Search This Blog

Sunday, June 24, 2012

WAZO LA EDO KUMWEMBE!

Congrats Yanga kwa kumnasa Yondani. lakini ebu tutumie akili ya kuzaliwa hapa. Itazame vizuri sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Kaunda. Hapana shaka ni Duni. Kev amesajiliwa zaidi ya sh milioni 30. Ni kama ilivyo kwa mastaa wengine wapya waliotua Yanga. Kwa nini isitengwe sh milioni 2 tu ya kuitengeneza sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Kaunda, plus pump za kumwagilia uwanja full time na ikiwezekana Kisima. hivi vyote vinagharimu pesa ndogo sana kuliko mamilion ya kuwanunua akina Kev. inakera kuona kocha anakuja na kuipeleka Yanga mazoezini kwingineko kwa gharama kubwa, wakati milioni 5 inamaliza tatizo la pitch la Kaunda. mbona players wanamwagiwa pesa nyingi tu bila ya shida? WAZO TU

10 comments:

  1. Pamoja na kwamba kuna ukweli katika wazo lake lkn haimuhusu,labda atuambie Coastal ina uwanja gani wa kufanyia mazoezi? mbona na wenyewe wametoa fungu kubwa kumsajili Nsa Job na wengineo,je hayo mafungu waliyotoa yasingeweza kuitengenezea uwanja wa uhakika wa kwao Coastal binafsi Coastal au ndo yale mambo ya Nyani haoni....

    ReplyDelete
  2. Dah ukwel mtupu dauda

    ReplyDelete
  3. Pichi ya kuchezea mpira haitengenezwi kwa mil 2 kaka,ndio maana manji akagombea ili ku make difference, so just wait and u wil see

    ReplyDelete
  4. kaka umesema k2 cha amana sana na mwenye macho na aone na mwenye mackio asikie

    ReplyDelete
  5. hivi wachezaji wa wazuri wapo simba na yanga tu? au ni kwaajili ya ufahari? afu usajili unafanywa na kocha au kamati? angalia kama yanga wamesajili viungo wengi wakati tatizo ni washambuliaji, kiungo kama dumayo,nizar,kijiko,niyonzima, chuji, nurdin bakari. wakati wanamatatizo ya ushambuliaji.

    ReplyDelete
  6. Wow! Kwa ujumla anayetoa mawazo (EDO KUMWEMBE)ana mtizamo mzuri ila kwa kiasi fulani naye pia ni sehemu ya uoza wa vilabu vyetu. Ni msemaji wa Coastal Union, sioni ni kwa vipi anapata authority ya kulaumu mambo ya Yanga wakati hata kwake mambo ndiyo hayohayo.
    Tanzania ya leo michezo yote si soka tu, mambo yako mrama. Itachukua miongo kadhaa tupate mafanikio ya mchezo wowote ule. Kwa sasa tumebakia kuandaa michezo ya CECAFA tu kila mwaka, tunapanga matokeo, timu zetu zinabebwa alafu tunashinda kimizengwe. Ushindi wa jasho hatuuwezi kamwe.
    Angalia hata Olimpiki sijui tunapeleka bondia mmoja tu, tena aliyefuzu kwa bahati nasibu. Kimsingi, michezo inaendeshwa na watu wanaotaka fedha kibinafsi, tumesahau michezo kama fani ya kisayansi. Mpaka tutakapokuwa na kizazi cha watu wenye dhamira ya kweli, wasioweka maslahi na umimi mbele ndio tutaamka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shekhe Innocent hapa Edo ameongea kama mwandishi wa habari na sio kama msemaji wa coastal union........

      Delete
  7. Tatizo la vilabu vyetu hivi si viongozi tu ila hata mashabiki, ukizungumza kitu against wao utaona jinsi mashabiki watakavyokushambulia na hao viongozi wanatumia mwanya huo huo wa umbumbumbu wa mashabiki wao kundeleza siasa ndani ya hivi vilabu badala ya mpira.
    Suala la simba na yanga kukosa hata viwanja vya vya kueleweka vya mazoezi linakera sana,hakuna kiongozi wa mpira kwenye hivi vilabu watu wanatafuta sifa tu.
    Anyway labda this time around Manji atafanya mambo makubwa kwani uwezo anao wa kuibadili yanga kwani nasikia amesema anaaza na uwanja.
    Ila ni aibu kubwa kwa mashabiki wa simba na yanga kwa timu zao kukosa viwanja na wao wako kimya wanashindwa kuwauliza viongozi wao.
    Mdau
    Mike

    ReplyDelete
  8. WATANZANIA TULIO WENGI HATUNA MAWAZO YA KESHO TUNAPENDA KUANGALIA LEO TU. EDO ULICHOKISEMA NI KWELI. TATIZO LETU SISI WATANZANIA (PAMOJA NA VIONGOZI WETU WOTE TU BILA KUJALI WA MICHEZO AU WA WAPI!!) TUNAPENDA VYA URAHISI SANA PAMOJA NA SHORT TERM PLAN(AMA SHORT CUT). PIGA MAHESABU YA GHARAMA YANGA ILIZOKUWA INATOA KUFANYA MAZOEZI TANGANYIKA INTERNATIONAL SCHOOL, LOYOLA HIGH SCHOOL. UKIJUMLISHA UTAKUTA ZINGETOSHA KUUKARABATI UWANJA WA KAUNDA. WATANZANIA TUMEKUWA VIPOFU. NDIO MAANA TUNAKIMBILIA KUSAJILI WACHEZAJI KWA HELA NYINGI ALAFU AKIJA KLABU ANAISHIA BENCHI AMA ANACHEZA CHINI YA KIWANGO.

    NI MATUMAINI YANGU MANJI KUSHIRIKIANA NA TIMU YAKE YA WATAALAMU WA UONGOZI PALE QUALITY GROUP WATAWEKA MISINGI IMARA NIKIMAANISHA KUKARABATI MIUNDO MBINU YA SOKA (UWANJA WA KAUNDA, PAMOJA NA HOSTELI YAKE, VIFAA VYA GYM).
    ALAF WAWEKE LONG TERM STRATEGIC PLAN YA KUINDESHA YANGA KIBIASHARA ILI IONDOKANE NA UTEGEMEZI.

    WAANZISHA AMA KURUDISHA YANGA KIDS NA IKIBIDI ACADEMY NA MAMBO MENGINE YA MAENDELEO.

    EDO KUMWEMBE WACHA HAWA WABABAISHAJI WAKUPINGE LAKINI KWA VISION ULIYO NAYO NAIONA COASTAL UNION YA MIAKA MIWILI IJAYO. IWAPO TU WANATANGA NA VIONGOZI WENZAKO WATAKUWA NA VISION ULIYO NAYO. NA KAMA WAO HAWATAGEUKA KUWA WABABAISHAJI. UKWELI UNAUMA NDO MAANA WANAKUPINGA.

    ReplyDelete
  9. Kuna mtu mmoja alisema kama hawa viongozi wasasa wa mpira wangepewa kujenga ofisi ndogo ya vyumba vinne wangeweza kwa ajili ya klabu wangeweza!!!!!!!!!?????

    vilabu hivi miaka kazaa imepita tangu vianzishwe lakini vinashindwa kuwa na viwanja vya mazoezi, ongera Azam fc,

    ZIWI

    ReplyDelete