SIMBA SPORTS CLUB
P.O.BOX 15318 | TEL+255
222183330 |FAX +255 222183330 |MSIMBAZI/MCHIKICHI STREET | DAR ES SALAAM | TANZANIA
| EMAIL simbasportsclub@yahoo.com|
WEBSITE www.simba.co.tz| AFFILIATED TO TFF, DRFA and IDFA
25/04/2012
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
NDUGU waandishi.
Kama mnavyofahamu, Jumapili
ya Aprili 29 mwaka huu, timu ya soka ya Simba inakutana na klabu ya Al Ahly
Shandy kutoka Sudan katika
mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ni timu pekee kutoka
katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iliyobaki katika michuano yote
ya kimataifa inayosimamiwa na CAF.
Kubwa zaidi, ndiyo
wawakilishi pekee wa Tanzania
waliobaki katika michuano ya kimataifa na hivyo wanabeba bendera ya taifa
kokote kule waliko.
Maandalizi yote kwa ajili ya
pambano hilo
yamekamilika.
Wapinzani wetu, Al Ahly
wanatarajiwa kuwasili kesho saa saba mchana kwa ndege ya Ethiopia Airlines.
Waamuzi na Kamishina wa
mchezo wamepangwa kuwasili Ijumaa (keshokutwa) wakitokea nchini Swaziland na Rwanda.
VIINGILIO
Kutokana na ukweli kwamba
mechi hiyo itakuwa ya kimataifa, Simba imepanga viingilio ambavyo kila
mwananchi ataweza kuvimudu. Viingilio vitakuwa kama
ifuatavyo.
Viti vya bluu na kijani
itakuwa Sh. 5,000, Rangi ya Chungwa Sh, 10,000, VIP C 15,000, VIP B 20,000 na VIP
A 30,000.
Tiketi zitauzwa katika maeneo
yafuatayo, Big Bon, Benjamin Mkapa, Stears Mjini, Mbagala Dar Live, OilCom
Buguruni, Tandika Mwembeyanga, Ubungo Oilcom, Mwenge Bus Stand, BP Mwananyamala
na Gapco Ukonga.
Tiketi zitaanza kuuzwa siku
ya Ijumaa asubuhi katika maeneo yaliyotajwa.
Klabu imepokea maombi mengi
kutoka kwa wanachama na wapenzi wake kutoka mikoani na ingeomba kwamba wale
wanaotaka kuja kutazama mechi hii kwa makundi kutoka mikoani, wawasiliane
mapema na uongozi ili wanunuliwe tiketi zao mapema.
Simba SC imechapa tiketi
za kutosha na ingeomba wapenzi na wanachama wake kujitokeza kwa wingi kwenye
pambano hilo.
Wana Simba wote wanaombwa
kuja uwanjani wakiwa wamevalia mavazi yao
ya rangi Nyekundu na Nyeupe ili uwanja mzima upendeze kwa rangi hizo.
Tunatoa wito kwa vyombo vya
habari kuisaidia Simba na Tanzania
kwa kuelekeza nguvu zao katika uandishi wa taarifa ambazo zitaisaidia timu yetu
kusonga mbele na si kuondoa morali au kusababisha watu wasiende uwanjani.
Shukrani.
Uongozi wa Simba SC
unatoa shukrani, kwa namna ya kipekee kabisa, kwa serikali kutokana na uamuzi
wake wa kuruhusu Wekundu wa Msimbazi kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa
kujiandaa na mechi hii muhimu.
Ezekiel Kamwaga
Msemaji
Simba
SC
No comments:
Post a Comment