Mchezaji wa zamani wa England Gary Neville ameteuliwa rasmi na kocha mkuu kuwa mmoja wa makocha wasaidizi wa benchi la ufundi la England aka Three Lions.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, ambaye tangu kustaafu kama mchezaji msimu uliopita, amekuwa akifanya kazi katika kituo cha SkySports kama mchambuzi wa soka, amesaini mkataba wa miaka 4 na chama cha soka cha FA.
Wakati wa enzi za uchezaji wake akiitumikia England alicheza mechi 85, akiiwaikilisha 3 Lions kwenye Euro 96, Euro 2000, Euro 2004, World Cup 98 na World Cup 2006.
"Gary amefanikiwa sana katika mchezo huu akiwa mchezaji wa Manchester United na England," alisema Hodgson. "Ana vyeti vyote vya ukocha vya UEFA na nina uhakika atapata heshima kubwa sana kutoka wachezaji kutokana na uzoefu mkubwa alionao."
Neville mwenyewe aliongea: "Roy aliniita na kuniomba niwe mmoja ya walimu kwenye benchi la ufundi na kufanya nae kazi katika timu ya taifa - jambo ambalo ni heshima kwangu."
No comments:
Post a Comment