Search This Blog

Tuesday, April 3, 2012

OFFICIAL: TFF YAIPOKA POINTI YANGA


Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeipa Coastal Union ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Yanga kumchezesha mchezaji Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwenye mechi kati ya timu hizo iliyochezwa Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Uamuzi huo ulifanywa na Kamati ya Ligi iliyokutana jana (Aprili 2 mwaka huu) kupitia ripoti mbalimbali za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza umezingatia Kanuni ya 25(f) ya Ligi Kuu ya Vodacom juu ya Udhibiti wa Wachezaji.

Kanuni hiyo inasema: “Ni lazima kwa klabu na wachezaji kutunza kumbukumbu za kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu (3) na mabao matatu (3), iwapo mchezaji atacheza akiwa haruhusiwi kucheza kwa ajili ya kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu timu yake itapoteza mchezo. Endapo klabu haina uhakika au inataka taarifa ya idadi ya kadi zake itaomba kwa maandishi toka TFF.”

Cannavaro alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kupiga kwenye mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu ambapo kwa mujibu wa Kanuni ya 25(c) ya Ligi hiyo anastahili kukosa mechi tatu. Mchezaji amekosa mechi mbili tu.

Pia klabu za Coastal Union na Yanga zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wake kutupa chupa za majini uwanjani wakati wa mechi hiyo. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 32(1).

Kamati ya Ligi pia imemuondoa Kamishna wa mechi hiyo Jimmy Lengwe kwenye orodha ya waamuzi kutokana na upungufu uliopo kwenye ripoti yake ambapo baadhi ya matukio makubwa hakuyaripoti. Moja ya matukio hayo ni kocha wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo kuzozana na mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza.

Vilevile waamuzi wa mechi namba 151 kati ya African Lyon na Simba wameandikiwa barua ya onyo kwa kupata alama za chini. Waamuzi hao ni Hashim Abdallah, Abdallah Selega, Hamis Chang’walu na Hassan Mwinchum. Naye Kamishna wa mechi namba 153 kati ya Moro United na Villa Squad, Arthur Mambeta amepewa onyo kutokana na upungufu katika ripoti yake.

3 comments:

  1. Hili soka letu sijui linaelekea wapi,kamati iliyozodolewa kwa kufanya kazi isiyowahusu hatimaye ime'revenge, imenishangaza sana mtu aliyeandika barua ya kujiuzulu aka'chair kikao cha kuipoka points Yanga,kumbe inaonekana bado anaupenda wadhifa wake,si vibaya basi akienda kwenye press na kuutangazia uma ku'withdraw resignation yake,kuna haja ya hizi kamati zikaangaliwa zinavyoundwa, Kamati ina Wawakilishi kutoka Azam (iliyo katika vita ya kutafuta 1 ya nafasi 2 za juu),Simba,Coastal sijui Africa Lyon, haki itatendekaje?
    Nawashauri Viongozi wa Yanga wapitie vifungu vyote viwili kilichowaruhusu kumchezesha na hicho walichokitumia kamati ya Ligi kuipoka points na kuchukua hatua za haraka,ikiwezekana hata kusonga Mahakamani potelea mbali kitakachotokea,huu ushakuwa ujinga sasa!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau ttzo hapo sio wanakamati unatakiwa kuwalaumu viongozi wa Yanga sbbu wanajua kanuni za ligi zinasemaje,hapa tatizo Canavaro kapew red kad straight kwa kumpiga refa na hata km akumpiga hapo sheria inabaki palepale ikigundulika tofauti refa ndio anafungiwa na hili viongozi wanalijua ttzo kubwa Yanga wenyewe wanaamini cku zote wapo juu ya sheria,khsu kwenda mahakamani viongozi wako wanaweza kufanya kufata ushauri wako cause ya upeo wenu mdogo wa kufikiri mkiamini mnaonewa wakati hamna timu ya ushindi mmebaki ubabaishaji na ubabe ktk mpira,hayo ni mawazo yangu mdau mwenzangu.

      Delete
  2. Kama kawa nasubiri maamuzi ya mzee tibaigana

    ReplyDelete