Wataalamu wa mambo ya masoko wametanabaisha kuwa mshambuliaji wa Real Madrid Christiano Ronaldo ana thamani kubwa kuliko mchezaji bora wa sasa wa dunia na klabu ya Barcelona Lionel Messi.
Chuo kimoja kinachojihusisha na mambo ya masoko cha IPAM kilifanaya utafiti na kugundua kuwa Ronaldo ni jina kubwa sana na linalouza sana katika masuala ya masoko.
Jina la mchezaji Ronaldo ni maarufu sana kwenye mitandao mingi sana duniani, Ana mashabiki wengi sana kuliko Messi kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook (ambapo Ronaldo ana mashabiki milioni 42 wakati Messi ana mashabiki milioni 34), kwenye mtandao wa Google Ronaldo ametafutwa zaidi ya mara milioni 139 sawa na milioni 80 zaidi ya Messi, ana jumla ya video 212,000 zilizowekwa kwenye mtandao wa Youtube,wakati kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuna watu zaidi ya milioni 8 wanaomfuata.
Umaarurfu wa Ronaldo kwenye soko unachangiwa sana na masuala ya kijamii. Nyota huyo kutoka nchini Ureno ametokea kwenye vitabu 205 vya Amazon (wakati Messi ametokea kwenye vitabu 85),pia ametokea kwenye nakala 2157 za kisayansi (wakati Messi ametokea kwenye nakala 1608). Kwenye umaarufu kama ilivyoandikwa kwenye jarida la Forbes Ronaldo anashika nafasi 47 wakati Messi anashika nafasi ya 62.
Chuo hicho cha masoko cha IPAM kinaamini Ronaldo anathamani ya €40 million kwa mwaka ukilinganisha na €37 million ya Messi kwa mwaka.
Source:http://kandanda.galacha.com
Thats why he was sold so highly...
ReplyDeleteHe deserved n performed Well wth de best form evr...