Search This Blog

Monday, May 14, 2012

JOHN BOCCO NA MBWANA SAMATTA WAITWA STARS!


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.

Akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu, Kim amesema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake.

Wachezaji walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).




Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).

Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).

Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan.

11 comments:

  1. Mungu ibariki timu yetu..mungu bariki kikosi hiki.

    ReplyDelete
  2. Kaka Shaffih ahsante kwa taarifa.. Mwenzangu unazi muhimu.. hichi kikosi hakina wazee wa Jangwani?

    ReplyDelete
  3. Will this team get support on the other side of the coin?

    ReplyDelete
  4. kidogo naanza kuona mabadilko kwa kuwajumuisha vijana ili wapate cofidence na experience but tukubali kuwa wavumilivu kidogo

    ReplyDelete
  5. Hawa jamaa 5 star FC si wataizomea sana timu yetu ya Taifa.

    ReplyDelete
  6. Shaffih; huyu BOKO alitangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa, sijawahi kusikia akitangazua huo upuuzi wake vipi ameitwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa wewe mtu keshakuwekea majina yote hapo juu halafu unauliza tena, anyway kwa kukusaidia Boko kaitwa na jina lake ni la mwisho.

      Delete
  7. safi///mm like this. wish all the best the dream team

    ReplyDelete
  8. Hyo tm ya taifa imefungwa ba alshandy itaweza kina drogba kwel wap nadir harub canavaro, wap gofry taita; omega seme; juma seif kijiko; shaban kado kwa kweli zomea zomea haitakoma mpaka makocha watakapoacha unazi; unaweka yondan unaacha nadir au unaweka mkude unaacha chuji

    ReplyDelete
  9. Hii team kwa kiasi kukubwa si ndiyo iliyopigwa mwaka kule Shandy?
    Ndo tunaikabidhi jukumu la Ivory Coast,haya...yangu macho!

    ReplyDelete
  10. sasa jamani mgependa wawe yeboyebo ili watembeze masumbwi dhidi ya aivorikoost? kigezo kimojawapo ni nidhaam uwanjani, haiwezekaan kuwa hamkuwa hamjalewa nyie. iweni na busara yanga bil lipuli

    ReplyDelete