Kanuni za ligi kuu ya Vodacom kama zilivyorekebishwa na kupitishwa tarehe 20 julai 2009 na kusainiwa na Rais wa TFF bwana L.C. Tenga na bwana F. Mwakalebela aliyekuwa Katibu Mkuu zinaeleza kinagaubaga jinsi shuguli za usajili na uhamisho wa wachezaji zinavyobidi kufanywa.
Msimu unapokwisha kanuni ya 49 inaeleza kwamba” klabu itawasilisha TFF kwa maandishi, majina ya wachezaji watakaositisha mikataba yao/ kuwa huru katika usajili wa msimu wa ligi katika muda wa uhamisho utakaotangazwa na TFF na kitalazimika kumpa taarifa ya maandishi/ mchezaji au wachezaji husika”. Kanuni hii inaipa mamlaka klabu kwamba ndiyo yenye kuitaarifu TFF juu ya mchezaji yupi yuko huru na ambaye hayupo huru, Simba Sports Club haijawahi kuiandikia TFF juu ya mchezaji Kelvin Yondani kuwa huru na isingeiambia kwamba yupo huru kwa sababu ana mkataba aliousaini tarehe 23/12/2011 ambao kwa mujibu wa kanuni ya 46 mkataba huo unapashwa kuwasilishwa kwa pamoja na mikataba mingine kwa ajili ya usajili wa msimu wa 2012/2013 kama kifungu hicho kinavyosema “Kilabu zinatakiwa kukamilisha na kuwasilisha kwa pamoja usajili wa timu zote mbili pamoja na majina na mikataba ya makocha wa timu za wakubwa na vijana katika kipindi cha usajili” Kifungu namba 40 kinaeleza kwamba maombi ya usajili wa mchezaji wa kulipwa lazima yawasilishwe pamoja na nakala ya mkataba wa mchezaji, hivyo wakati wa usajili mkataba wa kuendeleza mkataba uliopita kati ya Simba na Kelvin Yondani ndipo unapopashwa kuwasilishwa ingawa Simba imeuwasilisha mapema ili kulionyesha shirikisho hali halisi inayoendelea.
Pamoja na Simba kutoiandikia TFF kwamba Yondani ni mchezaji huru kwani muda haujafika pia kanuni za TFF na zile za FIFA za Regulation on the Status and Transfer of Players katika article 18 na kanuni za TFF katika kanuni ya 44 ambazo zipo “mutatis mutandis” kwa maana kwamba zimenakiliwa herufi kwa herufi lakini zimetofautiana lugha kwani moja ni kiingereza na nyingine ni Kiswahili inaeleza kwamba “kilabu inayotarajia kuingia mkataba na mchezaji wa kulipwa haina budi kuiarifu klabu yake ya sasa kwa maandishi kabla ya kufanya makubaliano na mchezaji wa kulipwa. Mchezaji wa kulipwa atakuwa huru tu kujingia mkataba na klabu nyingine iwapo mkataba wake na kilabu yake ya sasa umekwisha au utakwisha baada ya miezi sita. Uvunjaji wowote wa sharti hili utastahili vikwazo vinavyofaa.
Hili pia limeelezewa katika kanuni ya 57 (1) kwamba “Kilabu kinachotaka kumsajili mchezaji aliyesajiliwa na kilabu kingine au mwenye mkataba na kilabu kingine, kitalazimika kuafikiana na kilabu chake kabla ya kumsajili mchezaji huyo”. Sababu kubwa ya kuhimiza mawasiliano baina ya klabu mbili ni kwanza kujua kama mchezaji huyo ana mkataba wa nyongeza na timu husika lakini zaidi ya hayo ni kuhakikisha kwamba mchezaji huyo haathiriwi na mazungumzo ya timu nyingine wakati anatekeleza mkataba uliobaki. Yanga walichofanya ni kumrubuni mchezaji kwa kuongea nae bila kibali cha Simba Sc lakini pia wangeomba kibali Simba Sc ingewaeleza kwamba mchezaji huyu ana mkataba mwingine alioisha usaini. Kwa mujibu wa kanuni za TFF na FIFA kitendo cha Yanga kuongea na mchezaji wa Simba SC bila kuiandikia simba chochote ni kosa kubwa sana ambalo Simba inaishitaki Yanga iadhibiwe kwa kufungiwa usajili wake wote wa mwaka huu na mwaka ujao.
