Search This Blog

Thursday, April 12, 2012

SABABU 5 KWANINI MARIO BALOTELLI SIO WA KULAUMIWA KWA MSIMU WA CITY KUANZA KWENDA VIBAYA


Ndio ni mkorofi, anapigana mazoezini na wenzie, anagombania kupiga free kicks na wenzie uwanjani na pia anapata red cards mara kwa mara. Japokuwa makosa yake ni makubwa lakini Mario Balotelli sio sababu kubwa ya msimu wa Manchester City kwenda vibaya mwishoni mwa msimu.
 Roberto Mancini amechukua jambo hili na kumtoa kafara mshambuliaji huyu kwa kumtupia lawama ili kujaribu kulinda kibarua chake, lakini hizi ni sababu tano zinaonyesha ukweli kuhusu mambo kwenda mlama pale City.


KIWANGO CHA DAVID SILVA
Katika nusu ya kwanza yote ya msimu David Silva alikuwa akitajwa kama mchezaji bora wa ligi kuu ya England. Mhispania huyo ndio alikuwa roho ya City  akifanya maajabu wiki baada ya wiki.
Lakini baadae kuna kitu kimetokea. Labda ni majeraha au uchovu, Silva si yule wa mwanzo wa msimu, amekuwa katika kiwango cha chini katika mechi za hivi karibuni.
Baada ya Silva kupoteza kiwango, na timu nayo ikawa hivyo hivyo. Na sio jambo la kushangaza kwa kuwa mchawi huyu wa kihispania ndio alikuwa mtu muhimu katika kuuinganisha timu hii ya Roberto Mancini.


SAMIR NASRI WA CITY SIO YULE WA ARSENAL
Baada ya kufunga magoli 16 katika mashindano yote akiwa na Arsenal msimu uliopita, mashabiki wa City wanaweza kusamehewa kwa kutegemea makubwa zaidi kutoka Nasri ambaye mapaka sasa amefunga magoli 5 msimu mzima.

Anaweza akawa anawatolea maneno ya kejeli mashabiki wa Arsenal kwenye Twitter  baada ya mchezo wa wikiendi iliyopita, lakini alishindwa kufanya lolote la maana kuweza kuisadia timu yake isiepukane na kipigo.
 Lakini sasa mashabiki wa City watakuwa wameshaanza kuuona uwezo wake wa kuongea ni mkubwa kuliko kucheza soka.


SERGIO AGUERO AMEPOTEA
Sergiuo Aguero ana magoli mawili kupita magoli ya kawaida katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita. Hakika, ndio amekosa michezo kadhaa kutokana na majeraha yake ya kijinga kama anavyoyaita Mancini, lakini hicho sio kisingizio kinachotosha kwa mshambuliaji wa kariba yake.
 Muargentina huyo alifunga magoli 9 katika miezi yake mitatu ya kwanza pale Etihad.



ROBERTO MANCINI
Uwezo mdogo wa  Mancinikuweza kuwatuliza na kuwa-manage wachezaji ni tatizo ambalo limepelekea city kuwa walipo.

Kwa ufupi, kama Mario Balotelli ndio tatizo pale City, Roberto Mancini anahitaji kutafuta suluhisho. Mfano bora upo karibu yake kwa jirani yake Sir Alex Ferguson jinsi alivyoweza ku-handle ukorofi wa Rooney ambaye kwa sasa msimu huu hana kadi hata moja.

Lakini amekosa namna ya kumshugulikia au kumrekebisha Balotelli na mwishowe ndio anamtupia lawama ambazo hazina mashiko, matokeo yake timu imekosa muelekeo wala mshikamano miongoni mwa wachezaji.




CARLOS TEVEZ
Carlos Tevez aliifanya City itishe msimu uliopita. Lakini kutokana na kitendo chake cha kukataa kucheza katika champions league mwezi september kiliharibu kila kitu.
Japokuwa baada ya Tevez kufungiwa na kugoma kucheza, City waliendelea kucheza na kushinda. Then Roberto Mancini akaanza kelele za kutaka kumrudisha Carlitos kwenye timu, na hapo ndipo City walipoanza kupoteza points  na kufanya mbio za ubingwa kwa United kuwa nyepesi.

Tangu ndege ya Tevez kutoaka alipokuwa ilipotua jijini Manchester just after Valentines Day, City wameshinda mechi nne tu kati ya nane na  kupitwa points 8 na United kabla ya jana watoto wa Fergie kuteleza na kupunguza pengo hilo.

No comments:

Post a Comment