Search This Blog

Tuesday, May 15, 2012

TATHMINI YA MDAU Revo alex JUU YA MCHEZO WA AL AHLY SHANDY NA SIMBA.


Na Revo alex

Hii ni kwa mujibu wa mtazamo wangu jamani nikiwa kama Mtanzania niliyeuangalia mchezo ule kwa umakini sana huku nikiwa na matumaini makubwa na Wawakilishi wetu wa pekee waliokuwa wamesalia kwenye mashindano ya kimatafaifa.
(Score zote ni out of 10)
  1. Juma Kaseja

Bila shaka wakiambiwa huyu ndo Tanzania One watasema bado kama nchi hatujajaliwa mtu mwenye kipaji kizuri katika nafasi hiyo kwa kipindi hiki tulicho nacho licha ya kuokoa michomo kama 2,3 iliyoonekana kuwa na madhara makubwa kwa team yake ndani ya dk 90 hakuwa na la ziada, na hata beki yake ilivyopoteza dira kipindi cha 2 hakuonyesha jitihada zozote binafsi za kuzuia madhara kwa team yake,mipira iliyogonga besela na ile iliyokuwa inatoka nje baada ya kumpita inadhihirisha hili,hata ujasiri wake wa kudaka michomo ya penalt tunaoufahamu jana haukuonekana,upande wa kulia alikuwa haendi kabisa na Jamaa walivyogundua hilo wakawa wanampelekea hukohuko, na ndo aliyepiga penalt ya 9 ambayo ilidakwa na kipa wa Shandy na kuitoa team mashindanoni.

Anapata 5
2.Shomari Kapombe

Dogo huyu aliyeko kwenye form alicheza vizuri hasa katika kipindi cha kwanza, baada ya Ahly Shandy kuja na Plan B kipindi cha 2 alizidiwa ukichukulia namba 7 anzia Uhuru na hata alipoingia Machaku walikuwa hawashuki kumsaidia kiasi kwamba mipira mingi iliyoonekana kuwa na madhara makubwa kwa Simba ilikuwa ikipitia upande wake kitendo kinachoweza kuwa kimetia doa deal yake ya kwenda TP Mazembe kama tetesi zilivyokuwa zimezagaa.
Anapata 6
3.Amir Maftah

Alicheza kama beki 3,aliendelea kuwa ni yuleyule tuliyemzoea hakuwa na jipya sana na hakuonyesha kupanda kusaidia mashambulizi kama ambavyo amekuwa akifanya kwenye baadhi ya mechi za hapa nyumbani labda alicheza kwa kufata maelekezo ya kocha wake wakihofiwa kufungwa.
Anapata 5

4.Victor Costa

Alionekana kucheza kwa kujiamini sana kipindi cha kwanza wakati Simba walivyofanikiwa kuwabana Shandy na kupunguza mashambulizi yao,kibao kilivyogeuka kama ilivyokuwa kwa beki line nzima alichemsha,na ni yeye aliyezembea ku’clear pass iliyomfikia mfungaji wa goal la 3.
Anapata 4
5.Kelvin Yondani

Alikuwa ni yuleyule tunayemfahamu,alicheza vizuri lkn na makosa mawili matatu kama ilivyo kawaida yake.
Anapata 5
6.Mwinyi Kazimoto

Alianza kucheza kama namba 6,baada ya Simba kufungwa magoli ya fasterX2 kocha alimbadilisha namba na Mafisango,pamoja na kujitahidi kufurukuta haikusaidia.
Anapata 5

7.Uhuru Seleman:

Moja ya shambulizi makini la Simba liliishia mguuni mwake,shuti alilopiga kama si umahiri wa kipa wa Ahly Shandy lingeweza kuwapa Simba goli,hata hivyo pass nyingi alizokuwa akipiga zilikuwa zikinaswa na wachezaji wa Ahly Shandy na haikuwa ajabu kocha kumtoa.

Anapata 4


8.Patrick Mafisango:

Alianza kucheza kama kiungo mshambuliaji(labda wakiamini atawabeba kama ambavyo amekuwa akiwabeba kwenye baadhi ya michezo ya ligi iliyomalizika hivi karibuni) baada ya Simba kufungwa goli za 2 za fasterX2 walibadilishana na Kazimoto hata hivyo haikusaidia,still bado Jamaa walikuwa wanawapumulia kila wakati.
Kama ilivyokuwa katika mechi ya Dar, penalt yake iliyookolewa na kipa wa Shandy ndo iliyoendelea kuwaweka Waarabu wale mchezoni.

Anapata 4
9.Felix Mumba Sunzu

Alicheza nyuma ya Okwi,alijitahidi kufurukuta,alikuwa anaonekana ni hatari kuliko washambuliaji wengine waliopangwa katika mechi ile lkn kama inavyokuwaga kwa Mwape wa Yanga hakuwa na jipya.
Anapata 6
10.Emanuel Okwi:

Haikuwa rahisi kuamini kwamba Okwi yule aliyekuwa gumzo katika magazeti yote ya Sudan alikuwepo katika ile mechi,wa’Sudan walianza kwa kumkaba sana labda wakikumbuka jinsi alivyowaadhiri hapa Dsm lakini baada ya muda fulani waligundua alikuwa ni “kapi” wakaachana naye na kuhamishia concentration zao kwa Sunzu aliyeonekana kidogo ni hatari,hakuonyesha kuwa yeye ni professional footballer kwa kubishana na refa bila sababu za msingi kiasi kwamba refa angekuwa ni Israel Nkongo wa Azam angemlima kadi 2 za njano kisha nyekundu,hata hivyo aliambulia 1 ya njano ambayo ilikuwa ni ya kujitakia.
Kwaufupi alikuwa ni Okwi yule wa kipindi cha katikati nyuma( wa leo kucheza vizuri, kesho kuboronga) hakuwa Okwi huyu wa kipindi hiki cha hivi karibuni.
Anapata 3.
11.Haruna Moshi (wenyewe humuita Boban)

Jinsi alivyoingia safarini na Malapa niliamini akili yake haiku sawa na hivyo asingekuwa na lolote la ziada kwa manufaa ya team yake kiwanjani,na ndicho kilichotokea.
Anapata 4


Generally team kama team jana ilifia kwa Okwi,kama wewe ni mfatiliaji wa soka la bongo utakubaliana na mimi kuwa mafanikio ya Simba kwa siku za hivi karibuni kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakitengenezwa na jitihada binafsi za Okwi,kwahiyo kitendo cha Okwi kuwa "out of form" jana ndo kiliifanya Simba ya jana ionekane tofauti na ile Simba ya kwenye mechi ya kwanza Dsm.
Ushauri wangu:
Wakati wa kucheza soka kwa kutegemea mchezaji mmoja/wawili umekwisha,Simba inatakiwa kusajili kama kweli wanataka kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa (hii ya nyumbani longolongo za hapa na pale zinaweza kuendelea kuibeba),tofauti na hapo hata Yanga inaweza kujikuta inajipozea machungu hapo kwenye Kagame.

Nawasilisha!

21 comments:

  1. Kwa haraka haraka naweza kusema kuwa huyu mchambuzi ni mwana YANGA, hili halina ubishi.

    Uchambuzi wake upo one-sided, that's all.

    ReplyDelete
    Replies
    1. na ww inavyoonesha n shabiki wa SIMBA hii ndio tabu ya watanzani hawapendi kuambiwa ukweli.sisi mpira we2 bado uko chini 2sijidanganye kwa kumfunga yanga 5,kumfunga azam cjui jkt ruvu,mtibwa 2natakiwa 2jipange kama 2nataka kweli kufanikiwa eti proffesional hata kwenye timu ya taifa hayumo kago kasajiliwa kwa mbwembwe na rage maana sio na kocha,sunzu kwao zambia wanajua kuwa kishastafu hata mpira mwenyewe eti sisi 2namuona lulu 2namlipa dollar 3500 per month sasa jiulize john boko wa azam na sunzu who is the best.2navipaj vingi sana kule mchangani vinatakiwa kuendelezwa.asanten xana wadau.heri cape town

