Search This Blog

Monday, May 14, 2012

SIMBA VS SHANDY: WATANGAZAJI WA TBC NAO WAFANYIWA VITUKO SUDAN

Mtangazaji Jesse John na fundi mitambo Joseph Masanja wa Televisheni ya Taifa (TBC) walikiona cha moto kwenye uwanja wa Ndege wa  Khartoum baada ya kulazimishwa kuacha vifaa vyao vya utangazaji kwa madai  huenda ni watafiti kuichunguza Sudan.

Pamoja na jitihada za wanahabari hao kujieleza kwa kirefu dhumuni la safari yao kutangaza mechi ya Simba na Al Ahly Shandy, lakini hawakufanikiwa kuingia nchi humo na vifaa vyao.

Kwa mujibu wa John alisema walimpigia simu msemaji wa TFF, Boniface Wambura awasaidie kuwasiliana na viongozi wa shirikisho la soka la Sudan kuomba kuingilia kati ili waachiliwe vifaa vyao, lakini jitihada zao ziligonga mwamba.

"Ni msukosuko, kilichotuleta ni kutangaza mpira, sasa sijui itakuwaje, hii imekuwa ni desturi ya nchi za kiarabu,"alisema John.

Hata hivyo; watangazaji hao walipata visa ubalozi wa Sudan baada ya kupata barua kutoka Tanzania iliyoonyesha kazi ya kutangaza mpira iliyowaleta hapa Sudan.

1 comment:

  1. Kaka,
    Mi naona poa tu,mechi za ndani hapa Taifa hawatanagazagi,sasa kilichowapeleka Sudan ni nini...au P.d.m? hata hivyo sisi tunawashukuru sana StarTv kwa kutuletea mtanange ule live.
    Siyo siri hawa Jamaa(TBC) toka Mzee Tido Mhando atoke wamekuwa ovyo sana

    ReplyDelete