Jumla ya timu 14 ambazo zinatakiwa kushiriki ligi ya mkoa ambayo ilipangwa katika makundi matatu Timu zilizogawanywa katika makundi matatu na kundi lililokuwa na matatizo lilikuwa na timu ya Small Prison, African Sports , Segera FC , Air Shooting na Lushoto Shooting.
Timu ya Segera FC ndio ilionekana ni dhaifu katika kundi hilo ambapo mchezo wake wa kwanza ilifungwa mabao 2 kwa 1, mchezo wa pili walicheza dhidi ya Air Shooting wakafungwa mabao 4 kwa 1 na katika mchezo wa tatu dhidi ya Small Prisons ikafungwa mabao 5 kwa 1.
Mchezo uliokuja kuleta kasheshe ni baina ya African Sports dhidi ya Segera FC ambao ndio ulikuwa mchezo wa mwisho katika kundi hilo na hivyo African Sports waliingia uwanjani huku wakijua wanatakiwa kumfunga Segera FC mabao 5 kwa 0 ili waweze kuongoza kundi hilo na kwenda hatua inayofuata kwani kila kundi linatakiwa kutoa timu moja tu.
Kutokana na utafiti niliofanya na kuzungumza na baadhi ya wadau nikaelezwa kwamba African Sports waliwafuata Segera na kutaka kuwapa shilingi laki 3 ili waweze kupata idadi ya mabao 5 lakini Segera walikataa na kusema wao wanataka wakacheze na mwenye uwezo basi apate ushindi.
Baada ya Segera kukataa wahusika wakaambia kama mmekataa basi huu mzigo atapewa mwamuzi wa mchezo , lkn hapakuwa na uhakika kama huo mzigo kweli alipewa mwamuzi wa mchezo huo.
Sababu ya Segera FC kugomea mchezo dhidi ya African Sports wakati tayari wameshafungwa mabao 3 kwa 0 ni kutokana na maamuzi mabaya ya mwamuzi wa mchezo huo ambaye alikuwa Isihaka Shirikisho kwa kudai kwamba ndani ya dakika 30 mwamuzi alishatoa penati ambayo wanadai sio halali na mazingira ya mabao mengine
No comments:
Post a Comment