Ni lini mara ya mwisho kwa Klabu toka Tanzania kuitoa mashindanoni klabu ya uarabuni . Ni muda mrefu kidogo umepita na hii leo Simba inajikuta ikiwa na nafasi kubwa ya kutengeneza historia mpya ya kuwang'oa waarabu mashindanoni.
Haitakuwa kazi rahisi kufanya hivyo kwani siku zote unapocheza na mwarabu mpambano ni mkali balaa.
Ili simba iwatoe Entente Sportive Setif lazima kazi kubwa ifanyike ndani na nje ya uwanja na hadi sasa kwa nje ya uwanja kazi kubwa imeshafanyika . Tangu Simba iivyoingia Algeirs imepata sapotikubwa sana toka kwa Watanzania wachache waishio nchini humu na hili ni jambo ambalo limewafanya wachezaji kuwa na ari ya juu kwa kuwa hawajihisi kuwa wanyonge na hata mazingira ya wao kuweka akili zao mchezoni yamekuwa mepesi.
Uwepo wa Watanzania ambao wamesaidia kila kitu kuanzia kuhakikisha kuwa chakula wanachokula wachezaji kinasimamiwa mpaka mawasiliano ya siku hadi siku hakika mewapa wachezaji nguvu kwa kiasi kikubwa.
Historia pia ipo upande wa Simba ambapo kwa wale wanaokumbuka mara ya mwisho kwa Simba kucheza na timu ya Algeria iliweza kushinda baada ya michezo miwili miaka 18 iliyopita ilipocheza na Usma Al Harach. Pamoja na hivyo Simba imekuwa klabu pekee ya Tanzania kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa hata pale inapokutana na timu za urabuni.
Mazingira yaliyowekwa na mchezo wa kwanza hakika yataisaidia Simba kucheza mechi ya ugenini wakiwa wame-relax zaidi huku wakijua wanachotafuta .
Hata hivyo asilimia 95% kazi iko kwa wachezaji. Hawa ndio wanapaswa kutambua vita iliyoko mbele yao na ishara zote zinaonyesha kuwa wamejiandaa kwa mpambano kimwili na hata kiakili . Hata kama bahati haitakuwa upande wao basi itakuwa kwa sabau za kimchezo tu kwani wachezaji wote wako kwenye hali nzuri.
Upande wa ufundi kocha wa Simba Milovan Cirkovic anaonekana kuwa amejiandaa kuwakabili wapinzani wake kwani hana wasiwasi na hata mazoezini amekuwa akiwafundisha wachezaji wake mbinu tofauti na zile ambazo zimekuwa zikitumika siku za nyuma na timu za Tanzania dhidi ya timu za uarabuni.
Simba itashinda endapo wachezaji watashambulia dakika za mwanzo na kuwapa wapinzani wao 'element of suprise'. Kwa vyovyote Entente Sportive Setif wamejiandaa kushambulia mwanzo mwisho na hilo lilidhihirika tangu Dar es salaam ambako walikuwa wanasema kuwa wana uhakika wa kuifunga Simba mabao manne mashabiki wao mji mzima wamekuwa wakionyesha ishara ya vidole vinne wakimaanisha kuwa wataifunga Simba kwa idadi hiyo ya mabao.
Simba wanapaswa kuwa na mpango mkakati wa kuwashtukiza Waarabu hawa na kuwapa 'sucker punch' pasipo kutegemewa jambo ambalo litaufanya mchezo kuwa mgumu kwa waarabu.
Moja ya mapungufu ambayo Setif wameonekana kuwa nayo ni kuruhusu presha langoni mao hali inayowafanya wafungike mara kwa mara na hili Simba wanapaswa kulifanyia kazi.
Kama simba wakiruhusu kushambuliwa hali itakuwa ngumukwani wanaweza kujikuta wakiruhusu mabao ya mapema ambayo yataufanya mchezo kgeuka na kuwa mgumu kwao lakini haya yote yanaweza kubadilika kama Simba ikipata bao la mapema.
Pamoja na hayo wachezaji wa Simba wanapaswa kucheza kwa kutanguliza ndhamu mbele. Wachezaji hasa wale wanaocheza nyuma wanapaswa kuhakikisha kuwa hawacheza hovyo na kuepuka kupiga 'tackling' ambazo zinaweza kumshawishi mwamuzi kutoa penati au kadi.
Pamoja na hili pia wanapaswa kuwa wapole kwa maana ya kuepuka kuwa walalamishi kwa mwamuzi hali ambayo itaepusha kadi kwani tunatambua siku zote kuwa timu mwenyeji hupata 'favor' ya mwamuzi lakini favor hizi zinaweza kutokuwepo kama wachezaji watakuwa na nidhamu.
Mfumo ambao mwalimu atautumia unaweza pia kuamua mchezo, endapo Simba watacheza kwa kuwaruhusu viungo wa Setif kutawala mchezo hali takuwa mbaya, ningekuwa mwalimu ningechezesha viungo watano ili kuwamiliki waarabu ambao lazima watakuwa na wachezaji wajanja katikati ya uwanja. Mashambulizi ya kushtukiza na umiliki wa mpira utakuwa muhimu pia .
Washambuliaji wa Simba wanapaswa kuwa na njaa ya kufunga zaidi na kuongeza umakini wa kutumia nafasi chache zitakazopatikana.
Ukweli unabakia kuwa huu utakuwa mchezo mgumu sana ila Simba wana zaidi ya nafasi kubwa ya kusonga mbele endapo wachezaji watajituma na kujitoa kwa asilimia mia moja
Uchambuzi yakinifu kabisa huo ulioufanya bwana Shaffih, ulichokizungumza ni kweli kabisa ifike mahala wachezaji wetu wawe na hamu ya kuwa sehemu ya historia kwani hakuna kinachoshindikana kama wataamua kujitoa kwa asilimia 100, tatizo ni kwamba wamekuwa hawana malengo kwa kweli kazi iliyofanywa na viongozi wa simba pamoja na washabiki huko Algeria imenitia moyo sana na naungana na wewe kama Simba leo itashindwa kupigana kiume na kuitoa Setif basi lawama ziende kwa wachezaji.
ReplyDeleteBinafsi nawatakia kila la kheri simba naamini leo wataandika historia huko algeria pamoja na fitina zote ambazo waarabu huwa wamekuwa wakizitumia ndani na nje ya uwanja.
kila raheri simba watanzania 2po nyuma yao 2nawatakia ushndi kwa mech yao ya leo.eryk motown
ReplyDelete