Mauzauza kwenye soka la Bongo yameendelea kujidhihirisha leo.
Wakati klabu ya Simba ikiwa imejihakikishia kukamilisha usajili wa kinda la Azam under 20, Ibrahimu Jeba ambaye leo hii asubuhi alionekana kwenye mazoezi ya gym ya Simba - maeneo ya Chang'ombe. Uongozi wa klabu ya Azam FC umesema Simba inajidanganya kuhusu kumsajili mchezaji huyo ambaye Azam walimpeleka Villa Squad kwa mkopo kwa kujifua zaidi msimu uliopita.
Akizungumza na www.shaffihdauda.com kutoka nchini Marekani meneja wa klabu ya Azam FC, Patrick Kahemele amesema mabingwa wa Tanzania bara wanafanya uhuni kwenye uhamisho wa mchezaji huyo ambaye bado ana mkataba na klabu hiyo inayomilikiwa na mfanyabiashara Salim Bakheresa. "Simba wanafanya uhuni katika hili kama ilivyo kawaida yao, Jeba ni mchezaji wetu halali na bado ana mkataba na Azam. Kumbukumbu sahihi nilizonazo ni kwamba Ibrahimu Jeba alisaini mkataba wa kuichezea Azam kwa miaka miwili mwezi Desemba 2011 na akachukua kiasi cha fedha kama ada ya usajili - kabla ya kuelekezwa kwamba akacheze Villa Squad kwa mkopo ili apate nafasi ya kujifua then msimu huu arudi Azam FC. Simba wakaenda wakamrubuni asicheze Villa, na Jeba bado mdogo hivyo ikawa rahisi kumrubuni, na Azam hatukutaka kufanya nao malumbano kwa sababu suala hilo tayari tuna mkataba ambao umesajiliwa kabisa na TFF, ambao walishatuambia haki zetu za msingi zitalindwa."
Kahemele alipoulizwa ikiwa Simba wanataka kulimaliza hilo suala itabidi walipe kiasi gani alijibu, "Kiukweli sie tulishatangaza mapema kwamba hakuna mchezaji yoyote ambaye ameachwa wala yupo sokoni kwa msimu ujao. Hivyo kama Simba wanamtaka Ibrahimu Jeba kihalali basi atawagharimu sana kwa kuwa sisi tunamuona Jeba akiwa na thamani ya Shilingi millioni 50 na uwachanganye wachezaji wawili wa Simba Jonas Mkude na Shomari Kapombe, then hapo tunaweza kuwafikiria kuwaachia Jeba vinginevyo haitowezekana Jeba kuichezea klabu yao."
HIKI NDIO KIKOSI RASMI CHA AZAM KWA AJILI YA MSIMU UJAO.
Kikosi Kamili cha Azam FC msimu ujao ni kama ifuatavyo Magolikipa ni Mwadini Ally, Deo Munishi "Dida" Aishi Salum na Jackson Wandwi
Mabeki wa Pembeni kulia ni Ibrahim Shikanda na Erasto Nyoni na kushoto ni Waziri Salum na Samih Haji Nuhu
Babeki wa kati ni Luckson Kakolaki, Said Moradi, Joseph Owino na Aggrey Morris
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar, Abdi Kassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam, Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, na Ibrahim Joel Mwaipopo
Washambuliaji wa pembeni ni Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha, na George Odhiambo "Blackberry" Washambuliaji wa kati ni Gaudence Mwaikimba na mchezaji bora wa Azam FC John Raphael Bocco "Adebayor"
Inawezekana simba kweli hawajakamilisha mambo sawa but sayin kuwa jeba ni mkude plus kapombe and milion 50 iyo ni dharau kubwaaaa sana.am sure uyu jamaa ameropoka kwa hasira...amekosea na amewakosea aliowataja.si sawa kabisa!
ReplyDeleteMkufunzjr.
KAPOMBE + JONAS + 50 MILL = JEBA, thats crazy statement na bado hakuwa na namba kwenye kikosi cha kwanza cha Azam, huyo jamaa anaota ndoto za mchana.Ila hao simba nao kama ni kweli wanamtaka wafuate taratibu muda wa kupitia mlango wa nyuma umepitwa na wakati
ReplyDeleteMdau
Mike
Jeba under-18, amesaini vipi mkataba? Huo mkataba ni null & void!.......
ReplyDeleteHiyo sijaipenda haijakaaa vzuri kwani hao Azam wanamtaka huyo kijana baada ya kuona simba inamtaka. Nawshauri viongozi wa simba wawaachie huyo kijana Simba bado tuna vipaji lukuki kutoka katika timu yetu ya vijana......
ReplyDeleteAZAMA TUNWAOMBA MRUHUSUNI JEBA AJE SIMBA KUCHEZA SOKA,AKIKUTANA NA WENZAKE AKINA KAPOMBE,SINGANO,NA WENGINEO TUTAJENGA TAIFA KATIKA WIGO HUU WA SOKA.KUMBUKENI MLIVYOMCHUKUA RIDONDO NA AZIZ,TULIWACHIA.HIMA JAMANI TUNAWAOMBA SANA TENA SANA.
ReplyDelete