Nikiwa kama mdau mkubwa wa mchezo wa soka hapa nchini,najitokeza leo kuzungumza machache kuhusiana na uendeshaji wa soka hapa mkoani Tanga.
Hebu naombeni mtufahamishe sheria inasemaje kuhusu suala la mchezaji kuhama kutoka timu moja hadi nyingine. kuna mchezaji anaitwa Ignas Mangale Babu ameichezea timu ya Maisha fc ya hapa Tanga baadaye akahamia timu ya Korogwe united bila ya kufanya uhamisho,Sasa kwenye mchezo wa nusu fainal kati ya korogwe na African Sports mchezaji huyo alichezea korogwe baada ya mchezo African Sports walikata rufaa na vielelezo vyote vipo mpaka michezo aliyochezea timu ya Maisha Fc.
Lakini katibu wa mkoa Beatric Mgaya anagoma na kupindisha sheria kwa kuwa yeye anatoka wilaya ya Korogwe, hivyo anaitetea kwa nguvu zoite timu ya wilayani kwake eti mchezaji huyo hakutia saini ya dole gumba na sahihi ya mkono wake kwenye fomu , sasa leseni ameipata wapi ya kuchezea na michezo hiyo aliyocheza alicheza kwa kanuni zipi. Je hebu uhalali upo wapi kama mchezaji amechezea timu na leseni anayo na hakutia sahihi ya dole gumba wala ya mkono je huyo ni mchezaji huru? na aliweza vipi kuchezea timu hiyo?hayo yalikuwa maelezo yake ya siku ya jana na kutupigia simun viongozi wa African Sports twende tukachukue pesa yetu ya rufaa ama italiwa bure sisi kama viongozi tulikataa na kukaa kimya.
Leo yule mchezaji alikuja na kukiri kuwa alitia saini ya dole gumba mbele ya kiongozi wa timu ya maisha , na pia akakiri kuichezea timu hiyo ya maisha msimu wa ligi ya mwaka 2010-2011.Baada ya melezo ya kipa huyo kibao kikabadilika viongozi wa chama hicho cha soka mkoani hapa wakiongozwa na kaimu katibu mama Beatric Mgaya wakasema mchezaji huyo yupo huru kwa kuwa timu ya maisha haikushiriki ligi msimu uliopita.
Baada ya kuwa wakali ikabidi waiite kamati ya rufaa na usuluhishi, nao wakawa na msimamo huo huo kuwa mchezaji huyo yupo huru kwa kuwa timu hiyo haikushiriki ligi.Tukawaambia kamati ya rufaa kuwa chama hiki hiki waliwapokonya ushindi timu ya Jogoo Fc na kuwapa Jeshi kange kwa kosa la kumtumia mchezaji wa timu ya Maisha Rafael Cosmas ,pili sisi African Sports tuliwahamisha wachezaji wawili kutoka timu ya Maisha na kulipa ada ya uhamisho kwa chama cha soka wilaya ya Tanga na pia Chama cha soka mkoa wa Tanga sasa kama kweli timu hiyo ya Maisha ilikuwa haipo hai mbona pesa za ada za uhamisho walitutoza na wakatwambia hatuwezi kuwatumia wachezaji hao mpaka tupate uhamisho kutoka timu ya maisha wachezaji ambao tuliwahamisha na kulipa ada waliokuwa wanachezea timu ya maisha ni [Ramadhani Hamidu pamoja na Kasidi].
Baada yamvutano na kamati ya rufaa iliyokuwa na wajumbe kama mzee John Lyimo , mwanasheria wa halmashauri ya jiji la Tanga bwana Mramba na Mwita Waisaka, wakakirina wazi kuwa wao pia hawakupewa taarifa sahihi na suala la kama kuna timu huko nyuma ilikwisha pokonywa pointi kwa sababu ya kumtumia mchezaji wa timu hiyo ya Maisha ndio wanalisikia leo, na pia suala la African Sports kulipa ada ya uhamisho kwa timu ya Maisha nalo ni geni kwao kwani sheria inasema timu hiyo ya Maisha haikushiriki ligi hivyo wachezaji wote wapo huru.
Mwisho wa yote kamati ya rufaa na usuluwishi ikaamua kusimamisha fainal ya ligi ya mkoa ambayo ilikuwa ifanyike hapo kesho mpaka watakapotoa uwamuzi wa suala hili na wakasema watawataka TFF mkoa wapeleke vielelezo na kanuni gani waliitumia kuipokonya Jogoo ushindi kumbe wachezaji wote wa timu ya Maisha wapo huru.
Ila nakunong'oneza uchaguzi unakuja wa Tff Mkoa watu wanataka kura za vijijini waendeleze ufalme wao wa kulitawala soka la nchini hihi.
WAKO AFISA HABARI WA AFRICAN SPORTS
Said Karsandas Pandaram
No comments:
Post a Comment