      Delete
  2. inabidi tujipange ila tusubiri azam wanaweza kuleta jipýa maana ndio timu mpya inayo ingia kwenye kulionyesha soka letu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. jamani sio kila mwendawazimu anaweza akurupuke huko ajifanye kuchambua soka,we revo hebu tutolee upuuzi wako na hizo rating zako ambazo hazina viwango wala criteria za msingi,mfano kaseja unasema eti hana kipaji we jamaa una matatizo wewe,ulitaka afanye maajabu yapi kwenye yale magoli aliofungwa,hata casilas anafungwa magoli yale sijui ulitaka kaseja afanyaje na kuhusu penati si alidaka moja we ulitaka adake 5 zote,simba wamepoteza mchezo kwa kukosekana kwa umakini na concentration kwenye kipindi cha pili,approach yao ya kipindi cha kwanza ilikua safi bt second half jamaa walibadilika na kutumia uzembe wa beki hasa wa kati Victor costa kufunga magoli hayo,wote tuliona mpira na usituchanganye na hizi rating zako za ramli,sisi sio timu inayotunzwa na wazee
      chela wa dom

      Delete
  3. Mchambuzi kwa sehemu kubwa ameonyesha unazi wake kwa yanga. Kubwa lililonishangaza ni uchambuzi wake kuhusu Boban ambao umehusisha mavazi ambayo hayahusiani na dk 90 binafsi sikubaliani na uchambuzi wake.

    ReplyDelete
  4. Kama ulivyosema ni mtazamo wako ni wa ovyo kabisaaa!....

    ReplyDelete
  5. tatzo watanzania tunalaumu ki2 kikishatokea!ushauli wa huyu bwana alishindwa nini kuutoa kabla timu haijaenda sudan,wakati anajua ungeliwasaidia?Ni upuuzi m2pu..........!Acjifanye mechi kuwa aliiangalia mwenyewe,J.Kaseja wala hakushindwa kufuata penayi za kulia,ila ni ufundi wa wapigaji.Km anakumbukumbu nzuri na ni mchambuzi na mfuatiliaji mzuri wa soka na cio mshabiki,namuuliza swali kuwa,penati aliyookoa Kaseja ilikuwa upande gani?Huwezi kumjaji m2 kuwa hajui kwa mechi moja wakati mechi nyingine alikuwa anafanya vizuri,huwezi kusema Kapombe dili la kwenda Mazembe limetiwa doa kwa mechi moja tu ya juzi,wakati mechi nyimgine anafanya vizuri.Alichikifanya huyu mchambuzi ni kuwachafulia majina wachezaji wa simba na kuonekana hamna ki2 chochote wanachojua wakati ndio mabingwa tz,halafu hajazungumzia suala la maamuzi km ni mfuatiliaji mzuri na mchamuzi wa maana.Usajili anaouongelea ni upi,wakati wachezaji wa kitanzania anawafahamu,km ni wakimataifa akawaulize TFF,juu ya usajili wa wachezaji wa kigeni!SHAFFI nakushauri acha upenzi na ushabiki,maana analyses mbovu km hizi kuzichapa ktk blog yako unajidharirisha sana kwanza hata wewe uwe unazihariri kabla ya kuziweka.We ni m2 mkubwa bwana na tunakuaminia hacha hizoo!

