Search This Blog

Saturday, April 7, 2012

NI MAPEMA MNO KUMUHUKUMU LULU !


Na  MDAU REVO ALEXANDRIA Jr

mimi ni mwanasheria na nimefatilia sana ili sakata nawaomba
nyie kama waandishii subirini taarifa ya dakitari kuhusu
chanzo cha kifo cha kanumba. Mpaka sasa hakuna uthibitisho
kuwa Lulu alimsukuma, inawezekana kwenye purukushani
hiyo, ni Kanumba mwenyewe ali bugi step akateleza na
kuanguka bila kusukumwa na yoyote!.

Hata ...kama ni kweli Lulu alimsukuma, chanzo cha kifo sio
lazima kiwe kimetokana na kusukumwa!.

Inawezekana Kanumba alikuwa na heart problem, pressure
e...tc, hivyo alipokasirika pressure zikapanda, au akapata
heart failure ndipo akaanguka!.

Hata kama ni kweli alijigonga, subirini madaktari wathibitishe
chanzo cha kifo ndipo tuendelee kujadili!.

Najua msiba huu ni huzuni kubwa, lakini nawaombeni sana,
lets not be judgemental kwa Lulu!.

Mimi ni miongoni mwa waumini wakubwa wa the doctrine of
"karma", kuwa there is nothing new under the sun, hakuna coincidence wala bahati mbaya, lolote ambalo limetokea,
lilikuwa litokee tuu, yaani siku ya mpendwa wetu Kanumba
ndio ilikuwa imefika, saa ilipotimia Mungu akamuita, hata
asingesukumwa, angefia usingizini!.

ni vizuri jamii ikafahamu si vema kuanza kuhukumu mtu kabla
ya preliminary investigation yoyote kufanyika

After all, there is life after life and life before life!, death ni
change tuu ya life form from physical body to spiritual body!.

Rip Kanumba

21 comments:

  1. Asante sana mwanasheria walau utakuwa umesaidia kupunguza uvumi uliojitokeza miongoni mwa wanajamii wanaopenda kuweka maneno yao ya ajabux2 kila linapotokea jambo. Ukweli ni kwamba Kila nafsi itaonja Mauti"Mbele yake Kanumba Nyuma yetu" hili kwetu ni fundisho pia la kujiweka tayari wakati wote...R.I.P Kanumba The Great!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna cha kila nafsi itaonja mauti, kama ndio hivyo hata suala la kesi za mauaji zifutwe kwa kuwa kila nafsi itaonja mauti, huyu lulu lazima ashitakiwe ili iwe fundisho kwa wanawake wengine kupiga wapenzi wao, angempika kwa mabusu haya yote yasingetokea.

      Delete
  2. To be honest theirs a big difference between a european lawyer not all though and tanzanian lawyer or other european profesionals as compared to others tanzanian professionals regadless of whatever happens mostly worse we would put ourselves in a position to accept those terms as something that's happened all done to will of god, god knows best and he loves best and the best part is we would all come together regardless of ethnicity or religion we will all become one body and focus only on one thing,making sure we rightfully honour our brother towards his last journey on earth, It's this beauty that makes me appreciate and be proud of tanzanian, As a country we might suffer from malnutrition, our citizen might be poor, we might still suffer from lack of basic services such as lack of health centres, electricity, unemployment but lets be thankful to god still as always as in the eyes of the world we might be poor but he has blessed tanzanians with big and beautiful hearts and with peace, These treasures are for us to keep and cherish them down the generations. As everyday we fight to eradicate poverty, disease among our people and making sure that every household enjoys the privileges of basic services i.e clean water, health services we should also remind each other on maintaining that peace and continue being the people that we have always been when calamity befalls on us.
    Ndugu Revo no speech can better your wise and thoughtful words, As marehemu is someone who makes and directs movie am sure he would have had actors/actress sometime over runing the script and all he would do is repeating the cast until the script is spot on and we human beings are those actor/actress who think of so many things especially about this woman and your words brings us back to the script back to reality, All we can do is wait for post mortem, hear the lady version of the story of what happened that night, take our brother in his last journey, continue being the people we have always been and continue his legacy.
    Mungu ibariki Tanazania.
    Soud,London.

    ReplyDelete
  3. nashukuru sn m/sheria kwa kutoa ufafanuzi juu ya hili suala kwa kuwa inaonesha jamii ya wengi wameshindwa kutambua kuwa hiyo yote ni mipango ya Mungu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mi nafikiri Lulu bado hajahukumiwa bali anatuhumiwa kuyafanya Mauaji au kusababisha kifo cha Kanumba na ndiyo maana hadi sasa anashikiliwa na dola.Pia mwanasheria utuambie je kitendo chake huyo Lulu kabla na hata baada ya tukio nini alichokifanya maana tumeambiwa na mdogo wa marehemu kwamba mara baada ya tukio mtuhumiwa alimpatia taarifa ndugu huyo then yeye akaondoka.Je hapo ni ishara gani?Mi nafikiri taarifa ya daktari haiwezi kuonesha eti alisukumwa bali itaonesha ni kifo kimesababishwa na nini na kwanini alikufa,mazingira ya eneo la tukio yatabainishwa na polisi mara baada ya kukagua tukio nafikiri iwapo Lulu angekuwepo eneo la tukio angesaidia palepale kuelezea kilichotokea kwa hiyo hatuwezi kumuacha LULU bila kumtuhumu kuhusu kifo hiki nami nadiriki kuyaita ni MAUAJI ya Kanumba hatuwezi kutafuta neno zuri zaidi ya hilo hata kama ni mipango ya mungu ilikuwepo kwa vile yeye ni muumba wetu.Lulu ndiye causation ya kifo cha Kanumba na si vinginevyo.

      Delete
  4. Bw. Revo Alexandria Jr, tunashukuru sana kwa maelezo yako na ufafanuzi uliotoa juu ya kifo cha KANUMBA. Lakini nikukumbushe tu kuwa LULU ndo the first suspect wa kifo hiki cha THE GREAT, pili kama ikithibitika kuwa KANUMBA kafariki kutokana na Mzozo/ ugomvi kati yake na LULU hata kama awe alianguaka peke yake au ana matatizo ya kiafya yaliyopelekea kifo chake....basi LULU lazima awe na kesi ya kujibu but kwa sasa SHE IS INNOCENT. BWANA ALITOA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

    ReplyDelete
  5. Nimeamini Kusoma Haina Maana Ya Kuwa Na Elimu,Period

    ReplyDelete
  6. Nimeamini Kusoma Haina Maana ya Kuwa na Elimu

    ReplyDelete
  7. Tatizo kifo cha kanumba waandishi wengi imekuwa ndio kuzipa umaarufu blog zao,wenye mamlaka ya kutoa taarifa ni jeshi la polisi na taarifa ya daktari,hakika kwa hili lulu hajatendewa haki nanyi waandishi,mmemhukumu mapema sana na kuionesha jamii lulu ndio chanzo,tuache vyombo vinavyohusika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Lulu lazima atakuwa anahusika na kifo cha mpendwa wetu, iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi, na kisingizio isiwe eti siku zake zilifika, basi ingekuwa hakuna haja ya mtu akiua kuhukumiwa kwa kuwa siku za marehemu zilifika. Na kama alifanya hivyo kwa makusudi ina maana amemwaga damu na kama amemwaga damu atakuwa ametoa uhai wa kanumba, kwa hiyo ni lazima naye ahukumiwe. hebu angalia kama alikuwa na nia nzuri kwanini alitoroka? angekuwa na upendo na Kanumba angekimbilia polisi kuripoti na si kutoroka. inauma sana. Mimi ninaamini Mwenyezi Mungu hakupenda Kanumba afe na bali ni shetani ndio amependa na hakika Kanumba angemtegemea Mwenyezi Mungu asingejihusisha na mambo ya kina Lulu na angetafuta mchumba mmoja na akamuoa. hata hivyo namuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina

      Delete
  8. whether it is GOD's karma or not a died is dead unless we have ability to bring him back, the lawyer and doctrine believers both may be right but the doctor's report will confirm ( heart attack, cardiac arrest, brain contusion, concussion, suffocation if was strangulated during fight etc or natural death cause) all are GOD's cause let us pray for his soul AMEN