Pamoja na hayo timu haiwezi kumsajili mchezaji ata kama amekuwa huru bila kuwasiliana na klabu yake ya zamani kwani idhinisho la usajili lazima litolewe na klabu yake ya zamani kama kanuni namba 57 (2) inavyoelekeza hivyo hakuna namna yoyote ambayo Yanga inaweza kumsajili Kelvin Yondani bila Simba kupewa taarifa kwanza. Hili limesisitizwa zaidi katika kanuni ya 45 (6) kwamba “mchezaji ambaye ameingia mkataba wa zaidi ya msimu mmoja hatoruhusiwa kujisajili na klabu kingine kabla ya klabu yake mpya kuafikiana na klabu yake ya zamani” mkataba ulioisha wa Kelvin Yondani ulikuwa ni wa miaka miwili na ulioongezwa ni wa miaka miwili pia.
Mabezo haya yanaitia yanga hatiani kwa pande zote kwani maamuzi ya kama Kelvin ni mchezaji huru yanatolewa na Simba SC kama ikiwasilisha barua TFF juu ya wachezaji ambao wanamaliza mikataba au wanasitisha mikataba. Simba SC haijafanya hivyo kwa sababu muda wake bado, kwa mantiki hiyo yoyote anayetaka kujua mustakabari wa Kelvin inabidi awasiliane na Simba SC na jibu atakalopata ni kwamba Kelvin sio mchezaji huru, ana mkataba na Simba ambao kausaini na kuutia dole gumba (dole gumba lina alama za kipekee za mhusika ambazo hawezi kuzikana kama ilivyo kwa DNA).
Yanga wamefanya uhuni wa kumsajili Kelvin Yondani usiku wa tarehe 6/6/2012 kwa ushahidi uliopo, lakini wanasema mkataba umesainiwa ama October 2011 au February 2012, Simba SC itamshitaki wakili yoyote katika Tanganyika Law Society ambaye atashuhudia mkataba huo kwa kuurudisha tarehe za nyuma na kuomba chama hicho cha mawakili kimsimamishe mhusika uwakili.
Big up kaka Shaffi kwa kufuatia hili jambo endelea kutupa habari
ReplyDeletetumeshakuzoea shaffih, unazi mwingi zaidi ya uhalisia... nilikua nakuheshimu sana ila anzia uingie kwny siasa za simba na yanga heshima imevunjika...
ReplyDeleteSIONI TATIZO HAPO SIMBA NA YANGA WOTE WANA MAKOSA KWAHIYO NGOMA DROO.SIMA WALIPO MSAJILI RAJABU JEBA WA AZAM HAWAKUFUATA TARATIBU HIZO AMBAZO ZIMEBANDIKWA HAPO JUU. HAYA NA SASA HIVI SIMBA WAMEMSAJILI KIGGI MAKASY AMBAYE MKATABA WAKE UKO HURU BAADA YA KUISHA. SAS JE YANGA NDIYO WAMEIARIFU TFF?
ReplyDeleteHIZI NI MBIO ZA SAKAFUNI. SIMBA NA YANGA WOTE SIO WAUMINI WA SHERIA NA TARATIBU. NI AZAM PEKEE NDIO KLABU PROFESSIONAL.
HAWA WENGINE WASANII TU NA TUMEZOE MAGUMASHI MAGUMASHI TU.
