Search This Blog

Monday, April 9, 2012

SAMATTA JUKWAANI - TP MAZEMBE WAKIWACHINJA MABINGWA WA ZAMBIA




Mshambuliaji wa kimataifa na mchezaji ghali zaidi kuwahi kuuzwa kutoka ardhi ya Tanzania Mbwana Ally Samatta leo alikuwa jukwaani kutokana na majeruhi huku timu yake ya TP Mazembe ambao ni mbingwa wa mara nne wa Afrika wakitinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya ushindi wa 6-0 dhidi ya mabingwa wa Zambia, Power Dynamos leo mjini Lubumbashi.
Hadi mapumziko, Les Corbeaux walikuwa mbele kwa mabao 4-0, Nahodha Tresor Mputu Mabi akipiga mabao matatu peke yake, hivyo kufanya ushindi wa jumla wa 7-1, baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Alikuwa ni kiungo wa Zambia, Rainford Kalaba aliyefunga bao la kuongoza dakika ya tisa, kabla ya Mputu kufunga la pili dakika ya 22.
Mshambuliaji wa Zambia, Given Singuluma naye akafunga mawili dakika ya 42 na 44.
Kipindi cha pili, Mazembe ambayo iliyocheza bila mshambuliaji wake, Mbwana Ally Samatta anayeumwa bega, waliendelea kutawala mchezo na Mputu akaongeza mabao mawili.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alifunga kwa penalti dakika ya 66 na linguine dakika sita baadaye.
Mshambuliaji wa Tanzania, Samatta aliyefunga bao la Mazembe katika sare ya 1-1 na Dynamos Kitwe, anaendelea na matibabu na labda wiki ijayo atarejea uwanjani.

2 comments:

  1. power dynamo i thnk hawa ni mabingwa wa zimbabwe sio zambia,....kazi njema wadau.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Power Dynamos ni mabingwa wa Zambia kwani hata mechi ya kwanza ilichezwa Kitwe huko Zambia ambapo Mbwana Samata alifunga goli walipotoka sare ya 1 - 1 na pia Zimbabwe kuna Dynamo vile vile...!!!

      Delete