mwanafunzi maarifa na mbinu za kufaulu hiyo shule haiwezi kufaulisha.

Pia wawajenge wachezaji wao kisaikolojia ili wajione ni sehemu ya mafanikio ya Azam. Na ndio nasema hata Azam nao wana makosa, wameshindwa kumfanya Ngassa ajisikie yupo nyumbani, na kama wakiendelea kubaki na timu ile hawatafika kokote kwa sababu tangu Azam ya akina  marehemu Mafisango hadi hii ya leo haijabadlika chochote. Inacheza mpira uleule .

Huu ni mtazamo wangu mie, kila mmoja ana uhuru wa kutoa mtazamo wake na tupende kupata challenges.


Imeandikwa na mdau wa mtandao huu.

8 comments:

  1. Well said mdau, cha msingi kwa azam ni kuangalia ni jinsi gani watajijenga kitimu zaidi kuliko kunyosheana vidole. Waangalie ni vp wanaweza kuongeza nguvu kwenye timu yao. Mambo ya kumtafuta mchawi ni nani kwenye mech ambayo wachezaji wao walizidiwa ubunifu na timu pinzani ni kujirudisha nyuma wenyewe. Nilitegemea azam watawapongeza wachezaji wao kwa kuji2ma hadi kufika hatua ya fainali, lakini wao wanawalaumu na kuwaona hawana mchango. Hii itasababisha wachezaji kushndwa kujiamini cz hawaaminiwi na viongozi wao.
    Nlipenda azam iwe timu ya mfano hapa tz lakin inakoelekea, ni wazi itakua kama kurwa na doto {simba na yanga}

    namaliza hivi; mchawi wa azam ni yule wanaemuona kwenye kioo cha kujitazama.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  2. Azam ina miaka isiyozidi kumi simba na yanga zina miaka zaidi ya 50 na babo hazina mbele wala
    nyuma azam baada ya miaka 5 itakua mbali sana acha unazi mtoa mada azam wamejipanga

    ReplyDelete
  3. kuna point kadhaa ningependa kuzungumzia

    1)lack of plan B. ni kweli kabisa kuwa azam ilishindwa kubadilika katika mchezo wa fainali. ukosefu wa mbinu mbali mbali katika final third ndio ilikuwa tatizo kubwa la azam. nakubaliana na wewe kuwa labda kubadilisha mfumo kutoka 4-2-3-1 kwenda 4-3-3 ungeleta mafanikio. kiufundi ili kubadilisha mchezo inahitaji wachezaji ambao wanauelewa mkubwa wa mchezo na pia bench lako lazima liwe na wachezaji ambao wanaweza kutekeleza maelekezo mapya. so inawezekana kuwa kocha wa azam alikuwa na wasiwasi kuwa angebadilisha maelekezo basi angevuruga mwenendo wa mechi. lengine zakuzingatia ni kwamba yanga walikuja pale wakiwa na lengo la kulinda goli na kama ujuavyo ni vigumu sana kucheza dhidi ya timu inayo defend tuu.
    credit lazima iende kwa kocha wa yanga kwa kutumia mfumo ambo kwa wengi unaonekana umepitwa na wakati. nina hakika makocha wengi sana wangepata shida kutafuta mbinu za ushindi dhidi ya huu mfumo. kwa mfano espania walipata shida dhidi ya italia katika uero mechi ya makundi na pia juventus waliweza kushinda ligi ya italia bila kufungwa kwa kutumia huu mfumo.

    katika mechi dhidi ya vita kipindi cha pili azam walibadilika kwa kutumia sana upana wa uwanja na pia kupiga cross ambao bao lao la kusawazisha lilitokana na cross.

    2)ishu ya ngasa; stewart hall alisema kuwa ngasa analamba benchi kwa sababu yeye anataka aone jitihadi zaidi kutoka kwake both mchezoni na mazoezini. sasa kweli ngasa anaweza kuwa na kiwango kuliko hao wachezaji wengine lakini ukweli wa mpira ni kwamba talent gets you into the game but hardwork makes champions. makocha wengi wapo radhi kumpanga mchezaji ambaye ana kiwango kidogo lakini ana juhudi kuliko mchezaji mwenye talent lakini hajitumi. lionel messi wakati wa copa amerika last year argentina walipewa a day off na kocha lakini yeye alienda uwanjani kufanya mazoezi binafsi...na huyu ndie mchezaji bora duniani. hivyo katika sakata lote hili ni ngasa ndio atapoteza vingi kama sio kuwa mwisho wa career yake maana kama timu hazitafikia dau wanaotaka azam yeye ataendelea kulamba bench.