    ReplyDelete
  6. habari mdau!mimi pia nmefatilia mpira na mechi nimeangalia mwanzo mwisho kupitia tv sasa huyu Revo cjui REVOLA what ever!!Mpira cyo maneno wala majigambo ingekuwa hivyo UINGEREZA wangekuwa wanachukua kombe la dunia kila siku,kilichotokea katika mchezo wa simba na shandy kwanza 1.UCHOVU wachezaji walitoka kambini na kuingia kwenye mchezo ambao ulikuwa ni wa kukamiana hivyo hata mazoezi yao siyo ya kitoto mechi ya simba na yanga,ambayo kwa mtazamo wangu baada ya mchezo kuisha simba wakajua wamemaliza kazi pamoja na kufikiri shandy washawatoa,hivyo kupelekea kufanya starehe ambayo PSYCHOLOGICALLY lazima wawe wachovu.la pili 2.KUJIAMINI hili pia naweza kusema ilikuwa sehemu ya kufungwa kwao walijua mfumo wao wa kushambulia na kuzuia(DEFENSIVE ATTACK)ambao ndo walikuwa wanatumia Shandy yaani kujaribu kushambulia huku wakiwa na ukuta ila simba waliposoma ile formation ikabidi wajipange upya ambapo kpind cha pili walibadilisha jinsi ya kushambulia namwambia REVOLA hata ucheze na MUTWEVA ya Njombe kwa ule mfumo utafungwa tuu,hivyo sioni sababu ya kumlaumu Kaseja nachosema walijiamini sana na kuona hata wakifungwa haziwezi kuzidi mbili kwa jinsi ya uchezaji wao huwezi kutoa tathmini tena unatoa na marks cjui katika maisha yako kama uliwahi hata kucheza mpira,kama ulicheza basi cha ndimu enzi zilee coz hata nikwambia rusha mpira utatia aibu.la tatu 3. UZEMBE wa baadhi ya wachezaji ambao wameicost team kiukweli kwenye hili naomba nisisitize kuwa UZEMBE unatokea kote kwa wachezaji cjaribu kuwatetea SIMBA hapana naongea hali halisi MAFTAH huwa anasubiri aambiwe kama anakosea ili arekebishe makosa yake huyu namfananisha na Manuel Neira mchazaji wa chile enzi hizo akikosea ataua mtu uwanjani hadi aukamate mpira akashinde au ampe GOAL DOCTOR Sallas enzi hizoo sasa kwa uchezaji ule wa Maftah kocha hakutakiwa kumuacha acheze muda wote alolifanya Maftah juzi halitofautiani na alivyocheza kipindi cha kwanza kwenye mechi ya kiyovu ilochezwa hapa DSM hivyo usiwape lawama tuu Chollo kapigana sana,Milovan alifanya Sunzu na Boban ndio wafungaji kwa lengo la kumuacha okwi aachwwe free na kuwalisha sunzu na boban lakini sasa okwi hutumia akili yake binafsi ambayo hata hivyo haikuzaa matunda narudi kwako REVOLA Simba haitegemei mtu mmoja ingekuwa hivyo kiatu cha mfungaji bora VPL angechukua Okwi kwasababu simba ndo inaaongoza kwa magoli.la nne 4.VITUKO tujaribu kuangalia kila upande huwezi ukatoa hukumu kwa simba kufungwa3 kwasababu gani nao walishinda 3 tena kipindi cha pili hicho hicho baada ya kusomana na kutumia makosa,katika hali ya kawaida hata wewe REVOLA jirani yako mara anatupa takataka mbele ya nyumba yako,anakuchokoza na anajua sheria somtimes anaweza kukuharibu akili,hayo mambo yapo.JE tujiulize sisi watanzania tumezoea yale?au ndo alofanya kafanya Jenga tabia ya kujiuliza kwanini kafanya Mdau eeh SHAFFIH DAUDA angalia na watu wanao post wengine wanatafuta umaarufu tu atajwe Sports xtra ndo navoona,kwa sasa acha niendelee na kazi ya ujenzi wa Taifa naamini na wewe pia tupo pamoja..Mdau kila la kheri kazini kwako wasalimie JEFF,MAESTRO,LUAMBANO,ABDUL na wote idara ya michezo Clouds tv MEB,RAY,KABEZI,KATUNDA

    ReplyDelete
  7. huu uchambuzi si yakinifu hata kidogo, umejaa ushabiki

    ReplyDelete
  8. Huyu mchambuzi anaonekana ana chuki na timu nzima ya Simba.