SIJUI MWISHO WAKE UTAKUJA KUWA NINI? TATIZO HAPA LINAONEKANA NI KELVIN YONDANI MABEKI WALIKUWEPO WAKINA VICTOR COSTA ENZI ZAO WALIONDOKA NA SIMBA IKABAKI IMARA, JUMA KASEJA ALIENA YANGA SIMBA IKABAKI IMARA, ATHUMANI CHUJI ALIKWENDA YANGA SIMBA IKABAKI IMARA. SASA KULIKONI MZEE RAGE KUTAPATAPA? ALIKUWEPO PATRICK OCHAN, MBWANA SAMATTA, DANY MRWANDA,BEKI MAHIRI JOSEPH OWINO WOTE HAWA WALIONDOKA NA BADO SIMBA IMEFIKA MBALI SANA KWENYE MASHINDANO YA CAF AMBAYO WAMETOLEWA NA SHANDY AL AHLY. KWAHIO MZEE RAGE ASIWE NA JICHO LA HAPA AANGALIE MBALI. KEVIN YONDA MSIMU ULIKWISHA HAKUCHEZA MECHI NYINGI NA BADO SIMBA IMEKUWA BINGWA. TUWACHE HIZI HULKA MBOFU MBOFU. KAMA KWELI ALIKUWA ANAMTAKA YONDANI ASINGEMSIMAMISHA AU KUMKWAZA KWA MECHI NYINGI AMBAZO BWANA YONDANI ALIKUWA MWANZA.
NAHISI RAGE ANATAKA KUMHARIBIA KELVIN YONDANI (PERSONALY) NA WALA SIO KATIKA DHIMA NZIMA YA MICHEZO.
HAYA NDIO MAONI YANGU.
wewe nawe chizi kabisa unaemtoa heshima shaffih dauda. ukweli ni kwamba sikubaliani na kila anachokisema dauda lakini hapa alichofanya ni kutafsiri sheria je kosa lake lipo wapi? hili ni somo zuri kwenu nyinyi mazuzu ambao hukurupuka na kushabikia jambo bila kujua hali halisi au na wewe ndie usietaka muungano? maana wenzio wanadai wanatawaliwa na kukosa maendeleo wakati wana serikali yao ya mapinduzi na bajeti wanapanga wenyewe zanzibar na nyongeza wanapata kutoka serikali ya muungano. kama hujui bora unyamaze kuliko kumkosea heshima mtu alieamua kukuelimisha, tatizo washabiki wa yanga wengi mmekuja dar na mbio za mwenge!
ReplyDeleteishu ni kwa nn shaffih anachagua maswala ya kutolea ufafanuzi, tena mara nyingine anatoa ufafanuzi wa kinazi... umeelewa wewe pimbi?
DeleteShaffih katika maswala hayo jaribu kuweka unazi na ushabiki wako pembeni,ukweli ww kama mchambuzi eleza tatizo,acha wenye mamlaka ya sheria watoe maamuzi,nimekufatilia radioni na huku umeegemea upande mmoja,sijui elimu na taaluma yako,lakini sishangai kama mjumbe na mwenyekiti wa kamati ni mtangazaji wako unategemea nn?
ReplyDeleteShaffih katika maswala hayo jaribu kuweka unazi na ushabiki wako pembeni,ukweli ww kama mchambuzi eleza tatizo,acha wenye mamlaka ya sheria watoe maamuzi,nimekufatilia radioni na huku umeegemea upande mmoja,sijui elimu na taaluma yako,lakini sishangai kama mjumbe na mwenyekiti wa kamati ni mtangazaji wako unategemea nn?
ReplyDeleteLini utazungumzia usajili wa kinje,jeba na kiggi,je wao hawajasajiliwa kihuni?
ReplyDeleteKaka una jipya siku hizi, ni bora tu umeingia kwenye siasa za simba na yanga. Mwanzoni ulijifanya mchambuzi wa michezo, ukaanza hata kusema timu hii lazima itashinda sababu ya hii na hii, Mungu mkubwa timu zote ulizotabiri zingeshinda zikafungwa, ya mwisho ilikuwa fainali kati ya Chelsea na Bayern munich.
