VIKOSI VITAKAVYOANZA
RUSSIA: 1: Akinfeev 2: Anyukov 3: Zhirkov 4: Berezoutski 5: Ignashevitch 6: Denisov 7:Zyryanov 8: Dzagoev 9: Kerzhakov 10 Arshavin 11: Shirokov
CZECH REPUBLIC - 1: Cech 2: Selassie 3: Kadiec 4:Sivok 5: Hubnik 6: Piasil 7: Petrzela 8: Hubschman 9: Baros 10: Rosicky 11: Rezek
MAMBO MUHIMU KUHUSU TIMU
- Mchezaji wa Sporting Lisbon Marat Izmailov ndio mchezaji pekee aliyekuwa akihofiwa juu ya ufiti wake kuelekea kwenye michuano hii lakini sasa amerudi kwenye hali yake ya kawaida kwenye mazoezi pamoja na Alan Dzagoev, nchini ya nahodha Arshavin.
- Safu pekee ambayo itakuwa na upinzani ni kwenye goli, Akinfeev atakuwa akipambana na Malafeev.
- Czech watakuwa na nafuu kwamba mchezeshaji wao Tomas Rosicky amepona kutoka kwenye majeruhi na huku akiwekwa kwenye kikosi kitakachoshiriki kwenye michuano hii na anaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji wa kati akama ambavyo katika nusu ya msimu alipokuwa Arsenal.
- Striker Milan Baros, ambaye japokuwa ana tatizo la misuli na alifanyiwa vipimo juzi jumatano ili kupata uhakika wa ufiti wake, na kama hatokuwa fiti basi Necid na Pekhart watakuwa wanaisubiri nafasi yake.
- Wachezaji wengine muhimu watawahusisha wachezaji wazoefu kama vile Peter Cech, Kadlec na Plasil.
TAKWIMU
Russia hawajaruhusu wavu wao kuguswa mara sita kwenye mechi 7 za Euro zilizopita.Czech Republic wameshinda mechi zao 3 za mwisho kwenye Euro.
Russia hawajafungwa katika mechi zao za mwisho za Euro.
UTABIRI
Russia wataenda kwenye mechi za group ambalo linatajwa kama dhaifu kabisa kwenye michuano kama timu inayopewa nafasi ya zaidi kwenye kundi hilo, ingawa kila mchezo wa kundi hili utakuwa mgumu.Timu mbili zote zina uzoefu kwenye hatua hii, na makocha wote watakuwa wakiwategemea viungo wao wachezeshaji kusogeza mashambulizi mbele kwenye mechi hii.
UTABIRI: RUSSIA 2-1 CZECH REPUBLIC
shafii hivi kwa mpira waliounesha ugiliki na poland wana nafac yakusonga mbele hawa ? mana tim kama ujerumani,spain uholanz c wanwpiga hata 5 wale.
ReplyDelete