    ReplyDelete
  9. When your days arrive to go...then he has the right to take you cause he is our CREATOR...R.I.P Mr.Steven Kanumba

    ReplyDelete
  10. Lulu aliutaka ukubwa miaka mingi sana. Bila shaka sasa ameupata, wala hatouhitaji tena ukubwa mwingine. Vile vile michango na maoni kama haya pamoja na vyombo vya sheria visione sheria tu linapotokea kwa mwingine. Ningefurahi kuona na linapokutokea na mwenyewe kama vile kuuliwa mumeo, mkeo, baba au mama yako pia lionekane hivi hivi.

    ReplyDelete
  11. Uko sahihi mwanasheria, tunapaswa kuacha utamaduni wa kuhukumu kabla ya taarifa rasmi, sijui ni kwanini tunapenda kuwa, Mahakimu, Majaji, Marefa, Madaktari na hata waalimu, hata kama hatuna taaluma hizo, tuliache suala hili mikononi mwa watalaamu wa afya wao ndiyo watupe majibu.

    ReplyDelete
  12. mwanasheri kwahiyo unataka kusema hana hatia kuhusiana na hilo sakata?

    ReplyDelete
  13. Kweli angekuwa naupendo asingekimbia na kumuacha mwenzake. Ona sasa kamkimbia itakuwaje useme hana hatia? Naumkimbie mwenzakoya kumpeleka hospitali? Kweli inauma Kaeven upumzike mahali pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  14. kukimbia ama kutokimbia inategemea ubongo wako ufanyaji kazi kwa wakati ule ndio maana ajali zikitokea madreva wengi hukimbia, hata kama lulu amemsukuma kanumba pengine alikuwa anajidefence mwenyewe,ndio maana police wanapewa bunduki wanapokwenda lindoni je unaelewa maana yake, ama mtu anapomiliki bastola unaelewa maana yake?. tuache propaganda team ya madaktari imefanya kazi yake na upelelezi uendelee tusimlaumu lulu, kama ana makosa atahukumiwa kwa mujibu wa sheria ya jamhuri wa muungano wa tanzania, na kama hana kosa atakuwa huru, ila kuna baadhi ya vyombo vya habari report zao znaongeza chuki kwa watanzania dhidi ya lulu.kama lulu ndie chanzo hata kanumba mwenyewe ndio chanzo kama asinge kuwa na wivu wa simu ya mpenziwe haya yote yasingetokea.

    ReplyDelete
  15. umalaya wake umemponza alichokitaka amekipata wahenga walisema asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu maana walimwengu tumeona hiyo ndio saizi yake saa hizi anakula kwa kengele ya polisi aoge wapi ajipodowe wapi mapouda wapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimeipenda snaaaaaaaaaaaaaaa hii comment.BIG UP

      Delete
  16. kama lulu hakushiriki kifo cha kanumba kwanini? alikimbia baada ya kuona kaanguka

    ReplyDelete
  17. Tatizo wana sheria mnakuwa watumwa wa sheria hatakama mtu amekosa na vielelezo vipo mnatuambia ngoja sheria ifuate mkondo wake,hii mpaka lini?Sheria ni watu na watu ndo sheria.Lulu hastahili kuwa anapumua mpaka sasa,kwani aliyemsababishia kifo naye angependa kuwepo.Laiti kama asingelikwenda nyumbani kwa Kanumba haya yote yasingelitoke,na huyo bwana angelikuwa hai mpaka sasa.Endelezeni siasa zenu nyie wanasheria katika uhai wa watu ila jua siku ikiwakumba nyie ndo mtajua umuhimu wa mtu kuishi.Sababu za huyo msheria hazina uzito wowote kimantiki,bila Lulu hapakuwepo furukushani chumbani kwa Steven,Lakini baada ya huyo mjinga na taila asiyejifahamu na kutambua yupo duniani kufanyalipi kuingia ndo vurugu zikatikoea na mtu kufa,alafu ibilisi huyo akatoweka.Jamani siasa na ukipofu uwekwe pembeni na kwa njia yoyote ile iwe ni kwa neno ama kwa nguvu Lulu amehusika.

    ReplyDelete