    ReplyDelete
  4. Well said mdau, cha msingi kwa azam ni kuangalia ni jinsi gani watajijenga kitimu zaidi kuliko kunyosheana vidole. Waangalie ni vp wanaweza kuongeza nguvu kwenye timu yao. Mambo ya kumtafuta mchawi ni nani kwenye mech ambayo wachezaji wao walizidiwa ubunifu na timu pinzani ni kujirudisha nyuma wenyewe. Nilitegemea azam watawapongeza wachezaji wao kwa kuji2ma hadi kufika hatua ya fainali, lakini wao wanawalaumu na kuwaona hawana mchango. Hii itasababisha wachezaji kushndwa kujiamini cz hawaaminiwi na viongozi wao.
    Nlipenda azam iwe timu ya mfano hapa tz lakin inakoelekea, ni wazi itakua kama kurwa na doto {simba na yanga}

    namaliza hivi; mchawi wa azam ni yule wanaemuona kwenye kioo cha kujitazama.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  5. mtoa mawazo alikuwa yupo sahihi ila alipofika katika suala la ngasa kajichanganya sana,kwa hali yoyote ile duniani kwa mtu ambae soka ndio maisha yake ni upuuzi kufanya kitendo kama alichafanya ngasa ni vizuri kumwambia ukweli ili siku nyingine asijisahau,wachezaji wengi duniani wanaweza kuwa na mapenzi na timu fulani lakini si rahisi kufanya aliyoyafanya ngasa kwani ni kuua soka lake,kama yanga wasipomsajili ina maana hakuna timu itakuwa na imani nae tena,pili alifanya kitendo hicho wakati mechi iliyokuwa inafuata ni dhidi ya yanga,hapo hata sijaona makosa ya azam kukaa benchi sio tatizo wamekaa wakina okocha na walivumilia mpaka wakafika mbali,tunajua pia kuna wachezaji waliopo katika simba na yanga kwa miaka mingi na mapenzi yao kitimu yapo katika timu nyingine,nina maana anaweza akawa yupo simba ila mapenzi yake yapo yanga na wanajituma na kucheza kwa bidii pindi timu hizo zinapokutana,sitaki niwataje kwa majina ila nadhani hata mtoa mada analijua hilo,kwa mimi binafsi ningemshauri ngasa kuwa soka ndio maisha yake na maisha yapo popote hivyo kitendo alichokifanya kitamharibia maisha yake na soka kwa ujumla,azam ni timu inaweza kusajili hata kama yeye ataondoka lakini je yeye yanga wasipomsajili nani atamuamini esepecially hiyo timu itakapokutana na yanga?

    ReplyDelete
  6. Watu wengi walikuwa wanamatumaini kuwa Azam itasaidia kubalisha taswira ya mpira wa Tanzania(Simba na Yanga) lakini kwa hili naona nao wameanza kufuata mfumo uleule wa Simba na Yanga.Kuna mdau amesema kuwa waangalie kwenye benchi la ufundi ,wachezaji wanaonunua waendane na mfumo wao.
    1.Mfumo wa Azam unawalimit sana wachezaji kuonyesha vipaji vyao kocha anafata mfumo wa kiingereza ambao mchezaji mzuri ni yule mwenye work rate(Morris,Mourad,Bocco,Shikanda) kubwa.Ukweli ni kwamba Ngasa hafiti kabisa kwenye mfumo wa Azam,hachezi free kama alivyokuwa Yanga.Ukiangalia huu mfumo unamuwesha Bocco peke yake kufunga magoli ndio maana asilimia kubwa ya magoli ya Azam anafunga yeye.Angalia magoli waliyofunga viungo wao Sure Boy,Cheche,Ngasa,Redondo ni machache sana.

    2.Tunawaumu sana Simba na Yanga kwenye usajili wa wachezaji lakini Azam pia ilisajili wachezaji wengi ambao baada ya kutua Azam walichemsha tofauti na walivyokuwa timu nyingine mfano Mafisango,(kipa mzungu wa Yanga),kuna mabeki wa Nigeria/Ghana(sina uhakika),Kipre Balou

    3.Issue ya Mrisho Ngasa,ni kweli Ngasa anaipenda Yanga na alikwenda Azam sababu ya fedha,Azam hawakugundua mfumo wa pale haumfai na kiwango chake kimeshuka.Azam walitakiwa kufanya mipango ya kumuuza mapema na sio mpaka kusubiri abusu jezi ya Yanga.Naamini wangemuuza kwa dau kubwa kuliko waliomnunulia kwa Simba/Yanga/Coastal au hata timu za nje.Jinsi walivyo-handle hii issue kwa sasa Yanga tu ndio wanaweza kumchukua sidhani kama Simba watamsajili mtu ambaye wanajua ana mapenzi na hasimu wake.Pia sidhani kama kiwango wanachohitaji Azam ndio thamani ya Ngasa kwa sasa ,labda nusu ya fedha waliyomnunulia

    ReplyDelete
  7. Naunga mkono hoja ya "mleta mada" sasa kwenu wote mnaojifanya kulalamikia kitendo cha Ngassa kwenda kushangilia goli lake na mashabiki wa Yanga,hivi mmeshapata muda wa kusikiliza maelezo yake au mnabwabwaja tu?
    Ngassa amesema alilitoa lile goli lake alilofunga kama zawadi kwa mashabiki wa Yanga na ndo maana alikwenda pande ile kushangilia nao kwa sababu kuu zifuatazo:-
    1.Licha ya kuwa mchezaji muhimu kabisa katika team yao alipoondoka(ku'sign) Azam mashabiki wa Yanga hawakumchukia wala kumzomea mara zote alizokuwa akichezea team yake mpya badala yake mara zote wamekuwa wakimshangilia jambo ambalo linaonyesha licha ya kuwakimbia lkn bado wanampenda kama walivyokuwa wanampendaa alipokwa anaichezea.
    Mashabiki wa Yanga wameonyesha ustaarabu wa hali ya juu unlike mashabiki wa Simba ambao kila siku kazi yao ni kuzomea wachezaji ambao wameihama team yao ilhali bado wanawahitaji,angalia wanavyokazana kumzomea Kelvin Yondani sasa hv,hadi inatia huruma angekuwa si mchezaji matured leo hii Kelvin angekuwa hata namba hapati Yanga ksbb angekuwa anaharibu mchezoni.
    Sasa katika situation kama hii kwanini asiwashukuru mashabiki wa team yake ya zamani? au cha ajabu nini katika hili,mbona Thiery Henry wakati akicheza soka la ushindani kule Barcelona ilipocheza na Arsenal alionyesha mapenzi kwa mashabiki wa Arsenal na haikuwa issue.
    2. Ngassa amechefuka na mazingira ya Azam ya sasa hv,kila siku wanamshutumu kwamba bado ana mapenzi na Yanga na ndo maana hachezi vizuri Azam inapocheza na Yanga,ushuzi mtupu...hivi kama Ngassa anacheza mechi dhidi ya Tusker ya Kenya na anashindwa kufunga inakuwaje anapocheza mechi dhidi ya Yanga na kushindwa kufunga ionekane alicheza chini ya kiwango?
    Halafu mimi napenda kuongezea kitu...mtoa mada amesahau point 1...point ya hawa viongozi wa Azam kuanza kuwashika uchawi baadhi ya wachezaji wao just ksbb wana uhusiano na watu wa Yanga au watu waliowahi kucheza Yanga,huku ni kuwavunja moyo hawa Vijana,walianza kwa Ngassa sasa wameingia kwa Salum Aboubakar,huku ni kumvunja moyo Dogo wanataka kuharibu kipaji chake kama walivyofanya kwa Ngassa.
    Ni ukweli usiopingika kama Azam hawatabadilika wataishia kuwa na kiwanja kizuri,Hostel nzuri na miundo mbinu mizuri lkn hawatakuwa na maendeleo yeyote ya maana katika soka na si ajabu ije kufa ama ilivyokufa Kajumulo sijui team gani ile iliyoanzishwa na Kajumulo

    ReplyDelete
  8. "Azam ya kina marehem mafisango hadi hii ya leo haijabadilika chochote, inacheza mpira ule ule" hahaha umeona pumba hii? kaka ama kweli hujakosea ulivyosema kuwa hufuatilii soka la tanzania, unataka kocha awapange wachezaji wako ulowazoea? eti mcha na blackberry hawafai..haha. kaka muachie kocha afanye kazi yake na yeye ndo aliyewafikisha final ya kagame, kocha anajua ni i anachokifanya, kama azam kufungwa na yanga final hilo sio tatizo yale ni matokeo ya mpira, lakin sio suala la kuzungumza hizo pumba hapo juu..anyaway ni mawazo yako lakini ni mawazo potofu azam ipo katika kipindi cha mpito na itakuja kufanikiwatu, kama walipopita man city watu walisema hawatachukua premier league na wamechukua. ok brother ila hongera makala yako sio mbaya umejitahidi.

    ReplyDelete