Search This Blog

Monday, April 30, 2012

YANGA SASA NI LAZIMA KUIOMBEA SIMBA DUA IINGIE KWENYE MAKUNDI YA KOMBE LA SHIRIKISHO - IKIWA INATAKA KUCHEZA MASHINDANO YA KIMATAIFA MWAKANI.

YANGA inaweza kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani, iwapo itashika nafasi ya tatu mwishoni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 
Lakini hiyo ni iwapo tu, Simba SC itafanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF). 

Hiyo ni kwa mujibu wa kanuni mpya za mashindano ya klabu Afrika za Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwamba nchi ambazo kwa sasa zina nafasi moja moja za kuingiza timu kwenye michuano ya klabu, zitakuwa zikiongezewa nafasi moja moja katika michuano ambayo klabu yake imefanikiwa kuingia hatua ya makundi. 

Kwa mfano mwaka huu Sudan imeshirikisha timu nne kwenye michuano hiyo, mbili Ligi ya Mabingwa na mbili Kombe la Shirikisho, kwa sababu msimu uliopita iliingiza timu zake kwenye hatua za makundi za michuano yote hiyo. 
Tanzania bado ina nafasi moja moja tu ambazo hadi sasa tayari Simba na Azam zimejihakikishia kucheza kwa msimu ujao. Jioni hii, Simba SC imeonyesha dalili za kuifungulia njia Tanzania kuingiza timu tatu kwenye michuano ya Afrika mwakani, moja Ligi ya Mabingwa na mbili Shirikisho, baada ya kujiwekea mazingira mazuri ya kuingia kwenye hatua ya Nane Bora ya Kombe la Shirikisho kwa kuifunga Al Ahly Shandy mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Sasa Simba inahitaji sare yoyote au kufungwa si chini ya mabao 2-0, ili kuuungana na timu nane zitakazotolewa kwenye Ligi ya Mabingwa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho. 

source: http://bongostaz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment