Milla |
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Cameroon, Roger Milla ameunda Kamati ya kupambana kuwaondoa madarakani viongozi wa Shirikisho la Soka nchini humo (FECAFOOT) na kumrejesha kikosini, Nahodha wa timu ya taifa, Samuel Eto'o.
Milla anahofia Cameroon, ambayo haikufuzu kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka huu, inaweza pia kukukosa fainali zijazo."Lazima tuirudishe soka yetu kwenye reli, hatua nzuri kwa sababu tunakoelekea sasa chini ya uongozi wa timu wa sasa hakuaminiki," alisema Milla baada ya kuzindua Kamati ya kuivisha tena nguo soka ya Cameroon, iitwayo COCIREFCA, Kifaransa yaani Comite Citoyen pour le Redressement du Football Camerounais.
"Hakuna anayeona kwamba tunaekelea kufeli kutoka kwenye kufeli. Hii lazima tuimalize na mambo lazima yasonge mbele.
Uongozi wa sasa wa FECAFOOT, lazima uondoke, (rais) Iya Mohamed na wenzake lazima waondoke. Soka ya haiwezi kuendelea kuongozwa kwa watekaji," alisema Milla.
Kamati hiyo imeundwa na kundi la wachezaji wa zamani, ambao wanataka kauli thabiti ya shirikisho.
Milla anaheshimika sana kwenye soka ya Cameroon, kutokana na kufunga mabao yaliyoiwezesha nchi hiyo kutinga Robo Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1990.
Eto'o alisimamishwa baada ya kuongoza uasi katika timu ya taifa kutokana na madai ya maslahi ya wachezaji, hali iliyosababishwa kuahirishwa kwa mechi ya kirafi iliyokuwa ifanyike Novemba mwaka jana Algeria.
No comments:
Post a Comment