Hakuna maneno tena yaliyobaki kumuelezea. Arsene Wenger alishawahi kumfananisha na kompyuta, wakati kocha wake Pep Guardiola ameshakata tamaa ya kupata maneno ya kumuelezea Lionel Messi kipindi kirefu kilichopita.
Lionel Messi inaonekana atakuwa kila siku atakuwa akitengeneza vichwa vya habari, baada ya kuvunja rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Barcelona, jana kiumbe huyu wa ajabu katika soka alifunga magoli mawili dhidi ya Real Zaragoza na kufikisha jumla ya magoli 60 kwa msimu wote huu wa 2011/12 katika michezo 50 mpaka sasa.

LIONEL MESSI | 60 GOALS IN 2011-12 |
La Liga | Champions League | Copa del Rey | Spanish Supercopa | Uefa Super Cup | Club World Cup |
38 (30 games) | 14 (9 games) | 2 (6 games) | 3 (2 games) | 1 (1 game) | 2 (2 games) |
Kwa maana hiyo sasa Messi ameweka rekodi mpya katika soka barani ulaya akiwa ndio mchezaji wa pili kufikisha magoli 60 au zaidi katika ligi kubwa zote barani ulaya, akimfuata mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Ujerumani Gerd Muller aliyefunga magoli 67 katika msimu mmoja takribani miaka 40 iliyopita, akiwa anaichezea klabu ya Bayern Munich.
hakuna tena superlative kwenye mpira ambayo utaweza kuitumia kudescribe Leo. Nadhani kuna maximum of 12 games,mininmum 11 games left for Barca msimu huu, provided he stays injury free and plays in every match of which he will he's on course to equal Gerd Muller 72-73 season european tally and even set new record. Huyu ndio king Leo never stops to astonish by doing what looks the impossible.
ReplyDelete