ReplyDeleteUna jipya, wewe si bora ukuchukue kadi ya simba huwe msemaji wa simba. Umetudanganya watanzania aha,aha, nimefanya interview na kocha wa Germany and mchezaji fulani, tupe ushahidi, ukifanya interviews na Ivo Mapunda unatuwekea clips, au hata wale wabongo wa Germany, lakini kocha wa timu ya taifa no clip....usitudanganye bwana.
Shaffih una hakika gani kama yondani aliongeza mkataba na simba?unakumbuka sakata la chuji?pamoja na jeshi la polisi kushirikishwa unajua ukweli,nani alisaini form za chuji simba?sijui taaluma yako,inawezekana unasomea au umesomea sheria sijui,ila nina mashaka na taaluma yako
ReplyDeleteA club intending to conclude a contract with a professional
ReplyDeletemust inform the player’s current club in writing before entering into
negotiations with him. A professional shall only be free to conclude
a contract with another club if his contract with his present club
has expired or is due to expire within six months. Any breach of this
provision shall be subject to appropriate sanctions....kama mchezaji yupo free hana haja ya kusubiri mpaka club itoe taarifa maana ana copy ya mkataba and he knows mkataba wake unaishia lini...acha kuwadanganya watanzania..mtu kama ni free agent anauwezo wa kuongea na timu yoyote hata bila rusa ya timu ilokuwa imemuajiri
na kwa taarifa yako yako mikataba inayorefushwa ni ile inayokuwa inaishia katikati au season haijaisha na mnarenew mpkaka mwishoni mwa msimu...
Article 6 Registration periods
ReplyDelete1. Players may only be registered during one of the two annual registration
periods fi xed by the relevant association. As an exception to this
rule, a professional whose contract has expired prior to the end of a
registration period may be registered outside that registration period.
Associations are authorised to register such professionals provided
due consideration is given to the sporting integrity of the relevant.....
kila mtu anazisoma hizi kanuni shaffii usijidai wewe ndo unaweza kutafsiri umekuwa unaendekeza unazi kuliko kuongelea mpira...wewe umeambiwa kabisa mcheza akiwa amebakiza miezi sita kwenye mkataba wake he can start negotiation with another team period. hizo zingine ni mbwembwe unazotaka zikufurahishe..kama anamkataba na simba hiyo ni ishu nyingine na huo mkataba unaishia lini?
Brather kiukweli mambo ya simba na yanga yatakuvunjia heshima.Mbona swala la simba kumsajili kinyemela mchezaji kinda wa azam hulitafutii sheria,au lenyewe halimo kwenye kanuni za Fifa wala Tff? Pia unakumbuka usajili wa chuji kutoka simba kwenda Yanga ulikuaje? Kaka,huwezi ukafanya mtihani halafu usiukusanye,simba wanasema walimpa mkatabampya mwezi 12,imekuaje hawaja upeleka Tff wakati wa dilisha dogo?
ReplyDeleteYANGA KINAWAUMA SANA KUAMBIWA UKWELI,, LAKINI KUMBUKENI MLIVYO MCHEZESHA MCHEZAJI WENU ALIYEPEWA KADI NYEKUNDU KWA KIBURI CHENU CHA KUIJUA SHERIA HALAFU HAMUIFUATI SASA HAO MNAOWAONA NI WAZURI LEO NAO WAMEWATUMBUKIZA SHIMONI,,,! MNALETA MCHEZO NA MZEE WA MARUFAA AKA RAGE, INAKULA KWENU TENA
ReplyDeleteMdau upo sahihi kabisa,inawezekana kwa unazi au kutokujua shaffih amesahau kuwa mchezaji ana ruhusa ya kuanzungumza na timu nyingine kama mkataba wake umebakiza miezi 6,hii haihitaji ruhusa ya FA,wala haihitaji timu kwenda FA kusema huyu kabakiza miezi 6,pili mchezaji anaweza kuondoka kama free agent baada ya mkataba wake kwisha hii haina maana FA ndio wanaotangaza mchezaji aliyemaliza mkataba,shaffih au ww mdau tusaidieni kujua kama simba wasingepeleka FA kusema mkataba wa kelvin umekwisha ina maana kelvin angeendelea kuwa mchezaji wa maisha wa simba?je mchezaji hana haki ya kujua kama mkataba wake umekwisha hadi timu yake iseme?
DeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteas tymz göes 2tajua....kuliko kupigana vjembe 2each other!?
ReplyDeletemashabiki wa yanga badilikeni, yaani mchambuzi mzuri anatakiwa aseme yes kwa maswala yanayoihusu yanga hata kama no? hata kama ni timu ya serikali kama mnavyodai basi sio kihivyo. mlitaka aseme nini kuhusu simba? alishasema simba na yanga wote wababaishaji, alishasema simba hawapo makini katika usajili, alishasema ubovu katika mfumo wa uongozi simba pale kaburu alipomsajili abdalah juma bila kocha wala kamati ya ufundi kujua, unazi upo wapi hapo? kwanini watu wazima na akili zenu mnapenda kujitoa fahamu? au mnataka niamini ule msemo usemao kwamba akili za yanga arobaini sawasawa na mbuzi mmoja? umbumbumbu wenu utaendelea kuwagharimu maisha yote maana aliewaroga alishakufa. wengine hata sijui mmetokea wapi maana sijawahi kuona watu kucomment namna hii, hii yote kwa sababu tu ya kelvin yondan lakini ingekua mambo ya kiufundi msingeonekana hapa. ila siwashangai sana maana mlishawahi kuandamana kwenda kumuomba gulamali arudi yanga, na mlishaenda air port alfajiri kumpokea manji na kumbembeleza arudi yanga lakini mpaka leo timu bado ina madeni. maisha yenu nyie siku zote ni ya kutaka kuonewa huruma.
ReplyDeleteAache unazi,endelea na kazi uliyopewa na Rage ya kuwasaidia usajiri,hongera shafiih kwa kufanikisha usajiri wa SALUM KINJE.Wadau shaffih academically ame base kwenye computing,hivyo hana maadili ya jounalism,kajifunze maadili hayo pale TMJ naamini uta-improve na utajigundua ulikua ukifanya madudu.Wanaoruhusiwa kurumbana juu ya hili ni walengwa wenyewe na mwisho hili litaamuliwa na TFF/FIFA,Shafiih unafikia kuwaita yanga wahuni? haya maadili umejifunzia wapi! Mdogo wangu naomba nikupe assigment,hebu watafute ma-riporter wa sports ambao waliokua na unazi na timu fulani na kuonesha waziwazi unazi wao kwa timu hizo mwisho wao ulikuaje?
ReplyDeleteHuo usajili kiukweli kabisa lazma una namna,mnataka kuniambia kudanganya mda wa ku sign mkataba,jina+umri wa mchezaji hzo kasoro hazionekani,YANGA wanasema wamemsainisha zamani,lakini copy inayo onekana ni ya mwezi huu,mkataba wa Simba alizaliwa 84,Yanga 94,hapo napo mtasema unazi,Yanga kama kweli wanamuhtaji wapeleke fungu 2 na amini ata achiwa kujiunga nao
ReplyDeletehakuna neno zaidi ya uhuni ndo mana Tenga ameiandikia Simba kuitaka itulie kwa sababu TFF itafuatilia kwamba alitokaje kwenye kambi ya timu ya taifa. Namuamini Rage kwamba angalau yanga watalipa pesa ya kuvunja mkataba na kujifunza ustaarabu wa soka.Simba itabaki kuwa simba, likitoka jembe linaingia jembe,masatu,pawasa,costa,owino, yet simba bingwa! Simba haijawi kukosa viungo bora na macentre back jikumbushe utakubali!