    ReplyDelete
  9. kiukweli uchambuzi wako uko kishabiki zaid na hauna mashiko kokote nafikiri jarbu kusoma ulichoandika utaelewa namaanisha nn

    ReplyDelete
  10. pole simba next season
    www.eliudpro.blogspot.com

    ReplyDelete
  11. Huyo mchambuzi hana lolote yanga mkubwa anataka simba ionekane mdebwedo kama timu yake yanga. Wakati tumewatandika gwala. Subili kagame uone. Wako. James

    ReplyDelete
  12. shaffih fanya mambo kiueledi, umetuwekea vitu gani? naanza kukosa imani nawe kwa kupokea na kuposti vitu visivyo na msingi.au mnatufanya watoto sie wafuatiliaji wa hii blog.hatukatai mtazamo wa mtu lakini sie tunaiheshim hii blog au umeanza kuposti ukatuni.BE WISE BRO. UWE UNAFANYA MAMBO KIUELEDI NA UACHE DHARAU.

    ReplyDelete
  13. Sie hatujakataa kurolewa ila shaffih hawa wachambuz wakwenye kahawa unatoa wapi?huyu mnazi Mkubwa Wa yanga Kama unataka kuzungumza mpira zungumza mpira sio kuleta majungu na uchambuzi Wa kinazi

    ReplyDelete
  14. UHAROOOOO Mtupu.. Nahisi bado anaweweseka na zile goli 5 no wonda akam-rate okwi 3. Kununua datasiku yako haina maana upost kila uharo unaojisikia kupost.. Labda nkuulize mnaenda lini kupiga kambi nyumbani kwa Nchunga? Na ile Albadiri lini tuje kunywa chai ya tangawizi sie..

    ReplyDelete
  15. Duh! Hii inaonyesha jinsi wanayanga walivyoumia roho zao! Wanajaribu kuzituliza roho zao kwa kuandika mambo yasiyo hata na msingi. Eti huyu nampa 5, ... huyu nampa 4, ... huyu nampa 2, who the hell gave you the moral authority to judge this way?

    Huyo mtoa mada ni sawa na wale wanafunzi ambao baada ya kutambua pepa imewachungulia basi huamua kujitungia maswali yao na kuyajibu, au sawa na wale walioamua kuandika lyrics za bongo fleva kwenye exam answer sheets.

    Halafu huyu jamaa alikuwa na raha sana kwa kuamini kuwa ni yeye pekee pata nafasi ya kuangalia ile mechi, ... enzi hizo zimepita mshirikaaa - utandawazi babaaa! Eti anaamua tu kutoa point, hata ukimuuliza vigezo gani alitumia hajui! Watu wengine bwana, wakiwa na uwezo wa kununua andawea tu basi, naye anajiona ana mamlaka ya kuwa mchambuzi, aaarghh!

