Search This Blog

Tuesday, May 15, 2012

RYAN GIGGS ATANGAZWA KUWA MCHEZAJI BORA WA MUDA WOTE WA PREMIER LEAGUE - HUKU BABU FERGIE AKIWA KOCHA BORA


Ryan Giggs ametangazwa kuwa mchezaji bora wa muda wote katika historia ya Premier league - huku Sir Alex Ferguson akichukua tuzo kocha bora wa Barclays Premier league history.

Fergie na Giggs wamechukua tuzo hizo wakati ligi hiyo ikisherehekea miaka 20 ya mfumo wa premier league.

Giggs ndio mchezaji aliyecheza mechi nyingi na kushinda makombe mengi ya premier league chini ya uongozi wa Sir Alex Ferguson.

Mchezaji wa zamani wa United na kocha msaidizi wa England Gary Neville alisema: "Ryan Giggs ndio mchezaji kiingereza atakayebakia kuwa aliyefanikiwa zaidi kwa muda wote na sioni mchezaji mwingine wa kuja kuzivunja rekodi zake na kumpita.

"Amevunja na kuzipita kila rekodi katika suala la kuchukua makombe ndani ndani ya mipaka ya nchi hii. Mchezaji ambaye anafurahisha kumuona akicheza kila wiki."

Wakati huo huo kikosi cha Arsenal kilichomaliza ligi bila kufungwa kimetajwa kama kikosi bora - Arsenal walimaliza ligi bila kufungwa mwaka 2003/04.

Alan Shearer alitajwa kama mfungali bora wa muda wote akiwa na magoli 260 - huku David James akitajwa kama golikipa mwenye clean sheets nyingi(173)

Neville, Giggs, na Shearer pia walitajwa kwenye kikosi bora kabisa cha premier league history.

1 comment:

  1. Uchaguzi umejaa Uingereza na Umanchester United. Its unfortunately Midfielder kama Stephen Gerard hayumo kwenye kikosi hicho. Aidha siuoni ubora wa Gary Nevile!

    ReplyDelete