ReplyDeleteShaffih umekuwa mwepesi sana kuona kibanzi jichoni kwa mwenzio na kutoona kabisa boriti jichoni mwako.1.sijui kima adili inakuweje hapa ww kama mkuu wa idara mmoja wa wafanyakazi wako wa front page ni mjumbe na mwenyekiti wa kamati wa timu moja kwa mfano,leo Nape aajiliwe ktk kipindi cha siasa radio clouds kama mtangazaji hata kama anaitendea haki CDM bado hatoaminika.2.ww bila kificho umekuwa mshahuri na umetumika sana kusajili wachezaji wa simba kama owino,kinje tena bila kifiicho,unategemea yanga watakuwa na imani na wewe?jisafisheni ili clouds iendelee kupendwa,ushauri mtangazaji abaki kuwa mtangaziji,mwanasheria abaki kuwa mwanasheria,mtabiri abaki kuwa mtabiri,mchambuzi abaki kuwa mchambuzi.big up eddo kumwembe,wafundishe wenzio kaka
ReplyDeleteKaka tutaendelea kukupa heshima kwa kila jambo ambalo mwnye akili timamu hawez kupinga kiukweli yanga wamefanya mistake but mashabki wa yanga ni malimbukeni na ni washamba ambao kwnye dunia ya mpira hawatakiwi kuwepo kwa kua ni wagumu kuelewa na hata ukiwaelewesha wenyewe wanakwambia yanga mbele daima nyuma mwiko hawa hawa swala la canavaro si walisema wao wana haki ya kumtumia bt sheria ipo tutaona nani ana haki ktk hili we wait
ReplyDeleteTATIZO WATU MNASHINDWA KUMUELEWA SHAFFIH,MNAMTUKANA BUREE,KWENYE HEADING KAWEKA HALAMA YA KUULIZA,NYIE BAADA YA KUSOMA NA KUCHANGIA MADA MNAISHIA KUKURUPUKA TU NA USHABIKI WENU MAANDAZI,Mfano anayemsifia EDDO KUMWEMBE ktk hili ni mnafiki tu na hajui kinachoendelea katika dunia ya michezo,huyo Eddo kumwembe hujui pia kama ni msemaji wa COASTAL UNION ? acheni chuki zenu zisizokua na mantiki,Tatizo Dauda anazungumza ukweli mno ndio maana mnaishia kumtukana...wewe kama una hoja njoo hapa weka hoja yako, siyo kukalia majungu tu,
ReplyDeleteMkuu tuache uvivu wa kusoma,umeishia kusoma heading tu ukasema kauliza,soma hadi mwisho utaona katoa conclusion kabisa,tena kwa unazi anatudanganya kama vile sheria hatuzijui,unajua maana ya free agent?je unajua kama mchezaji amebakiza miezi 6 anaruhusiwa kuzungumza na timu nyingiine,swali kama simba wakinyamaza kimya baada ya mkataba wake kwisha mchezaji ataendelea kuwa mchezaji wa simba kwa sababu FA hawaambiwa?je ipo wapi haki ya mchezaji ktk mkataba?