    ReplyDelete
  16. Naona Wanazi wa Simba wamekuja juu ile mbaya,lkn sishangai ksbb binadamu hususani watanzania huwa hatupendi kuambiwa ukweli,na kama Shaffih utaendelea ku'post ukweli unaogusa upande fulani huo upande unaoguswa unaweza siku kuja kukutukana live,watu wana hasira bwana,goli 3 ndani ya dk 16 siyo mchezo ati.
    Anyway mimi nipo neutral na naomba nitoe maoni yangu kama ifuatavyo,
    Criticism za Mashabiki wa Simba kama wanavyojibainisha kwa maoni yao hapa ni za kipuuzi na ndo zimekaa kinazi zaidi kuliko hata huu uchambuzi,embu twendeni sawa Mtu anasema aliuangalia mpira kwa makini hlf anatuambia Chollo alipigana sana,yaani hana hata habari kuwa Chollo siku ile hakucheza,haya mwingine anamtetea Kaseja kuwa he was at his best,ama kweli kupenda upofu yaani mtu hakuona kabisa zile penalt karibu 3 za upande wa kulia Kaseja alisimama tu,anaongelea penalt 1 ambayo dhahiri kabisa ilipigwa kichovu,mimi naungana na mchambuzi Kaseja siku hiyo kama hakupoteza umakini basi umahiri wake umeanza kupungua(kwanza kucheza kwa misimu 11 Ligi ya ushindani siyo kitu rahisi)Kaseja ninayemjua mimi experienced one hawezi kufungwa penalt 9 zile kwa style ile jamani.
    Haya mwingine anaongelea Mwamuzi,eti aliionyonga Simba...huyu ndo bure kabisa,Simba wenyewe(wachezaji waliokuwa kwenye pitch na Viongozi wao waliokuwa uwanjani) hawajaliona hilo,yeye aliyeko Mpiji Magohe sijui Mabwepande kaona kupitia siajabu Tv yake ya 14 inches.
    Haya mwingine anaongelea hujuma,jamani suala la hujuma nalo ni geni,hatulijui? kama ni U'tanzania wetu ndo unatufanyaga tuzikarimu team pinzani pindi zinapokuja kucheza na team zetu ni sisi,waarabu hizo ndo zao na ndo maana team nyingi zinapokwenda kule zinakwendaga zimejiandaa kikamilifu kabiliana na hizo hujuma,afterall hujuma hazichezi,kama hujuma zingekuwa zinacheza basi TP Mazembe wangetakiwa kufungwa 6 kabisa ksbb wao ndo walihujumiwa zaidi.
    Haya mwingine anambishia Mchambuzi kuwa Simba haitegemei wachezaji wachache....mimi nafikiri mashabiki wengine wapowapo tu,yeye kazi yake ni kusubiri akiulizwa unashabikia team gani aseme SIMBA SPORTS CLUB hana lolote analolifahamu kuhusu hiyo team yake,anachojua yeye ni kusoma kwenye magazeti Simba imecheza imepata matokeo gani basi,binafsi naungana na mchambuzi kuwa Simba ni kati ya team chache zinazotegemea wachezaji wachache kupata matokeo(nyingine ni kama Ruvu ilivyokuwa inamtegemea Nsa Job),na hili nimelifanyia research kabisa siongei tu kama kutapika,Mbishaji naomba arudishe kumbukumbu zake nyuma wakati Ligi hii inaanza aangalie matokeo ya Simba katika zile mechi za awali kabla Okwi hajaja(tukumbuke Okwi alichelewa sana ku'report msimu huu)Simba ilianza kutakata baada ya Mshikaji kurejea,aangalie pia hata mechi za hivi karibuni,mechi kadhaa muhimu Simba ilipata ushindi kutokana na juhudi binafsi za Okwi,nitamkumbusha chache aangalie goli lake dhidi ya Es Setiff kule Algeria,aangalia magoli ma'2 kati ya matatu dhidi ya Shandy Dar,angalia magoli yote ma'5 dhidi ya Yanga ni nani kama siyo Okwi,Okwi na Mafisango kwa kiasi kikubwa ndo wamekuwa waki'determine ushindi wa Simba kwenye mechi nyingi walizocheza msimu huu na kudhihirisha hilo ndo maana team kama team imekuwa ikishindwa hata kuwachukulia hatua pindi wanapofanya vitendo vya utovu wa nidhamu reffer kuchelewa kuja kwa Okwi bila sababu za msingi,reffer kulewa na kutoa lugha chafu kwa Kiongozi wa Simba kwa Mafisango,walishindwa kuwaadhibu,wawaadhibu halafu iweje,wangeshindaje?,hivi kweli mwenye akili timamu unaweza kubisha hili?
    Bwana Shaffih mimi naungana na yule mdau aliyeshauri uweke utaratibu wa kuchuja,maoni yenye mtindio kama ya huyo anayebisha ukweli hayapaswi kabisa kupewa nafasi.
    Big up Brother Levo,najua pamoja na kuwa Mashabiki wanapinga tathmini na ushauri wako lkn nina uhakika baadhi ya Viongozi wenye busara wa Simba wataupokea na kuufanyia kazi ushauri huu ukichukulia mwakani watashiriki Club bingwa Africa.
    Narudia tena mimi ni Neutral.

    ReplyDelete
  17. Kuna kitu sikielewi huyu mchambuzi alifikiria nini mpaka kuandika hivi kuhusu boban...?

    ReplyDelete
  18. kaka ANSELEM Kimsingi wewe nakukubali sana kwa uchambuzi huu, may God bless u! sisi sio wanazi wa yanga bali tunaongea ukweli uliotokea, kama mtu anaona tumekosea tunaomba atoe ANALYISI yake! mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki shaffii Blog

    ReplyDelete