DeleteSASA BORA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA LABDA VICHWA MAJI WA YANGA MTAELEWA NA KUACHA KUMSAKAMA SHAFFIH DAUDA MAANA NIMEANDIKA MARA MBLILI KWAMBA DAUDA HANA MAKOSA ALICHOFANYA NI KUTAFSIRI KANUNI KAMA ILIVYO LAKINI HAMTAKI, NIKAANDIKA PIA HANA UNAZI SABABU AMESHAANDIKA MAMBO MENGI KUHUSU UOZO UNAOFANYIKA SIMBA PIA HAMTAKI, JEE MNATAKA MUAMBIWE KITU GANI? AMA HAKIKA WASHABIKI WA YANGA HAPO MLIPOFIKIA HATA MKISHUSHIWA WAHAI KUTOKA MBINGUNI BADO MTABISHA, MAANA KUPINGANA NA UKWELI KWENU NI SEHEMU YA MAISHA. NAJUA BADO KUAN WASHABIKI WA YANGA AMBAO MPAKA LEO BADO WANAAMINI RAIS BADO NI NYERERE. JAMANI MNATIA AIBU HEBU BADILIKENI ACHANENI NA HABARI SHEIKH KASEMA BALI TUMIENI AKILI ZENU KUCHANGANUA MAMBO, HIVI KATI YA SENDEU NA HUYO MAGARI NANI NI MTU WA MPIRA? LEO HII HATA TUKIWEKWA MEZA MOJA MIMI NA WAO TUZUNGUMZIE SOKA HAKI YA MUNGU WATAKIMBIA PAMOJA KWAMBA MIMI NI MTU MWEPESI TU ILA MPIRA NAUJUA WAO LEO WAMEFIKA YANGA SABABU YA UZEMBE ULIOPO KATIKA VILABU VYETU VIKUBWA UNAOSABABISHA WATU KUVIGEUZA NJIA YA MKATO KUPATIA UMAARUFU, LAKINI INGEKUA ZAMANI TIMU ZIKO CHINI YA WENYEWE WATOTO WA MJINI BASI LEO HII HUYO SENDEU NA MAGARI WOTE WANGEKUA KIJIJINI KWAO NCHONGEE KIJITI NTOE FUNZA AU KIDUNDA NDIMU WANALIMA NA WALA KUSINGEKUA NA KELELE HIZI HAPA MJINI. WENZENU WANARITHI MALI NYIE MNARITHI UPUMBAVU WA VIONGOZI WENU. SHWAINI WAKUBWA NYIE!
ReplyDeletekaka hapo umekosea wanachozungumza wadau sio ushabiki lah. ni insi gani shffh alivyotoa tafsiri ya kanuni na akatoa hukumu moja kwa moja. Na kwa mchambuzi wa mpira si kazi yake kutoa maamuzi, yeye anachotkiwa ni kutoa uchambuzi wake na maoni yake na si maamuzi. Mambo mengine awaachie mashabiki ndio waamue nini cha kusema. Dhairi anaonekana ameegemea upande mmoja au kwasababu mfanyakazi mwezie ni mmoja wa viongozi SIMBA na anambiwa aseme nini.
ReplyDelete"KWA HIYO MATUSI SIO ISHU ISHU NI KUSEMA KILE AMBACHO UNATAKIWA KUSEMA NA KUTUACHIA SISI MASHABIKI TUTOE MAWAZO YETU" *kweli usisadi hautaisha nchi hii kwa staili hiii*
sasa hivi redio inayo tamba kwa habari za michezo zilizo aminika ni CAPITAL REDIO TU. HII REDIO YA SHAFFII ILIKUWA ZAMANI SANA SASA IMESHAPIGWA BAO NA CAPITAL. WATABAKI KUANDIKA MADUDU TU. MAANA VIJIDPLOM VYAO NA VIJI FIRST DEGREE VINAWACHANGANYA. RUDI TENA KAKA UKASOME USIFIKIRI KINAZAWADI MACHIBIA NA ABDALAH MAJURA WAMEKWENDA BBC KWA NJIA ZA PANYA. WANAJUA MAADILI YA UANDISHI WA HABARI. MBUMBUMBU WEWE.
ReplyDeleteHUNA JIPYA WEWE, WOTE NDIO WALEWALE WANAOFIKIRIA KWA MIGUU BAADA YA KICHWA. SASA YEYE AMEAMUA KITU GANI? AU AMESEMA YONDAN ABAKI SIMBA? NA UNAONGEA BILA AIBU ETI YEYE ACHAMBUE KISHA MASHABIKI MUACHWE MTOE MAAMUZI, SASA JINSI UNAVYOONEKANA WEWE UNAWEZA UKASEMA KWELI KAMA JAMBO LINA MADHARA NA YANGA? MNANISIKITISHA SANA MIGONGO WAZI, HIVI NAFIKIRIA KUANZISHA DARASA LA JIONI KUJARIBU KUWAWEKA KATIKA NJIA ILIYONYOOKA LA SIVYO MNAPOELEKEA NI KUBAYA.
ReplyDeleteMimi nachojua toka zamani Shaffii ni mshabiki wa YANGA sasa inakuwaje anawekwa upande wa Simba?
ReplyDeleteMimi mpaka sasa sijaona kosa la Shaffii kwani ameanza kwa kuuliza swali kuwa YANGA WAMEFANYA UHUNI KUNSAJIRI KELVIN YONDAN? Pili akatoa ufafanuzi wa kanuni sasa je kosa lake ni nini mpaka aonekane yuko kinyume?
ReplyDeleteShaffii endelea kutupa vitu bhana hao jamaa wanapenda lika siku uwe unawapa taarifa nzuri kwao kama ile EXCLUSIVE: Maximo kutua Dar J4 kumalizana na Yanga walikupongeza mpaka basi saahizi wamekugeuka tana hujui vitu ahahahaha wanafurahisha sana mashabiki hasa wa kibongo.
ReplyDeleteHuwezi kuona tatizo la Shafii kutokana na Ama uvivu wa kufikiri au nawe uko bias kama yeye.Tatizo la Shafii hazingatii uweledi wa kazi yake badala yake amekuwa akionesha dhahiri unazi wake kwa simba kama alivyo maulid Kitenge kwa Yanga. Waandishi zingatieni Professionalism sio kuonesha unazi wenu MNATUBOAAA
DeleteTujifunze kwa wenzetu jinsi wanavyosajili. Mie nimekuwafuatilia sana usajili wa wenzetu, Unzuri Shafii huwa anatueleza kupitia hii blog au Cloudsfm. Pamoja na mambo mengine wachezaji huwa makini kuchagua club ya kuhamia. Na mara nyingi huangalia club inayoshiliki Uefa. Kwa nini huangalia hilo? Mfano Kipindi CR7 anahama man utd hakwenda man city iwapo walikuwa na pesa bali alienda timu inayoshiriki uefa. Modric anataka kuhamia man utd sababu club yake haitashiriki uefa.
ReplyDeleteHapa kwetu ni pesa na wakati mwingine hutufanya tusifuate sheria za soka sababu ya tamaa ya pesa. Kama Yondan atasajiliwa yanga basi ajue mwakan hatashiriki mashindano ya club kimataifa.
Simba wamwache Yondan akacheze sehemu roho inapenda watapata mwingine,mbona Samatta aliondoka mkapata Okwi, nasikia naye mnataka kumuuza. George Masatu aliondoka mkapata Pawasa. Mtapata mwingine ila msimwache Nyoso kwa sababu za kihuni. MGANYE, S
TAPELI WA MAWAZO WEWE. HUYO JUMA NYOSO ALIESHIRIKI SHIRIKISHO AMEPATA NINI? AU HUYO OSCAR JOSHUA ALIECHEZA NA ZAMALEKI CLUB BINGWA AMEPATA NINI? UNAFIKIRI MSHAHARA WA ROON NI SAWA NA ETOO ANACHEZEA TIMU ISIYOJULIKANA. MPIRA PESA KAKA. NA UKUMBUKE KUNA KUFULIA KISOKA. SASA KAMA YONDANI HATACHUKUA UAMUZI SASA WA KUSAKA MSHIKO UNAFIKIRI ATAZIPATA LINI. KWA MAWAZO YAKO SITASHANGAA KUWALAUMU ETOO NA ANELKA. ACHA UNAZI WA KIJINGA. MPIRA WA BONGO NI MIAKA 5 TU MWACHENI YONDA ATUFE MSHIKO HUU NDO WAKATI WAKE SASA.
ReplyDeletewote mnaongea kishabiki kwenye swala linalogusa simba na yanga lazima hali iwe hivi lakini kila mmoja ana makosa kwenye suala la Yondani, simba wana makosa yao, yanga wana makosa yao, Kelvini ana kosa lake na Shafi pia ana makosa yake
ReplyDelete